Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mikoa ya Arusha na Geita
wamewapongeza viongozi Mkoani Simiyu kwa ubunifu waliofanya kuanzisha kambi za
kitaaluma kwa ajili ya kuongeza ufaulu na kutoa wito kwa viongozi wengine kuiga
ubunifu huu ili waweze kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao.
Hayo
yamesemwa na Ndg. Anna Agatha Msuya Mjumbe wa NEC (Arusha) na Ndg. Idd Kassim Idd
Mjumbe wa NEC(Geita) mara baada ya kutembelea wanafunzi wa Kidato cha Sita
mwaka 2019 walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa, mara baada ya viongozi hao kuungana na Mjumbe wa
NEC kutoka Mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga kukabidhi msaada wa
chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
Akizungumza
mara baada ya msaada wa chakula kukabidhiwa Ndg. Anna Agatha Msuya amesema
laiti kambi hizi zingekuwa zinafanyika katika maeneo mengi matokeo ya Mitihani
hususani ya Taifa yangekuwa mazuri zaidi ya sasa kwani zimeonekana kuusaidia
mkoa wa Simiyu kupanda kielimu.
“Nimevutiwa
na ubunifu wa Simiyu kuwa na kambi za kitaaluma, tungekuwa na matokeo mazuri
kama tungekuwa na viongozi wa Serikali wabunifu kama hapa Simiyu, naomba
tulichokiona Simiyu kifanyike na mikoa mingine; mwaka juzi walikuwa wa 26
Kitaifa, mwaka jana wakawa wa 10 na naamini kwa kambi hii hatutaikosa Simiyu
katika mikoa mitano bora” alisema Anna Agata Msuya.
Naye Ndg.
Idd Kassim Idd Mjumbe wa NEC(Geita) pamoja na kupongeza juhudi za mkoa wa
Simiyu katika elimu, ameahidi kuwa amejifunza kupitia kambi hiyo ya kitaaluma
na kulichukua wazo hilo kwa jili ya kushauri viongozi wa mkoa wa Geita kuona
namna ya kulifanyia kazi ili kuwa na ufaulu mzuri.
Aidha,
Mwl. Ezekiel Mollel mwekezaji katika Sekta ya Elimu amesema suala la kambi za
kitaaluma ni la kipekee kwa mkoa wa Simiyu, hivyo akatoa wito kwa mikoa mingine
kuiga huku akiwaomba wadau mbalimbali wa elimu kuendelea kuchangia mahitaji
mbalimbali ya wanafunzi walio katika kambi ili waweze kujifunza kwa amani
wakiwa na mahitaji ya msingi.
Kwa
upande wake Mjumbe wa NEC kutoka Mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga amesema
ametimiza ahadi yake ya kutoa kilo 1000 za mchele na kilo 400 za maharage kwa
wanafunzi wa kidato cha Sita na kueleza matarajiao ya wana Simiyu kwa wanafunzi
hao kuwa, ni kuwaona wanasoma kwa bidii na hatimaye waifanye Simiyu kuwa ya
kwanza Kitaifa mwaka 2019.
Wakizungumza kwa niaba ya
wanafunzi wenzao wa kidato cha Sita mwaka 2019 walioko kambini Hidaya
Simba(Maswa Girls) na Masanja Ng’hwenu (Meatu) wamewashukuru viongozi hao kwa
msaada wa chakula walioutoa na kuahidi kuwa shukrani yao kubwa kwa walimu,
viongozi, wazazi na wadau wa elimu wanaowasaidia ni kufanya vizuri na kuifanya
Simiyu iwe nambari moja.
Pamoja na kilo 1000 za mchele na
kilo 400 za maharage zilizotolewa na Mjumbe
wa NEC (Simiyu), Ndg. Emmanuel Gungu Silanga, Ndg. Idd Kassim Idd Mjumbe wa
NEC(Geita) ametoa kilo 200 za mchele, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu ametoa kilo
100, Mdau wa Elimu Ezekiel Mollel kilo 50 na Ndg. Anna Agatha Msuya Mjumbe wa
NEC (Arusha) ameahidi kutoa zawadi kwa wanafunzi watakaopata daraja la
kwanza(divion one)
MWISHO
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga
(katikati mbele), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa wa Arusha, Ndg.
Anna Agatha Msuya(wa sita kushoto mbele) wakiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali na wanafunzi wa kidato cha Sita mwaka
2019 Mkoani Simiyu, wakati wa
makabidhiano ya chakula (mchele na maharage), kilichotolewa na Ndg. Emmanuel Gungu Silanga
na Wajumbe wenzake wa NEC na baadhi ya viongozi CCM mkoa kwa wanafunzi hao
walio katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa .
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga akizungumza
na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kabla ya kukabidhi msaada wa chakula
kwa ajili ya wanafunzi hao Aprili 11,
2019.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya akizungumza na
wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, alipotembelea shuleni hapo wakati
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu
Silanga na viongozi wengine walipokabidhi msaada chakula kwa wanafunzi hao
Aprili 11, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato
cha Sita walio katika Kambi ya Kitaaluma katika Shule ya Sekondari Maswa, wakifurahia
masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na Viongozi mbalimbali wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) na Mkoa wa Simiyu, waliofika shuleni hapo kwa
ajili ya kukabidhi msaada wa chakula na kuzungumza na wanafunzi hao Aprili 11,
2019.
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka Mkoa wa Geita, Ndg. Idd Kassim Idd akizungumza na
wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, alipotembelea shuleni hapo wakati
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu
Silanga alipokabidhi msaada wa kilo 100 za mchele na kilo 400 za maharage kwa
ajili ya chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya akimpongeza mmoja wa
wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kutoa maneno ya
shukrani kwa baadhi ya viongozi mbalimbali wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC
na Mkoa wa Simiyu waliofika shuleni Aprili 11, 2019 hapo na kutoa msaada wa chakula.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya(katikati)
akizungumza jambo na baadhi ya viongozi na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka
2019 walio katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa, allipotembelea shuleni hapo Aprili 11, 2019.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa(NEC) kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya(katikati)
akizungumza jambo na baadhi ya viongozi na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka
2019 walio katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa, alipotembelea shuleni wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga alipokabidhi msaada wa
gunia 10 za mchele na gunia mbili za maharage kwa ajili ya chakula na baadhi ya
viongozi wengine wa CCM (NEC) na Viongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu pia
walipokabidhi msaada wa chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
Baadhi
ya Viongozi wa CCM Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) na CCM Mkoa wa Simiyu na
baadhi ya walimu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa msaada wa
chakula kwa wanafunzi wa Kidato cah Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya
Kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mdau wa Elimu wa Mkoa
wa Simiyu ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Nyamagana, Bi. Flora Magabe akizungumza
na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, alipotembelea shuleni hapo wakati
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka mkoa wa Simiyu, Mhe.
Emmanuel Gungu Silanga alipokabidhi msaada wa gunia 10 za mchele na gunia mbili
za maharage na viongozi wengine walipokabidhi msaada wa chakula kwa ajili wanafunzi
hao Aprili 11, 2019.
Kutoka kushoto ni Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka mkoa wa Simiyu, Mhe. Emmanuel Gungu
Silanga, Ndg. Idd Kassim Idd Mjumbe wa NEC(Geita), Katibu Tawala Wilaya ya
Maswa, Bw. Godwin Chacha, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka Mkoa
wa Arusha, Mhe. Anna Agatha Msuya na Mwl. Ezekiel Mollel mwekezaji katika Sekta
ya Elimu wakiwa katika mazungumzo kabla ya zoezi la makabidhiano ya msaada wa
chakula cha wanafunzi walio kambi ya kitaaluma wilayani Maswa.
0 comments:
Post a Comment