Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.Anthony Mavunde ametoa wito kwa wanafunzi wa kidato
cha sita Mkoani Simiyu kutokubali mtu yeyote kufifisha wala kukatisha ndoto zao
badala yake wasome kwa bidii.
Mavunde ametoa wito huo wakati
akizungumza na wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka shule kumi na mbili za sekondari za
kidato cha sita walioko katika kambi ya kitaaluma, shule ya sekondari ya wasichana
Maswa.
Mavunde amesema Taifa lolote duniani linajengwa na vijana na hasa vijana
wasomi hivyo wanapaswa kusoma kwa bidii, ili wasiwaangushe, wazazi na jamii
inayowazunguka ambayo inawategemea, huku
akipongeza uongozi wa mkoa kuanzisha kambi za kitaaluma ambazo zimeoneka
kuusaidia mkoa kupanda katika ufaulu.
“wanafunzi msikubali ndoto zenu zikatishwe, someni kwa bidii mfikie ndoto
zenu, Taifa wazazi na jamii inayowazunguka inawategemea, msiwaangushe viongozi
wenu waliofanya mkawa hapa, Mkoa wa Simiyu ndio umetuonesha kuwa kumbe kambi za
kitaaluma zinawezekana” alisema Mhe. Mavunde.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza walimu wote
kwa kazi nzuri wanayoifanya na kueleza lengo la kuanzishwa kambi za kitaaluma ambazo
amesema zimeonekana kuwa na mwamko mkubwa kwa wanafunzi.
“Sisi tulitafakari watoto wetu wanatoka kwenye mazingira ya kawaida tukajiuliza
kwa nini wasikae kwenye madarasa yaliyo na sakafu na dari safi wakasoma,
tumejaribu kwenye shule za O’level (kidato cha nne) tumeona mwamko wa watoto
kusoma” alisema Mhe. Mtaka.
Kwa upande wao viongozi na wadau mbalimbali wa elimu waliowatembelea
wanafunzi hao pia walipata nafasi ya kuwausia wanafunzi hao wa kidato cha sita
na kuwasisitiza juu ya umuhimu wa kufanya bidii ili kufikia malengo yao.
“ Tunajadiliana hapa ili kuwa na uelewa wa pamoja, ninataka kuwaambia kuwa
hakuna mafanikio yanayokuja kwa bahati mbaya iwe katika masomo hata katika maisha,” alisema
Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisha.
“Mnaweza kutimiza ndoto zenu bila kujali mahali mtu anapotoka, najua wengi
wetu hapa tumetoka katika familia za kawaida, tumesoma shule za kawaida kabisa
lakini tulifanikiwa, hata ninyi mnaweza ni suala la kuamua tu” alisema
Happiness Lugiko Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Naye Askofu
wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la kusini, Mch. Mark Malekana
amesema ili wanafuzi hao waweze kufikia ndoto zao wanapaswa kuwa na dhamira ya
kushinda, wasome kwa bidii, wawe na nidhamu, washinde hofu wanapokuwa kwenye
mitihani na wamwamini Mungu.
Mwanafunzi
Kelista Joseph kutoka shule ya sekondari Itilima amesema maswali mbalimbali ambayo
wamekuwa wakiyafanyia kazi yatawasaidiana mwishowe watafanya vizuri na wanaamini kama walivyoahidi toka siku ya
kwanza ya kambi kwamba watapata ‘Division One’ wote.
Kambi
ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoani Simiyu
inatarajiwa kufungwa rasmi Aprili 28, 2019 na baadaye wanafunzi watarejea
katika shule zao kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa unaotarajia kuanza
Mei 06, 2019.
MWISHO
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita walio
katika kambi ya Kitaaluma Mkoani Simiyu wakati aliwapowatembelea wanafunzi hao
wilayani Maswa, Aprili 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akipokea mchango wa shilingi milioni moja kutoka
kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira,
Mhe.Anthony Mavunde aliochangia kwa ajili ya kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa
kidato cha sita inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Baadhi ya wanafunzi wa
Kidato cha Sita mkoani Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.Anthony Mavunde wakati alipowatembelea
wanafunzi hao Aprili 19, 2019. katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa wakati viongozi mbalimbali wa Serikali walipowatembelea wanafunzi
walio katika kambi ya kitaaluma kwa
wanafunzi wote wa kidato cha sita Mkoani Simiyu inayoendelea katika shule hiyo.
Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita Mkoani Simiyu walio
katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule ya sekondari ya wasichana
Maswa (hawapo pichani) wakati viongozi mbalimbali wa Serikali walipowatembelea
shuleni hapo.
Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Happiness Lugiko akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita Mkoani
Simiyu walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule ya sekondari
ya wasichana Maswa (hawapo pichani)wakati viongozi mbalimbali wa Serikali walipowatembelea
shuleni hapo.
Baadhi ya viongozi
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waanfunzi wa kidato cha sita mwaka
2019 mkoani Simiyu, walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule ya
sekondari ya wasichana Maswa wakati viongozi hao walipowatembelea shuleni hapo
Aprili 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akimtambulisha Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.Anthony Mavunde kwa wanafunzi wa Kidato
cha Sita Mkoani Simiyu walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika
shule ya sekondari ya wasichana Maswa (hawapo pichani) wakati viongozi
mbalimbali wa Serikali na wa dini walipowatembelea shuleni hapo.
Askofu wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la kusini, Mch. Mark Malekana akiwaombea wanafunzi
wa Kidato cha Sita Mkoani Simiyu walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea
katika shule ya sekondari ya wasichana Maswa wakati viongozi mbalimbali wa Serikali
na wa dini walipowatembelea shuleni hapo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita
waliokatika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule ya sekondari ya
wasichana Maswa wakati viongozi mbalimbali wa Serikali na wa dini walipowatembelea
shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita
waliokatika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule ya sekondari ya
wasichana Maswa wakati viongozi mbalimbali wa Serikali na wa dini walipowatembelea
shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Kalista Joseph Mwanafunzi
wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya
Sekondari Itilima akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa mkoa wa Simiyu
waliopo katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule ya sekondari ya
wasichana Maswa wakati viongozi mbalimbali wa Serikali na wa dini walipowatembelea
shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Mmoja wa wanafunzi wa
Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari Simba wa Yuda akizungumza kwa niaba
ya wanafunzi wenzake wa mkoa wa Simiyu waliopo katika kambi ya kitaaluma inayoendelea
katika shule ya sekondari ya wasichana Maswa wakati viongozi mbalimbali wa Serikali
na wa dini walipowatembelea shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(wa nne kushoto) na vingozi wengine wa dini na wa serikali
wakizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoa wa Simiyu waliopo
katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule ya sekondari ya wasichana
Maswa, wakati viongozi hao walipowatembelea shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Baadhi ya viongozi na
wanafunzi wakishuhudia ng’ombe wawili waliotolewa na wadau wa elimu kwa ajili
ya kuchangia kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita inayoendelea
katika shule y sekondari Maswa.
Baadhi
ya viongozi wa dini na Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoa wa Simiyu waliopo katika kambi ya kitaaluma inayoendelea
katika shule ya sekondari ya wasichana Maswa, wakati viongozi hao walipowatembelea
shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya(mwenye miwani) na Mkuu wa
mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha
Sita mkoa wa Simiyu waliopo katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule
ya sekondari ya wasichana Maswa, wakati viongozi wa Serikali na wa dini walipowatembelea
shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Mkurugenzi wa Utawala
na Fedha wa BRELA, Bw. Bakari Mketu akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita
Mkoani Simiyu walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika shule ya
sekondari ya wasichana Maswa (hawapo pichani)wakati viongozi mbalimbali wa Serikali
na viongozi wa dini walipowatembelea
shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya akisalimiana na Silya Jasamila(19)binti aliyenusurika kuozeshwa na
baba yake mzazi mara baada ya kuhitimu kidato cha nne , ambaye kwa sasa anatunzwa
na kulelewa na viongozi wa Serikali katika Shule ya sekondari Maswawakati
akisubiri kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano, wakati balozi huyo
alipowatembelea wanafunzi wa kidato cha sita walio katika kambi ya kitaaluma
shuleni hapo Aprili 19, 2019
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.Anthony Mavunde(wa pili
kushoto) akiteta jambo na Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati viongozi
mbalimbali wa serikali na dini walipowatembelea wanafunzi wa Kidato cha sita
mkoani Simiyu(hawapo pichani) Aprili 19, 2019 katika kambi ya Kitaaluma
inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka na kulia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki,
Mhe. Happiness Lugiko.
Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe na
Afisa Elimu Mkoa, Mwl. Ernest Hinju wakifurahia jambo wakati wa ziara ya
viongozi mbalimbali katika kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita
inayoendelea katika shule ya sekondari ya wasichanaMaswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
mhe. Anthony Mtaka(mwenye kipaza sauti) akimtambulisha Askofu wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la kusini, Mch. Mark Malekana kwa wanafunzi wa
Kidato cha Sita mkoa wa Simiyu waliopo katika kambi ya kitaaluma inayoendelea
katika shule ya sekondari ya wasichana Maswa, wakati viongozi wa Serikali na wa
dini walipowatembelea shuleni hapo Aprili 19, 2019.
Baadhi
ya wanafunzi wa kidato cha sita walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea
katika shule ya sekondari ya wasichana Maswa wakiimba wimbo wa Tanzania
Tanzania, wakati viongozi wa Serikali na wa dini walipowatembelea shuleni hapo
Aprili 19, 2019.
0 comments:
Post a Comment