Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony
Mtaka amezindua rasmi kambi ya
kitaaluma kwa Wanafunzi wa Kidato
cha sita kwa mwaka 2019 yenye wanafunzi 1166 na kuagiza taa zisizimwe usiku ili
wanafunzi waweze kupata nafasi ya kujisomea zaidi.
Mtaka ametoa agizo hilo , wakati
akizindua kambi hiyo kwa wanafunzi 1166 wa kidato cha
sita na walimu mahiri 34 kutoka shule 12 za mkoa wa Simiyu, inayofanyika katika shule ya sekondari ya wasichana ya Maswa.
Amesema ili mkoa wa SIMIYU uweze kushindana kiuchumi unapaswa kufanya mageuzi makubwa ya kielimu, hivyo elimu ni kiupaumbele cha mkoa ambapo ameagiza katika kipindi chote cha kambi wanafunzi waruhusiwe kusoma bila kuzimiwa taa darasani.

Katika
hatua nyingine Mtaka amewahakikishia wanafunzi na walimu upatikanaji wa mahitaji
yote muhimu wawapo kambini, ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama, upatikanaji
wa chakula, maji, umeme, mahitaji mengine na kueleza kuwa tayari viti vipatavyo
1000 vimeshanunuliwa kwa ajili ya kambi hiyo.
Aidha,
ameahidi kutoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi, walimu na shule itakayofanya
vizuri katika mtihani wa kidato cha Sita mwaka 2019 “Ofisi yangu itatoa zawadi
ya shilingi milioni tatu kwa mwanafunzi atakayepata ‘division one ya point
tatu’ atakayepata ‘division one ya point 4 na 5’ atapata shilingi laki tano;
shule itakayokuwa katika kumi bora Kitaifa itapata shilingi milioni tano”
alisema.
Kuhusu
walimu watakaofanya vizuri katika masomo yao, Mtaka amesema mwalimu atapata
zawadi ya shilingi elfu 50 kwa kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake,
huku akiahidi pia kutoa shilingi milioni 12 kwa ajili ya posho ya walimu walio
kambini.
Kwa upande wao Afisa Elimu Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Ernest Hinju na Mwenyekiti wa wakuu wa shule mkoa wa Simiyu, Mwl.
Amede Ndonje wamekiri kuwa kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza
ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita kutoka nafasi ya 26 mwaka
2017 hadi nafasi ya 10 mwaka 2018 na kwa kidato cha nne kutoka nafasi ya 11
mwaka 2017, hadi kufikia nafasi ya tisa mwaka 2018.
Baadhi ya walimu mahiri na wanafunzi wa Kidato cha Sita wametoa maoni yao kuhusu
kambi “Tuna malengo ya kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana, kambi ya mwaka jana
ilikuwa kwa siku chache tu sisi tumepewa siku 28 nina uhakikika tutazitumia
vizuri na tutahakikisha mkoa wetu unakuwa wa kwanza” MkimaWarento kutoka Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
“ Kuanzisha kambi za kitaaluma ni wazo zuri na napenda kuwahakikishia kuwa fedha zenu
mlizowekeza hapa kambini si bure, tunawaahidi kuwa hatutawaangusha sisi
tumejipanga kufanya mapinduzi ya kitaaluma na tutakuwa nambari moja mwaka huu”
alisema Kasto Nyakarungu mwanafunzi wa
Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Binza.
“Nikiwa miongoni mwa walimu wawezeshaji katika kambi hii ya Kitaaluma
niwahakikishie kuwa tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mkoa wetu unaingia katika
tatu bora na matarajio yetu ni kuwa nafasi ya kwanza” alisema Mwalimu Mary
Kavishe anayefundisha somo la Kiswahili.
Katika uzinduzi huo wa kambi za kitaaluma wadau mbalimbali wakiwemo
viongozi wa Chama na Serikali pamoja na watumishi wa Umma wameahidi kuchangia
vyakula ambavyo ni mchele zaidi ya tani mbili, maharage kilo 200, ng’ombe
wawili na fedha taslimu ili kufanikisha kambi hiyo kufanyika vizuri.
Wanafunzi wa Kidato cha Sita wako kambini kuanzia tarehe Mosi Aprili, 2019
na wanatarajia kukaa kambini kwa takribani siku 28 na baadaye kutawanyika kwenda
kwenye shule zao kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya Mtihani wa Taifa
utakaoanza Mei 06, 2019.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akifurahia jambo na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha
Sita katika Shule ya Sekondari Itilima, mara baada ya kuzindua rasmi kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akizungumza katika uzinduzi
rasmi kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019,
uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Afisa Elimu Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akizungumza katika uzinduzi rasmi kambi ya Kitaaluma
kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi
wa Chama na Serikali (walioketi) na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019
Shule ya Sekondari Meatu, mara baaada ya uzinduzi rasmi kambi ya Kitaaluma kwa
wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mwanafunzi wa Kidato cha
Sita katika Shule ya Sekondari Maswa, Mkami Warento akizungumza wakati wa
uzinduzi rasmi kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019,
uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Kasto Nyakarungu Mwanafunzi
Wa Kidato Cha Sita Shule Ya Sekondari Binza Warento
akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato
cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa,
Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akifurahi jambo na baadhi ya wanafunzi wa Kidato
cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na Mkuu wao wa Shule,
mara baada ya kuzindua rasmi kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha
Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa,
Aprili 3, 2019.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Mariam Manyangu akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Katibu wa CWT Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Said Mselem akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Baadhi ya walimu mahiri
kutoka shue 12 za Kidato cha Tano na Sita mkoani Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) , wakati wa uzinduzi rasmi
kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi fedha Mwanafunzi mtarajiwa wa Kidato cha Tano,
Silya Shiwa Jasamila(19) ambaye analelewa na Serikali katika Shule ya Sekondari
Maswa Girls baada ya kukimbia nyumbani kwao baba yake alipotaka kumuozesha mara
baada ya kumaliza kidato cha nne 2018 katika Shule ya Sekondari Kilabela
Wilayani Bariadi na kupata ‘division two ya point 19’.
Baadhi ya wanafunzi
wakiimba wimbo wa Tanzania kabla ya uzinduzi rasmi kambi ya Kitaaluma kwa
wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Afisa Elimu wa Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Ernest Hinju (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (wa pili kulia) wakifurahia
jambo na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita mara baada ya uzinduzi rasmi
kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza jambo na mwanafunzi wa Kidato cha Tano mtarajiwa,
Silya Shiwa Jasamila(19) ambaye analelewa na Serikali katika Shule ya Sekondari
Maswa Girls baada ya kukimbia nyumbani kwao baba yake alipotaka kumuozesha mara
baada ya kumaliza kidato cha nne 2018 katika Shule ya Sekondari Kilabela
Wilayani Bariadi na kupata ‘division two ya point 19’.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na walimu na wanafunzi katika
uzinduzi rasmi kambi ya Kitaaluma kwa
wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi
wa Chama na Serikali, mara baaada ya uzinduzi rasmi kambi ya Kitaaluma kwa
wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi wanafunzi mara baada ya kuzindua rasmi kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na walimu na wanafunzi katika uzinduzi rasmi kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa
Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana
Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi wanafunzi mara baada ya kuzindua rasmi kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi wanafunzi mara baada ya kuzindua rasmi kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika Shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itilima, mara baada ya uzinduzi rasmi wa kambi
ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019, uliofanyika katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 3, 2019.
0 comments:
Post a Comment