Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinatarajia
kujenga Tawi jipya katika Kata ya Sapiwi Tarafa ya Dutwa wilayani Bariadi
Mkoani Simiyu.
Viongozi wa chuo hicho wakiongozwa na Makamu Mkuu wa
Chuo hicho, Prof. Tadeo Andrew Satta wametembelea eneo hilo leo Machi 26, 2019
na baadaye kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Mkoa wa Simiyu ambapo
wamekubaliana kushirikiana katika hatua
zote kuanzia upimaji wa eneo mpaka ujenzi wa majengo ya chuo.
Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Makamu
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Andrew Satta
amewashukuru viongozi hao kwa kutoa eneo la ekari ishirini bure akaahidi kushirikiana
na Serikali mkoani hapa kuhakikisha tawi hilo linajengwa mkoani Simiyu ili kusogeza
karibu huduma kwa wananchi wa Simiyu.
Awali akizungumza na viongozi hao Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo iko tayari kushirikiana
na viongozi wa Chuo hicho kwa kutoa wataalam watakaosaidia katika Usimamizi wa
upimaji na akashauri ujenzi wa majengo ya chuo hicho ufanyike kwa kutumia mfumo
wa ‘Force Account’ ili kupunguza
gharama.
Amesema mfumo huu utapunguza gharama kwa kuwa
hautumii wakandarasi badala yake ujenzi utafanywa na mafundi wa kawaida
wakisimamiwa na wahandisi wa ujenzi Mkoa
na Halmashauri mkoani Simiyu huku vifaa vyote vya ujenzi vikinunuliwa kwa pamoja na chuo hicho.
Aidha, amemhakikishia upatikanaji wa wanafunzi kwa
kuwa hadi sasa Mkoa wa Simiyu bado una Vyuo vichache vya elimu ya juu, huku
akibainisha kuwa tayari Serikali mkoani hapa imeshatoa ardhi bure kwa ajili
ujenzi wa Matawi ya Vyuo mbalimbali vya elimu ya juu ikiwemo Chuo cha Mipango, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
na Chuo cha Mahakama.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini amesema wanaendelea kushawishi Taasisi nyingi za Elimu ya Juu kujenga
matawi yake Mkoani hapa, ili kutoa nafasi kwa Wanasimiyu kupata elimu ya juu itakayochangia kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii.
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza Makamu Mkuu wa Chuo
cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta alipomtembelea ofisini kwake Machi
26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika
Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho
mkoani hapa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati), baadhi ya watumishi wa Mkoa
wa Simiyu (watatu wa mwanzo kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu
wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tano kulia) na
watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara
baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta(kulia) akizungumza
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka walimpomtembelea ofisini kwake Machi
26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika
Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi , kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho
mkoani hapa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto), akizungumza na Makamu
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto)
na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26,
2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo
lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa
ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mwenyekiti
wa RAAWU Taifa, Dkt. Micahel Mawondo
akizungumza jambo wakati Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho
walimpomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) ofisini
kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa
Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi , kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la
Chuo hicho mkoani hapa.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne A. Sagini (katikati), baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Simiyu (watatu
wa mwanzo kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kulia mbele) na watumishi
wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada
ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta akisaini Kitabu
cha wageni katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
(kushoto) walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea
na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi
wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), walipomtembelea
ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na
Mkoa wa Simiyu, katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi kwa ajili ya ujenzi wa
Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (katikati) akizungumza na baadhi ya
viongozi na watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), walipomtembelea
ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na
Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa
Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment