Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye
ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kuendelea kufanya ukaguzi wa kinga
na tahadhari ya moto kwa shule zote za mabweni
nchini kujiridhisha ikiwa zimezingatia ushauri wa kitaalam katika ujenzi wa
majengo, kwa lengo la kuepusha majanga ya moto yanayogharimu maisha ya watu na
mali.
Andengenye
ametoa maagizo hayo Juni 19, 2019 Mkoani Simiyu wakati
akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na
sekondari za Mjini Bariadi katika shule ya sekondari Simiyu, katika Halmashauri
ya Mji wa Bariadi.
Akizungumza na wanafunzi Kamishina Jenerali
Thobias Andengenye amesema kumekuwa na matukio ya moto katika shule kadhaa za
bweni ambayo yameleta athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo kwa
wanafunzi, kuteketea kwa mali, hivyo jeshi la zimamoto na uokoaji linaendelea
kuweka mikakati ya kukabiliana na majanga hayo.
Amesema mikakati hiyo ni pamoja na kusogeza
huduma za zimamoto karibu na wananchi kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya
moto katika majengo, kusoma ramani za majengo na kuanzisha klabu za zimamoto
katika shule, ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujua vitu vya kufanya na vya
kuepuka na uwezo wa kukabili moto katika hatua za awali na kuuzima.
Katika hatua nyingine Andengenye amewataka
wamiliki wa shule kuzingatia ushauri wa kitaalam unaotolewa na wataalam wakati
wa ukaguzi juu ya namna ya kufanya mabweni , madarasa na ofisi ziwe salama kwa
kuwasilisha michoro ya majengo hayo katika Ofisi za Zimamoto
ili ushauri wa kitaalam uweze kutolewa.
“Niwaombe wanaomiliki shule wazingatie ushauri
wa kitaalam unaotolewa, wazingatie ujenzi unaofuata ushauri wa
kitaalaam kwa kuwasilisha michoro kama wanataka kujenga mabweni,
kuongeza madarasa au kuongeza vyumba vya ofisi basi wazingatie ushauri ili
majengo yanayojengwa yawe salama zaidi” alisema.
Aidha, amewaasa wananchi kuacha kuweka mitungi
ya gesi ndani na kutikisa mitungi ya gesi kama njia ya kufahamu kiasi cha gesi
kilichopo; kwa kuwa kunaweza kusababisha moto na kushauri kuwa njia sahihi ya
kupima kiasi cha gesi katika mtungi ni kuweka mtungi katika maji, ambapo baada
ya kuutoa sehemu isiyo na gesi itaonekana kuwa kavu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kutumia gesi, hivyo ameshauri
Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuendelea kutoa elimu katika mikusanyiko ya watu
na kupitia vyombo vya habari kuhusu dhana ya matumizi sahihi ya gesi
ili kuepusha majanga ya moto.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga amelishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji kutoa elimu kwa
wanafunzi na akawataka wanafunzi wote waliopata elimu hiyo kuwa mabalozi katika
maeneo yao wanayoishi.
Magreth Sonda mwanafunzi wa kidato cha pili
shule ya sekondari Simiyu ameshukuru kupata elimu ya tahadhari na kinga dhidi
ya moto na kuahidi kuwa yeye pamoja wanafunzi wenzake watakuwa mabalozi wa
kueneza elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka ili kuepusha majanga ya moto ambayo
yana athari nyingi ikiwemo vifo na kuteketea kwa mali.
MWISHO
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akiweka kizimia moto katika moja ya
vyumba vya madarasa katika shule inayotarajiwa kuwa shule ya wanafunzi wenye
vipaji vya michezo Simiyu Sekondari, wakati wa ziara yake Mjini Bariadi Mkoani Simiyu,
Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
(kushoto) akimtambulisha Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina
Jenerali Thobias Andengenye kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari za Mjini Bariadi kabla ya kuzungumza nao juu ya kinga na tahadhari ya
majanga ya moto wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
Kamishina Jenerali Thobias Andengenye na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka wakiwasha moto kwa ajili ya kuwaonesha wananchi namna ya kuzima moto
pindi moto unapotokea, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya
shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi
ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia)
akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias
Andengenye kukagua moja ya mabweni yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya
Simiyu, wakati alipotembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa baadhi ya
shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi
ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimuongoza Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye
kukagua moja ya mabweni yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu,
wakati alipotembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule
za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya
majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Askari wa jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu,
akimuelekeza mmoja wa wanafunzi namna ya kuzima moto wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye katika shule
ya Sekondari Simiyu, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
Kamishina Jenerali Thobias Andengenye(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake
Mkoani hapa Juni 19, 2019.
Askari wa jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu,
akimuelekeza mmoja wa wanafunzi namna ya kuzima moto wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye katika shule
ya Sekondari Simiyu, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye
tai) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali
Thobias Andengenye madarasa kuona namna yalivyojengwa na namna vizimia moto
vinayoweza kuwekwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea
shule hiyo akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu,
Maulo Kigahe wakishangilia mara baada Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye
kufunga kizimia moto kilichopo kushoto, katika moja ya madarasa katika Shule ya
Sekondari Simiyu, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye
tai) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali
Thobias Andengenye madarasa kuona namna yalivyojengwa na namna vizimia moto
vinayoweza kuwekwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea
shule hiyo akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi
ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, wakati alipofika mkoani hapa kufanya ziara Juni 19,
2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini
Bariadi, kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
Kamishina Jenerali Thobias Andengenye, alipotembelea shule ya sekondari Simiyu,
akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.

0 comments:
Post a Comment