Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wazazi, walimu na watumishi
wengine wa Serikali, wanafunzi wa kike wanaopata mimba na jamii yote kwa ujumla
kushirikiana na Serikali kuhakikisha wale wote waliowapa mimba wanafunzi
wanabainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mtaka
ameyasema hayo wakati akifunga kikao kazi cha viongozi na watendaji wa idara ya
elimu kilichofanyika Machi 12, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati
ya kuimarisha taaluma mkoa wa Simiyu.
Amesema katika uchunguzi wa awali
uliofanyika imebainika kuwa wazazi, walimu, Maafisa Watendaji wa Kata na
watumishi wengine wa Serikali na wanafunzi wenyewe waliopewa mimba wamekuwa
wakikwamisha juhudi za serikali katika vita hii kwa kuwa sehemu ya kuharibu
ushahidi.
“Kuna mimba zaidi ya 300
zimripotiwa katika maeneo mbalimbali baadhi ya maeneo wazazi wanashiriki
kuharibu na wakati mwingine wanafunzi waliopata mimba wanashirikina na wazazi
kuharibu ushahidi wa kesi wasi za wanafunzi wajawazito, baadhi ya maeneo walimu
wetu wamehisiwa, kwingine watendaji wetu, naomba tushirikiane kuwabaini watu
wanaowapa wanafunzi mimba kwenda kwenye
hatua” alisema Mtaka.
Ameongeza kuwa Kamati ya Ulinzi
na Usalama Mkoa imekaa na wameshakubaliana hatua za kuchukua kwa wanafunzi,
watumishi, wazazi na watu wote waliokatisha ndoto za wanafunzi wa kike kwa
kuwapa mimba.
Kwa upande wake Mwalimu Huruma Mjinja kutoka Shule ya Sekondari
Kidinda, amesema katika kukabiliana na tatizo la mimba kwa wanafunzi ni vema
walimu na wazazi wakashirikiana kuwalinda watoto wa kike na wapate muda wa
kuzungumza nao.
Katika hatua nyingine Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka amesema Wanafuzi wa kidato cha sita mkoani
hapa wanatarajia kuanza kambi za kitaaluma rasmi Machi 31, 2019 kwa ajili ya
kujiandaa na mtihani wa Taifa.
Aidha, Mtaka amewataka Wakuu wa
shule za sekondari zenye wanafunzi wa kidato cha nne chini ya 25 kukutana na
wazazi ili wakae na kukubaliana baadaye kuwakusanya wanafunzi hao kwa pamoja katika
Shule ya sekondari Simiyu kwa ajili ya kufanya kambi za kitaaluma.
“Tunamaliza kujenga Simiyu Sekondari
tukiwa na ziada ya vyumba vya madarasa 20 hivyo wakikaa watu 40 kwa kila chumba
ni wanafunzi 800 tunajenga mabweni manne; shule zote za sekondari zenye
wanafunzi wa kidato cha nne chini ya 25, bodi zao na viongozi wa Serikali wakae
pamoja shuleni hapo kwa ajili ya kambi za kitaaluma baada ya likizo ya
MweziAprili, 2019” alisema Mtaka.
Nao Baadhi ya Wakuu waShule
wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanafanya vizuri ili mkoa uweze
kufanya vizuri pia kitaaluma huku akiomba viongozi wa mkoa waendelee kutoa
motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vvizuri ili waweze kufanya vizuri
zaidi kila mwaka.
“ Tutafanya jitihada kuhakikisha
tunafanya vizuri lakini tunaomba viongozi wetu waendelee kuona haja ya kutoa
motisha kwa wanaofanya vizuri kwa sababu mkiendelea kufanya hivyo mtatupa nguvu
ya kufanya vizuri zaidi” Mwalimu Enelico Mwandibila kutoka wilaya ya Itilima.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema mkoa huo umejiweka mkakati kabambe wa
kuimarisha ufuatiliaji na ufundishaji na tathmini itafanyika kila mwezi kujua
vipindi vilivyofundishwa na ambavyo havijafundishwa vitafidiwa.
Kikao hiki kimehudhuriwa na
Maafisa Elimu na Taaluma wa Mkoa na Wilaya, baadhi ya Waratibu Elimu Kata,
Wakuu wa Shule za Sekondari za Kidato cha Nne, wadhibiti ubora na baadhi ya
wadau wa elimu mkoani Simiyu.
MWISHO.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka(mwenye suti katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Bariadi, mara baada
ya kufunga kikao kazi cha viongozi na watendaji wa idara ya elimu kilichofanyika
shuleni hapo Machi 12, 2019 kwa lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha taaluma mkoani
Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na watendaji wa idara
ya elimu katika kikao kazi kilichofanyika Machi 12, 2019 Mjini Bariadi kwa
lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha taaluma mkoani Simiyu.
Baadhi
ya viongozi na watendaji wa idara ya elimu mkoa wa Simiyu wakiwa katika kikao
kazi kilichofanyika Machi 12, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati
ya kuimarisha taaluma mkoani Simiyu.
Mmoja
wa Viongozi wa Elimu mkoani Simiyu akichangia hoja katika kikao kazi cha viongozi
na watendaji wa idara ya elimu kilichofanyika Machi 12, 2019 Mjini Bariadi kwa
lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha taaluma mkoani Simiyu.
Ibrahimu
Buyungumya mwanafunzi bora wa Mkoa wa Simiyu katika Mtihani wa Kidato cha Nne
mwaka 2018 kutoka Shule ya Sekondari Nkololo wilayani Bariadi, akionesha kiasi
cha fedha alichopewa na baadhi ya wadau wa elimu mkoani Simiyu kama pongezi,
katika kikao kazi cha viongozi na watendaji wa idara ya elimu kilichofanyika
Machi 12, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha taaluma
mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na watendaji wa idara
ya elimu katika kikao kazi kilichofanyika Machi 12, 2019 Mjini Bariadi kwa
lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha taaluma mkoani Simiyu, (kushoto) Afisa
Elimu Mkoa, Mwl Ernest
Hinju.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka(mwenye suti katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Bariadi, mara baada
ya kufunga kikao kazi cha viongozi na watendaji wa idara ya elimu kilichofanyika
shuleni hapo Machi 12, 2019 kwa lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha taaluma mkoani
Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka(mwenye suti katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Bariadi, mara baada
ya kufunga kikao kazi cha viongozi na watendaji wa idara ya elimu kilichofanyika
shuleni hapo Machi 12, 2019 kwa lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha taaluma mkoani
Simiyu.
0 comments:
Post a Comment