Katibu MTENDAJI wa Baraza la Taifa la
Mitihani Tanzania (NECTA) amewataka wanafunzi wa kidato cha sita nchini, wanaotarajia kufanya mtihani wao wa mwisho mapema mwezi Mei, 2019 kuepuka aina
yoyote ya udanganyifu kwenye mtihani huo.
Dkt. Msonde ameyasema hayo wakati
akiongea na wanafunzi wa kidato cha sita mkoani Simiyu waliopo kwenye kambi ya
kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, ambayo inayohusisha
wanafunzi 1166 kutoka shule 12 zikiwemo 10 za umma na mbili za binafsi zenye
kidato cha sita.
"Niwatake msifanye asilani habari
yoyote ya udanganyifu kwenye mtihani wenu, mkifanya hayo tu kwanza yatawafanya
mshindwe lakini pili tutakaponusa tu harufu yoyote ya udanganyifu tutawafutia
matokeo"alisema Dkt. Msonde.
Wakati huo huo Dot. msonde amewataka
wanafunzi hao kuondokana na dhana kwamba mtihani wa Taifa ni mgumu hali
inayopelekea kuwa na homa ya mtihani(hofu), badala yake wajiamini na wajiandae
vema kwa kuzingatia waliyofundishwa na walimu wao.
Pamoja na hayo amewapongeza viongozi wa
mkoa wa Simiyu kwa ubunifu wao wa kuanzisha kambi za kitaaluma hatua
inayopelekea mkoa huo kupiga hatua ya katika ufaulu wa mitihani ya kidato cha
sita na kidato cha nne.
Awali akimkaribisha Katibu Mtendaji wa
NECTA, Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl.
Ernest Hinju amesema kuwa awali mkoa ulikuwa na ufaulu mbaya lakini kupitia
kambi ufaulu umepanda kuanzia matokeo ya kidato cha sita kutoka nafasi ya 26 mwaka
2017 hadi nafasi ya 10 mwaka 2018 na kidato cha nne kutoka nafasi ya 11 mwaka
2017 hadi nafasi ya 9 mwaka 2018.
Akiongea kwa niaba ya walimu mkuu wa
shule ya sekondari ya wasichana Maswa Mwl. Kuyunga Jackson amesema kuwa vijana
wa kidato cha sita Simiyu wamepikwa vizuri kitaaluma hivyo matarajio yao ni
kuingia tatu bora kitaifa.
Katika hatua nyingine wanafunzi waliopo
kambini hapo wamesema kuwa ujio wa katibu mtendaji NECTA umekuwa chachu ya
ufaulu wao na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoyaeleza ikiwemo kuepuka
udanganyifu pamoja na kuondoa homa ya mtihani.
"Tunakushukuru Sana kwa ujio wako
umetujenga na kutuondolea hofu ya mtihani, tutafanyia kazi uliyotueleza,
tunakuhakikishia hatutajihusisha na udanganyifu wowote kwa sababu walimu
wametuandaa vizuri na tunajua udanganyifu
unaweza kusababisha tusifikie ndoto zetu; tutazingatia yote tuliyofundishwa na
walimu wetu" alisema Julieth John.
MWISHO
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita
mkoani Simiyu walio katika kambi ya Kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa, wakati alipotembelea kambi hiyo Aprili 25,2019.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato Cha Sita mkoani Simiyu wakimsikiliza
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde
(hayupo pichani) wakati alipowatembelea katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 25, 2019.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.
Ernest Hinju akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mtendaji wa Baraza la
Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde azungumze na wanafunzi wa Kidato
Cha Sita mkoani Simiyu, walio katika kambi ya Kitaaluma katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa Aprili 25, 2019.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa, Julieth John akitoa shukrani kwa Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde
alipowatembelea Wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, Aprili 25,
2019 katika kambi ya Kitaaluma Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa
PICHA 4:-Mwanafunzi wa Kidato Cha Sita
Shule ya Sekondari Simba wa Yuda, Innocent Leonard akitoa shukrani
kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taiga(NECTA), Dkt. Charles Msonde
alipowatembelea Wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, Aprili 25,
2019 katika kambi ya Kitaaluma Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana
Maswa, Mwl. Kuyunga Jackson akizungumza kwa niaba ya walimu wakati wa ziara ya
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde
katika kambi ya Kitaaluma kwa Wanafunzi wa KIDATO Cha Sita katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 25, 2019.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde(katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Maafisa wa Idara ya Elimu Mkoa wa Simiyu, walimu wanafunzi wa Kidato Cha
Sita mkoani Simiyu, Mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika kambi ya
Kitaaluma ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita inayoendelea katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde (katikati kwa walioketi)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Maafisa wa Idara ya Elimu Mkoa wa Simiyu, walimu wanafunzi wa Kidato Cha
Sita mkoani Simiyu, Mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika kambi ya
Kitaaluma ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita inayoendelea katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa.
Picha 7:-Katibu Mtendaji wa Baraza la
Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde(wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Maafisa wa Idara ya Elimu Mkoa wa Simiyu, walimu mahiri
wanaowafundisha wanafunzi wa Kidato Cha Sita katikankambibya Kitaaluma ya
Wanafunzi wa Kidato Cha Sita mkoani Simiyu, Mara baada ya kutembelea
kambi hiyo Aprili 25, 2019 ambayo inayoendelea katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde(kushoto) akiteta jambo na Afisa Elimu wa Mkoa
wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju wakati alipowatembeleawanafunzi wa kidato cha sita
Simiyu katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa, Aprili 25, 2019.
0 comments:
Post a Comment