Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefungua rasmi Ofisi
ya Kanda mpya ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na
Shinyanga ambapo makao makuu ya kanda hiyo yatakuwa Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama
amesema mamlaka hiyo imeanzisha Kanda Mpya ya Ziwa Mashariki inayojumuisha
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ili kusogeza huduma kwa wananchi na kuharakisha
ukuaji wa uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
Amesema ofisi hii itajishughulisha na usajili wa
maeneo yanayo jihusisha na uzalishaji na uuzaji wa chakula, dawa, vipodozi na
vifaa tiba, kupokea maombi ya usajili wa bidhaa za vyakula vinavyofungashwa,
kufanya ukaguzi wa bidhaa za vyakula katika soko kuwalinda walaji na kudhibiti usindikaji wa chakula dawa na
vipodozi.
Kazi nyingine zitakazofanywa na kanda hii ni kutoa
vibali vya uingizaji nchini na usafirishaji wa chakula nje ya nchi, kufanya ufuatiliaji
wa bidhaa za vyakula katika soko, kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa, vipodozi
na vifaa tiba pamoja na kuelimisha na kutoa taarifa kwa wadau na wananchi kwa
ujumla kuhusu bidhaa zinazothibitiwa na mamlaka.
Aidha, Mwasulama amesema Ofisi ya kanda hii
itatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, ambapo wataalam waliopo kwenye wilaya, manispaa, miji na majiji
watasimamia sheria ya chakula na dawa kwa mujibu wa kanuni ya kukasimu baadhi
ya majukumu na madaraka ya TFDA katika
Halmashauri.
Akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa wa Simiyu na
TFDA katika ufunguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni
vema Taasisi nyingine zinazohitajika katika uwekezaji wa viwanda na maeneo
mengine ya uwekezaji zikaiga mfano wa TFDA kwa kusogeza huduma karibu na wananchi ili waweze
kupata huduma kwa wakati.
“Hiki kilichofanywa na TFDA ni vizuri taasisi
nyingine nazo ziige, kama leo TFDA ipo Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki ningetamani
kuwaona TBS, NEMC, OSHA wako Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki na Taasisi
zote ambazo kwenye uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya uwekezaji zinakuwa
karibu na maeneo ya kutolea huduma” alisisitiza Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa watumishi
wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaotekeleza majukumu waliyokasimiwa na TFDA kufanya
majukumu hayo kwa mujibu sheria huku akiwaasa kuacha tabia ya kufungia biashara za wananchi
bila kuwaelimisha badala yake wawasaidie kuwapa elimu ili wazalishe bidhaa bora
kwa walaji.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Dkt. Mike Mabimbi akizungumza kwa niaba ya waganga wakuu wa wilaya ambao ni Makatibu
wa kamati za ukaguzi wa chakula na dawa amesema watahakikisha wanasimamia
utekelezaji wa majukumu wanayokasimiwa na
TFDA na akashukuru TFDA kusogeza huduma karibu na wananchi.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya
Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa
Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Meneja wa Mamlaka
ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama akitoa
taarifa fupi ya uanzishwaji wa Kanda
hiyo itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, katika uzinduzi waa kanda hiyo uliofanyika
Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wataalam wa
mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) wakifuatilia masuala
mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea katika Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka
hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga
na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019
Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi, wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya
Chakula na Dawa(TFDA) wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa
yanaendelea katika Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki
itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa
Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na
Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama mara baada ya kuzindua
rasmi Kanda ya Ziwa Mashariki ya Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga,
Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Mganga mkuu wa
Mkoa, Dkt. Mugune Maeka akitoa neno la shukrani
mra baada ya kuhitishwa kwa uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Mashariki ya
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na
Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya
Chakula na Dawa(TFDA) mara baada ya
Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini,
Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya
Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa
Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya
Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa
Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Meneja wa Mamlaka
ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama akitoa
taarifa fupi ya uanzishwaji wa Kanda
hiyo itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, katika uzinduzi waa kanda hiyo uliofanyika
Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment