Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa wazazi na walezi wenye watoto walio katika madarasa ya mitihani ya Taifa kuwapunguzia kazi ili wanafunzi hao waweze kupata muda wa kujiandaa na mitihani hiyo na hatimaye waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Mtaka
ameyasema hayo Mei 06, 2021 Mjini Bariadi wakati wa futari maalum iliyoandaliwa
na ofisi yake kwa ajili ya waumini wa dini na Kiislamu walio katika mwezi
mtukufu wa Ramadhani ambayo pia iliwahusisha viongozi na watendaji mbalimbali
wa Serikali mkoani Simiyu.
“Matarajio
yangu ni kuhakikisha kuwa mkoa huu unabaki kuwa miongoni mwa mikoa mitano
inayofanya vizuri kwenye elimu nchini, kwenye malengo yetu ya mwaka huu ni
kuona tunatoka kwenye nafasi ya tano, kwenda nafasi ya tatu na kufikia nafasi
ya kwanza ili kufikia hapo tuna kazi ya kufanya; niwaombe wazazi na walezi wote
wa mkoa wa Simiyu wenye watoto wa madarasa ya mitihani wawapunguzie kazi ili
wapate muda wa kujisomea na kufanya matayarisho ya mitihani yao ya Taifa,”
alisema Mtaka.
Aidha,
Mtaka amewataka wazazi kutowaruhusu wanafunzi kwenda katika minada kufanya
biashara badala yake wahakikishe wanafunzi wote wanahudhuria masomo, “ Hii
habari ya kuona watoto (wanafunzi) minadani hapana, kila mmoja awe mzazi na
mlezi minada ni kwa ajili ya wazazi kufanya biashara siyo mahala kwa watoto
kupeleka bidhaa maana minada yetu mingi inafanyika siku za kazi”
Kwa
upande wake Sheikh wa Mkoa wa Simiyu Mahamudu Kalokola amemshukuru Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu kwa futari na kushiriki katika shughuli mbalimbali zinasowahusu Waislamu
ikiwa ni pamoja na kushiriki katika ujenzi wa msikiti mkuu wa Bariadi , huku
akiwataka Waislamu wote mkoani Simiyu kuendelea kuiombea nchi na kudumisha
amani iliyopo.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Simiyu,Askofu Marco Maduhu ametoa rai
kwa wananchi mkoani Simiyu kuendelea kushirikiana na kuthaminiana bila kujali
tofauti za dini zao.
Naye Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Bi. Haula
Kachwamba amewatakia heri Waislamu wote walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhani na kuwaombea waweze kumaliza mfungo huo salama.
MWISHO
Muimbaji maarufu wa Kaswida Bi. Arafa Abdillah Salum akiimba katika hafla maalum ya futari Mei 06, 2021 Mjini Bariadi, iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya Waislamu waliofunga na baadhi ya makundi ya watu mkoani hapa.
TAZAMA PICHA MBALIMBALI KATIKA HAFLA MAALUM YA FUTARI MEI 06, 2021 MJINI BARIADI, ILIYOANDALIWA NA MKUU WA MKOA WA SIMIYU, MHE. ANTHONY MTAKA KWA AJILI YA WAISLAMU WALIOFUNGA NA BAADHI YA MAKUNDI YA WATU MKOANI HAPA.
0 comments:
Post a Comment