Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema mkoa huo umejiwekea malengo ya kuhakikisha zaidi ya
asilimia 80 ya wananchi wake kuwa na kadi za bima ya afya ili kujihakikishia upatikanaji
wa huduma za matibabu katika vituo vya
kutolea huduma za afya hapa nchini.
.
Mtaka ameyasema hayo wakati
ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika Afya wa Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo
la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)wanavyoweza
kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia,
ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Amesema yeye kama Mkuu wa Mkoa
atafanya vikao na wanachama wa AMCOS na
makundi mbalimbali ya wananchi katika wilaya zote mkoani hapa na kuzungumza nao
kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya
matibabu.
Aidha, amesema atawaelimisha
wananchi juu ya umuhimu wa kuwa katika Vyama vya Ushirika Vya Msingi ambavyo
vinawapa nafasi ya kupata matibabu makubwa katika vituo vya kutolea huduma za
afya vya binafsi na vya umma kwa gharama nafuu ya shilingi 76,800/= kwa mtu
mmoja(mwanachama wa ushirika).
“Nitafanya vikao na wanachama wa
AMCOS zote, wakulima, wafugaji, wajasiriamali, makundi yote ya wananchi kwenye
mkoa wetu wa Simiyu, tuweze kuwaelimisha faida ya mwananchi wa mkoa wa Simiyu
kuwa na bima ya afya, kubwa zaidi umuhimu wa kuwa kwenye ushirika ambao
utamwezesha kupata matibabu makubwa kwa bei nafuu” alisema
Katika hatua Nyingine Mtaka
amesema katika kipindi cha msimu wa pamba katika kila kituo cha kununulia pamba
NHIF itaweka Afisa wake kwa ajili ya kusajili wakulima na wanachama wa vyama
vya ushirika walio tayari, hivyo akatoa wito kwa viongozi walioshiriki jukwaa
la ushirika afya kutoa taarifa na elimu kwa wenzao juu ya umuhimu wa suala
hilo.
Mtaka pia ametoa wito kwa
wakulima wote wa pamba kulipa kipaumbele suala la afya kwa kuchukua hatua ya
kuwa na bima za afya ili waweze kuona manufaa ya Serikali kuboresha huduma za
afya ikiwa ni pamoja na kujenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Hospitali za wilaya
kwa kila wilaya na Vituo vingine vya kutolea huduma za afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF), Bernad Konga amesema NHIF ni wadau wakubwa mkoani
Simiyu, hivyo wako tayari kutoa huduma bora na wanawafikia wananchi wa makundi
yote mkoani hapa na watahakikisha wanatoa kadi za bima ya afya kwa wakati kwa
wanachama wote watakaojiunga.
Katika jukwaa hili washiriki wamepata nafasi ya
kuchangia michango mbalimbali huku wanachama wa AMCOS wakiunga mkono mpango huo
wa kupata bima ya afya kwa gharama ya shilingi 76,800/= ili waweze kumudu
gharama za matibabu.
“Mpango huu nimeupokea vizuri ila ninashauri elimu
iendelee kutolewa zaidi na zaidi ili wanachama wote wajue umuhimu wa kuwa na
kadi za bima ya afya na namna zitakavyowasaidia” Lucas Ephraim mshiriki kutoka
AMCOS ya Dutwa Bariadi.
“ Binafsi niko tayari kujiunga na mfuko wa bima ya afya
ili nipate hiyo kadi itakayonifanya niweze kutibiwa popote hapa Tanzania,
lakini naomba tutakapolipia hiyo 76,800/= kadi zetu tuzipate mapema” Mmoja
wa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya msingi, Bw. Magwashi Gandila
Mkoa wa Simiyu una vyama vya Ushirika Vya Msingi(AMCOS)
zaidi ya 300 na Jukwaa hili limeazimia wanachama wa AMCOS wakawe mabalozi wazuri kuwahamasisha wananchi kujiunga na Bima ya
Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani humo katika
Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu
lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya
Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia
vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mkurugenzi mkuu wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Benard Konga akizungumza na viongozi wa
Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani humo, katika Jukwaa la
Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna
wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima
ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika
Machi 14, mjini Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati) aizungumza na Meneja wa Wanachama kutoka
NHIF(kushoto) na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),
Benard Konga, mara baada ya kumalizika kwa Jukwaa
la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna
wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima
ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika
Machi 14, mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa
Serikali na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani Simiyu,
wakifuatilia masuala mbalimbali yakiwasilishwa katika Jukwaa
la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna
wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima
ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika
Machi 14, mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa
dini, viongozi na watumishi wa Serikali na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya
Msingi (AMCOS)mkoani Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yakiwasilishwa katika
Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu
lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya
Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia
vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mwanachama wa Chama cha
Ushirika cha Msingi cha Dutwa wilayani Bariadi, Bw. Lucas Ephraim akichangia
hoja katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu
lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya
Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia
vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya utangulizi katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa
lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)
wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama
familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia katika Jukwaa
la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna
wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima
ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika
Machi 14, mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia katika Jukwaa
la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna
wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima
ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika
Machi 14, mjini Bariadi.
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga ,akichangia hoja katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa
lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)
wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama
familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha
Ushirika Mkoa wa Simiyu(SIMCU), Bw........ akichangia hoja katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa
lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)
wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama
familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mmoja wa Wanachama wa
Vyama vya Ushirika vya msingi akichangia hoja katika Jukwaa
la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna
wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima
ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika
Machi 14, mjini Bariadi.
Shekhe Mkuu wa BAKWATA
Mkoa wa Simiyu, Shekhe Mahamoud Kalokola akitoa dua kwa ajili ya ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa
lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)
wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama
familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment