Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la
Waadventista Wasabato(ATAPE), kinakusudia kuwekeza katika ujenzi wa mradi wa
maji kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi
na ujenzi wa hosteli ili kutoa huduma za
malazi katika Mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Freddie
Manento, Aprili 17, 2019 wakati
alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Kusekwa Memorial Mjini Bariadi, ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama
hicho kwa takribani siku saba ambao umeanza Aprili 16 na utahitimishwa Aprili
21, 2019.
Manento amesema ATAPE imedhamiria kuwekeza kwenye miradi
itakayokuwa na tija kwa Watanzania wote kwa ujumla huku akieleza kuwa timu ya
wataalam wa uwekezaji wa chama hicho inaendelea kufanya utafiti, ili kubaini
eneo litakalofaa kuchimba kisima cha maji na kujenga hosteli mkoani Simiyu.
“Tumedhamiria kuacha alama katika Mkoa wa Simiyu
kupitia mkutano wetu wa 20 wa ATAPE, tumepewa fursa ya kiwanja kwa ajili ya
kujenga hosteli katika kukabiliana na changamoto ya malazi, lakini pia wataalam
wetu wanaendelea na utafiti kubaini mahali tutakapochimba kisima kwa ajili ya
huduma ya maji kwa Wanasimiyu” alisema Manento
Pamoja
na miradi hiyo inayotarajiwa kutekelezwa mkoani Simiyu, Manento amesema ATAPE imewekeza
katika kilimo kwenye mashamba ya miti, miwa, mikorosho, miti ya maparachichi
ambayo kwa ujumla yana ukubwa wa ekari 10,000 na ekari zaidi 3500 ambazo
zinatarajiwa kufanyiwa uwekezaji mwingine.
Amesema hadi sasa ni takribani shilingi bilioni 1.039
imewekezwa katika miradi hiyo ambayo pia imechangia kutoa ajira za kudumu na za
msimu kwa Watanzania walio katika maeneo yenye miradi hiyo, huku akibainisha
kuwa katika baadhi ya maeneo hayo ATAPE imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa
miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii husika.
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa ATAPE ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu
hususani Bariadi kutumia mkutano huo kama fursa kiuchumi kupitia biashara ya bidhaa
na huduma mbalimbali ikiwemo usafiri wa kuwatoa na kuwapeleka wajumbe katika
eneo la mkutano.
Kwa
upande wao baadhi ya wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu wamesema Mkutano wa ATAPE
umekuwa fursa kwao kwa kuwa utawasaidia kujiingizia kipato na kupata ujuzi mpya
kupitia huduma na bidhaa zitakazouzwa kwenye mkutano huo.
“
Binafsi ninashukuru uwepo wa mkutano huu, mimi kama mjasiriamali nimepata pesa,
nimepata ujuzi mpya kutoka kwa wenzetu waliotoka nje ya Simiyu, hivyo
ninaendelea kuwaomba viongozi wetu waendelee kutuletea matukio kama haya ili tupate
pesa zaidi” alisema Bw. John Bubinza mjasiriamali kutoka Bariadi.
Nao
wajasirimali wanaoshiriki katika mkutano huo kutoka nje ya mkoa wa Simiyu wametoa
wito kwa Wananchi mkoani Simiyu kufika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kusekwa
Memorial kujifunza na kujionea kazi mbalimbali za ujasirimali ili waweze kupata
ujuzi na maarifa mapya ya kufanya kazi za ujasiriamali kwa ufanisi na kununua
bidhaa mbalimbali.
“
Binafsi nawakaribisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu kufika katika viwanja hivi
waje wajionee, wakifika hapa watapata bidhaa kwa bei za jumla na rejareja,
laikini pia nawasisitiza wanawake wainuke waje waone maana ujasiriamali
unatuinua sana wanawake” alisema Mjasiriamali Esther Jichogo kutoka Jijini Dar
es salaam.
Wanachama
zaidi ya 1500 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato(ATAPE) wanaendelea na mkutano wao wa 20 mkoani Simiyu, ukiwa na Kauli
mbiu “KUSONGA
MBELE NA MUNGU” ambao utachukua takribani siku saba kuanzia tarehe 16/04/2019 hadi 21/04/2019.
MWISHO
Mwenyekiti
wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania (ATAPE), Freddie Manento akizungumza na waandishi wa habari katika
Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako
unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mkoani Simiyu kuanzia
Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la
Waadventista Wasabato, ukanda wa AfrikaMashariki na Kati(nchi 11), Mchungaji
Emanuel Pelote akizungumza na Wanachama wa Wanataaluma na Wajasiriamali wa
Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE) katika vipindi maalum
vinavyoendelea katika Mkutano wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya
Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16
hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya Wanachama wa Wanataaluma
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE) wakiwa
katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano mkuu wa Chama hicho
unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania (ATAPE), wakiwa katika vipindi maalum vinavyoendelea katika
Mkutano wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa
Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya wananchi wakinunua bidhaa
mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali ambao ni Wanachama wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania
(ATAPE), katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini
Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mkoani
Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Bi. Jusline Gilbert mkazi wa Bariadi
akaingalia baadhi ya bidhaa za Wajasiriamali ambao ni Wanachama wa Chama
cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania (ATAPE), katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial
Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa Chama hicho Mkoani Simiyu
kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya mabanda ya watoa huduma
mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini
Bariadi ambako unaofanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama
cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019
Baadhi ya
mabanda ya watoa huduma mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkubwa wa hicho
unaofanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani
Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019
Baadhi ya mabanda ya
watoa huduma mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa
Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili
21, 2019.
Mpambaji na
mjasiriamali kutoka Bariadi, Bw. John Bubinza akiendelea na upambaji wa mabanda
ya maonesho ya bidhaa za wajasiriamali, katika Viwanja vya Shule ya Sekondari
ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili
21, 2019.
Baadhi
ya wananchi Mjini Bariadi wakinunua bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali
ambao ni Wanachama wa Chama cha Wanataaluma
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), katika
Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako
unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama
hicho unaofanyika Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Mjasiriamali kutoka
jijini Mwanza akiwaelezea waandishi wa habari juu ya viazi lishe katika Viwanja
vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika
Mkutano mkubwa wa hicho unaofanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani
Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya wananchi
Mjini Bariadi wakipata maelezo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali
ambao ni Wanachama wa Chama cha Wataaluma
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), katika
Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako
unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama
hicho unaofanyika Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya watoa huduma
za mawasiliano walio katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial
Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili
21, 2019.
Baadhi ya Wanachama wa Wanataaluma
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE) wakiwa
katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho
unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
0 comments:
Post a Comment