Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi kutumia nguvu nyingi kujifunza badala ya
kutumia nguvu nyingi kuamua ili wanapofanya maamuzi waamue maamuzi yenye tija kwa
maendeleo ya wananchi katika maeneo yao.
Mtaka
amesema hayo Machi 11, 2019 Mjini Bariadi katika Mdahalo wa uongozi na maendeleo
yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa viongozi wa Mkoa
wa Simiyu,ambao uliwashirikisha viongozi ngazi ya Wilaya na Mkoa.
“Ni vizuri tukatumia nguvu nyingi
kujifunza kuliko kuamua kwa sababu kama hutaki kujifunza unataka uamue utaamua
hata usiyoyajua, inawezekanaje mtu anateuliwa leo kuwa Mkuu wa Mkoa, Wilaya au
Mkurugenzi halafu unakuwa mtaalam wa kila kitu, kilimo wewe, afya wewe, elimu
wewe ; unafikiri unaweza kutranform ( kufanya mabadiliko/mapinduzi ya) uchumi
wa nani?” alisema Mtaka.
Aidha, katika kumuenzi Mwalimu Nyerere amewaasa
viongozi wenzake waliopewa dhamana na Mhe. Rais kuwatumikia wananchi kushughulika na masuala yanayohusu maendeleo
ya wananchi badala ya kujikita katika mambo yasiyo na tija ikiwemo ugomvi kati
yao.
“Tumeaminiwa na Mhe. Rais
tukapewa dhamana tuwatumikie Watanzania wenzetu tujishughulishe na masuala ya
wananchi tuache mambo yasiyo na tija kwa wananchi; hivi kuna haja gani DC
kugombana na DED au RC kugombana na RAS? Kwa nini tumsumbue Mhe. Rais badala ya
kuongelea masuala ya maendeleo ya wananchi abaki kuzungumzia mambo ya ugomvi wa
viongozi? Alihoji Mtaka
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere,
Bw. Joseph Butiku ametoa wito kwa viongozi kuheshimu Katibu ya Jamhuri ya
Muungano waTanzania na kuishi katika misingi ya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere katika uongozi wao.
Aidha, Butiku ametoa rai kwa
viongozi wote wa Serikali kutumia madaraka waliyopewa kwa maslahi ya wananchi
na wahakikishe wanawafikia wananchi
mpaka ngazi za chini ili waweze kuwasaidia namna bora ya kutumia shughuli za
uzalishaji wanazozifanya hususani kilimo
na mifugo kujikwamua kutoka katika umaskini.
Akitoa mada kwa viongozi wa Mkoa
wa Simiyu, Mjumbe kutoka Taasisi ya Mwalimu
Nyerere Bw. Gallus Abed amesema katika kuwaletea maendeleo wananchi ni lazima viongozi
wajiwekee malengo na kusimamia utekelezaji wa malengo hayo na kuhakikisha wanapima
matokeo yake.
Nao baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa
Simiyu wakichangia hoja katika mdahalo wa uongozi na maendeleo yenye tija kwa
wote wamezungumzia mchango wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere na namna wanavyomuenzi
Mwalimu Nyerere katika utekelezaji wa shughuli zao za kuwaletea maendeleo
wananchi.
“Tunaishukuru Taasisi ya Mwalimu
Nyerere kwa namna ambavyo imeamua kutufikia na kuendelea kutuonyesha, kutukumbusha
na kuturejesha ili tuishi maisha ya Mwalimu Nyerere ambaye amekuwa mfano wa
kuigwa” Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
“Serikali ya awamu ya tano
imekuwa ikiyaishi maono ya Baba wa Taifa, Mwl.Julius Nyerere, kama unavyoona
Mhe. Rais amekuwa akisema na sisi tunaona miradi mikubwa ya maendeleo
inatekelezwa kwa fedha zetu za ndani” Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano
Mwera.
“Tunatekeleza
fikra za Mwalimu Nyerere kwa kuanzia hasa katika utekelezaji wa malengo yaliyoko katika
Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Miaka Mitano kwenye maeneo yetu” Kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bibi.Suzana Sabuni.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akifungua Mdahalo wa uongozi na
maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa
wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku
(wa pili kushoto) akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuanza
Mdahalo wa uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi hiyo
kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi(kushoto)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku
akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, katika Mdahalo wa
uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku katika
Mdahalo wa uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi hiyo
kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akifungua Mdahalo wa uongozi na
maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa
wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika mdahalo wa uongozi na
maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa akichangia hoja katika
mdahalo wa uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi ya
Mwalimu Nyerere kwa viongozi wa Mkoa wa
Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja
na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya ufunguzi wa mdahalo uliondaliwa wa
uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote na Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa
wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bi. Suzana Sabuni akichangia hoja katika mdahalo
wa uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu
Nyerere kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu,
ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi
anayeshughulikia Uchumi na Uzalishaji katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Dkt. Gamitwe Mahaza akichangia hoja katika mdahalo wa uongozi na maendeleo yenye
tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao
ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Kitengo cha
Sheria katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Mwanahamisi Kawega,
akichangia hoja katika mdahalo wa uongozi na maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa
na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika
Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa
mkoa wa Simiyu wakiwa katika mdahalo wa uongozi na maendeleo yenye tija kwa
wote maalum ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ambao ulifanyika Machi
11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika mdahalo wa uongozi na
maendeleo yenye tija kwa wote uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao
ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa
wa Simiyu mara baada ya ufunguzi wa mdahalo wa uongozi na maendeleo yenye tija kwa
wote uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao
ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya ufunguzi wa mdahalo uliondaliwa na
Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019
Mjini Bariadi.
Kutoka kushoto
(mbele)Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani, :- Mkuu wa Wilaya
ya Busega, Mhe. Tano Mwera,Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
wakifuailia mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao
ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akimweleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu
Nyerere Joseph Butiku (kulia) ofisini kwake , mara baada ya kiongozi huyo
kuwasili Mjini Bariadi, kwa ajili ya mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu
Nyerere kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu,
ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (kulia) akimweleza jambo Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kiongozi huyo kuwasili Mjini
Bariadi, kwa ajili ya mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao
ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (wa
pili kushoto) akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuanza
Mdahalo uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao
ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi(kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (wa nne kushoto) akizungumza na viongozi wa
Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuanza Mdahalo uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (wa nne
kushoto) akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuanza Mdahalo
uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika
Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa huo na baadhi ya
Viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere ofisini kwake kabla ya kuanza Mdahalo
uliondaliwa na Taasisi hiyo kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, ambao ulifanyika
Machi 11, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment