Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka ametoa wito kwa wanawake, kuwa mstari wa mbele kuhimiza jamii juu ya
umuhimu wa kuwasomesha watoto, ili kuondokana mila potofu zilizopitwa na
wakati, ukiwemo ubaguzi wa kijinsia na mfumo dume.
Mtaka ametoa wito huo,wakati wa siku ya
maombi ya Dunia yaliyofanyika Nyamiongo Manispaa ya Musoma Mkoani Mara
ambako alikuwa mgeni rasmi, ambayo yaliwahusisha wanawake kutoka katika
madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki
Tanzania(WAWATA).
Amesema suluhisho la mila potofu zilizopitwa na wakati kama mfumo dume, ubaguzi
wa kijinsia na kuona watoto wa kiume ni bora kuliko wa kike ni kuwasomesha
watoto wote pasipo kujali kuwa ni wa kike au wa kiume.
“Ukisomesha watoto wako vizuri wakafanikiwa kwenye hiyo nyumba hakuna
atakayesema yeye ni bora zaidi ya mwenziye, hakuna atakayesema mimi ndiye mwanaume
kwenye hii nyumba na huyu ni mwanamke, somesheni
watoto hayo mambo yote yaliyopitwa na wakati yataisha” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amewaomba wanawake na waumini wote wa ujumla kuendelea
kuliombea Taifa, Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi
wengine, ili nchi iendelee kuwa na amani na viongozi waweze kufanya mazuri
yaliyokusudiwa kwa ajili ya Watanzania wote.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya dini pamoja
na kusimamia kiroho wawe msaada kwa makundi mbalimbali yaliyomo makanisani
hususani vijana na wanawake, ili yaweze kuendesha miradi ya maendeleo itakayowasaidia
kubadilisha maisha yao kiuchumi.
Baadhi ya wanawake walioshiriki katika Maombi ya dunia baada ya kusikia
hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka ambaye alikuwa mgeni rasmi wamesema watahakikisha wanasimamia
vema malezi ya watoto wao na kuhakikisha wanasoma huku wakiunga mkono wazo la
vikundi kuwa na miradi ya maendeleo.
“ Kama mama nimejifunza mengi; moja ni kuwa tukiwasomesha watoto wetu
hakutakuwa na unyanyasaji, mfano kama kuna watu wanafanya ukeketaji kwa watoto
wa kike, jamii ikielimika haya hayatakuwepo na tutahakikisha wanasoma mpaka vyuo
vikuu; ujasiriamali nao tutafanya ili tujikwamue kwenye umaskini” Devotha
Charles mshiriki kutoka Mwisenge
“Baadhi ya wanawake katika makanisa yetu tulikuwa hatua miradi na wengine
waliokuwa nayo ilikuwa inaenda kwa kusuasua, lakini baada ya ujumbe
tulioupokea leo nina hakika utaleta mwamko kwa wanawake wengi kuanzisha miradi
ya kuwasaidia kupata kipato” Jackline Cheche mshiriki kutoka Parokia ya
Nyamiongo Musoma.
Kwa upande wake Askofu
wa Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila amesema maombezi kwa
ulimwengu yaendelee kufanyika ili watu waweze kuheshimu uhai wa mwanadamu.
“Ombeeni
ulimwengu uheshimu uhai wa mwanadamu tumeumbwa katika sura na mfano wa Mungu,
tumekabidhiwa dhamana hiyo ya uumbaji, uhai huu tuulinde tuutetee na tuukuze
kwa ajili ya kujenga ulimwengu, maisha yetu yana nafasi ya pekee yanapokuwa na Mungu”
alisema Askofu Mlonganzila.
Maombi
ya Dunia kwa wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na
Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) hufanyika kila mwaka Machi Mosi yakiwa na
lengo la kuombea familia, Taifa na Dunia kwa ujumla juu ya amani na mahitaji
mengine.
MWISHO.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiimba
pamoja na Kwaya ya Upendo kutoka Kanisa la Anglikana Musoma katika Siku ya
maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya
Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya
Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA) .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza
na wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki
Tanzania(WAWATA) wa Mjini Musoma mkoani Mara katika Siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika
Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo
Musoma.
Mwenyekiti wa Wanawake
wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki
Tanzania(WAWATA) wa Mjini Musoma mkoani Mara, akimtambulisha Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Siku ya
maombi ya Dunia yaliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya
Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya
Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA) .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na
Askofu Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila wakifurahia jambo katika
Siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika katika Viwanja vya Parokia ya Yohana
Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya
Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake WaKatoliki Tanzania(WAWATA) , Machi Mosi, 2019.
Askofu Jimbo Katoliki
la Musoma, Mhashamu Michael Mloganzila akitoa baraka mara baada ya kumalizika kwa
ibada ya siku ya maombi ya Dunia yaliyofanyika katika Viwanja vya Parokia ya
Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa kujumuisha wanawake wa madhehebu ya
Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) , Machi Mosi, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto),
viongozi wa Kanisa na baadhi ya viongozi wa wanawake wakifuatilia jambo katika ibada ya siku ya maombi ya Dunia iliyofanyika Machi
Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma kwa
kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na
Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) .
Katibu wa Wanawake wa madhehebu
ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) wa
Mjini Musoma mkoani Mara, akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo
pichani)akiwa Mgeni Rasmi katika katika ibada
ya siku ya maombi ya Dunia iliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia
ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma na kujumuisha wanawake wa madhehebu ya
Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) .
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto)
akiteta jambo na Askofu Jimbo Katoliki la Musoma Mhashamu Michael Msongazila na
Paroko wa Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma, wakati wa ibada ya siku ya maombi ya Dunia iliyofanyika Machi
Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma na kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya
Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA) .
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akipokea zawadi kutoka kwa Katibu wa Wanawake
wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki
Tanzania(WAWATA) wa Mjini Musoma mkoani Mara wakati wa ibada ya siku ya maombi ya Dunia iliyofanyika Machi
Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma na kujumuisha wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya
Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki
Kwaya ya Upendo kutoka
Kanisa la Anglikana Musoma wakimtukuza Mungu katika ibada ya siku ya maombi ya
Dunia iliyofanyika Machi Mosi, 2019 katika Viwanja vya Parokia ya Yohana
Mbatizaji Nyamiongo Musoma na kujumuisha
wanawake wa madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki
Tanzania(WAWATA) .
Baadhi ya wanawake wa madhehebu
ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Wanawake Wakatoliki Tanzania(WAWATA)wakiwa
katika ibada ya siku ya maombi ya Dunia iliyofanyika Machi Mosi katika Viwanja
vya Parokia ya Yohana Mbatizaji Nyamiongo Musoma.
0 comments:
Post a Comment