Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na
Ajira, Mhe. Anthony Mavunde ametoa wito kwa kwa Chama cha
wanataaluma na wajasiliamali wa Kanisa la Wadventista Tanzania (ATAPE) kushiriki
katika uchumi wa viwanda ili kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na kupunguza
umaskini.
Mavunde ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa 20
wa chama hicho ambao Kitaifa unafanyika mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na
zaidi ya wanachama 1500 kutoka maeneo yote nchini.
“ATAPE kupitia wataaluma na wajasiriamali mnayo nafasi
kubwa ya kukusanya rasilimali na kuhakikisha mnafanya vitu vyenye mchango
chanya kwa Taifa hususani katika kutengeneza ajira kwa vija na kupunguza
umaskini”
“Angalieni fursa zinazowazunguka ili miaka 20 ya uwepo wa ATAPE iende sambamba
na uwekezaji na mafanikio mtakayoyapata, nitoe wito msiwe nyuma kushiriki
katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, Simiyu wanajenga viwanda vikubwa Maswa cha
chaki na vifungashio, wtajenga kiwanda cha vifaa tiba amkeni changamkieni”
alisema Mhe. Mavunde.
Hata hivyo ameongeza kuwa kama serikali inatambua
mchango mkubwa walioutoa ATAPE kwa kuendelea kuisaidia serikali
kutengeneza nafasi za ajira kupitia uwekezaji walioufanya kwenye meaneo
mbalimbali ikiwemo kilimo, misitu na utoaji wa elimu ya ujasiliamali bure hatua
iliyopelekea idadi kubwa ya watanzania kujiajiri pasipo kusubiri kuajiriwa.
“ATAPE imethubutu nitoe wito kwa madhehebu mengine
kuiga mfumo huu wa kuwaleta pamoja wanataaluma na wajasiriamali ili wawe chachu
ya mabadiliko kiuchumi waweze kufanya vitu vyenye manufaa kwa waumini na jamii
kwa ujumla, epukeni dhana potofu ya kusema hatutoweza mjiamini mtaweza tu”
Awali akimkaribisha Naibu waziri, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema
kuwa kama mkoa uliona kila sababu ya kuzialika taasisi mbalimbali ikiwemo BRELLA
, Shirika la bima la Taifa , EFTA lengo likiwa kuwafikia wajasiliamali na
kuongeza kuwa ni vema wana ATAPE wakajifunza kutenda badala ya kuzungumza
“Ifike mahali mtofautishe mahubiri na ujasiliamali ni
lazima mkizungumza mjifunze kutenda ….hivi karibuni ujenzi wa chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM) kinaanza kujengwa wanachuo 1000 wanatarajiwa kusoma
hapo, nendeni pale mkajenge hosteli punguzeni porojo” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka ametoa wito kwa Wajasiriamali kusajili
biashara zao ili ziweze kutambuliwa na wazikatie bima kwa ajili ya kuepuka
hasara pindi biashara zao zinapokumbwa na majanga hususani majanga ya moto.
Mwenyekiti wa ATAPE Taifa, Bw. Freddie Manento amesema
kuwa chama hicho kimefanikiwa kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni moja kupitia
miradi ya maendeleo waliyiwekeza katika maeneo mbalimbali hapa nchini na
kuongeza kuwa wamewekeza kwenye miradi ya kilimo afya, maji, ujasiliamali na elimu.
“Tuna mashamba zaidi ya ekari 10,000 ambayo tumelima
korosho ,miti na mihogo ,tumewekeza mradi wa maji kigamboni jijini Dar es
salaam hivyo tunavyoadhimisha miaka hii 20 ya ATAPE tuna kila sababu ya
kujivunia maana miradi hii yote imetoa ajira nyingi kwa watanzania wenzetu
zikiwemo za kudumu na za mkataba” alisema Maneto.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Waadventista
Wasabato, Mark Malekana amewataka waumini wa kanisa hilo kufanya kazi kwa bidii
ili kukwepa dhambi ya umaskini na kuwataka kuunga mkono juhudi za Serikali
iliyopo madarakani katika kujiletea maendeleo.
Naye Irene Kweka ni miongoni mwa wajasiliamali
walioshiriki mkutano huo amesema kuwa mkutano huo umemsaidia kuongeza wateja
wapya kujifunza kupitia kubadilishana uzoefu sambamba na kuongeza kipato.
MWISHO
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na
Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama
hicho unaofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya Wanachama wa
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE), wakiimba wimbo wa pamoja wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
20 wa Chama hicho unaofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony
Mavunde (wa pili kulia) akifurahia jambo na viongozi wa Serikali na Kanisa la
Waadventista Wasabato baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama Wanataaluma
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE) unaoendelea
Mjini Bariadi, (wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde(wa nne
kushoto) akiwa na baadhi ya Kanisa la Waadventista
Wasabato na viongozi wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa hilo
wakishuhudia onesho la Vijana watengeneza njia(Pathfinders) kabla ya kufungua
Mkutano wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania(ATAPE)Mjini Bariadi(wa tatu kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Vijana watengeneza
njia(Pathfinders) wakitoa heshima kwa Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde(hayupo pichani) muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano wa Chama
cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE)Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia
baadhi ya bidhaa za wajasiriamali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Kusekwa Memorial, muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano wa Chama cha Wanataaluma
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE)Mjini
Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE)
Bw. Freddie Manento akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde(mwenye skafu) juu ya masuala
mbalimbali yanayofanywa na chama hicho mara baada ya kutembelea banda lao, muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano mkuu wa
chama hicho unaoendelea mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia
mikanda ya ngozi inayotengenezwa na kikundi cha vijana kutoka Mkula wilayani
Busega, muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE)
Mjini Bariadi.
Mbunge wa Bunge la
Afrika Mashariki, Mhe. Happiness Lugiko akizungumza na Wanachama wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),
wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu.
Kwaya ya Ushuhuda
kutoka Kakola Mkoani Geita ikiimba wimbo maalum wakati wa ufunguzi wa Mkutano
Mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania(ATAPE), unaofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana
na Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mark Malekana mara baada ya
kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE).
Askofu wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Mark Malekana(katikati) akionesha zawadi iliyotolewa na
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE) kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, mara baada ya
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wanachama wa
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE), wakiimba wimbo wa pamoja wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
20 wa Chama hicho unaofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia
baadhi ya bidhaa za wajasiriamali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Kusekwa Memorial, muda mfupi kabla ya kufungua Mkutano wa Chama cha Wanataaluma
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE)Mjini
Bariadi.
Vijana watengeneza
njia(Pathfinders) wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakimvisha skafu Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony
Mavunde mra baada ya kuwasili Mjini Bariadi, kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu
wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania(ATAPE).
0 comments:
Post a Comment