Usimamizi shirikishi, elimu kwa umma zimetajwa kuwa ni miongozi mwa sababu zilizochangia kupunguza uwepo wa dawa bandia katika mikoa ya kanda ya ziwa, jambo ambalo limechangia soko la bidhaa hizo (dawa) kuwa soko salama.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba, Bi. Sophia
Mziray Mei 06, 2021 wakati akizungumza katika ufunguzi wa kikao kazi cha wataalam
wa afya na mifugo pamoja na wakaguzi wa dawa , kilichofanyika Mjini Bariadi
Mkoani Simiyu.
“Tumeza
kulisimamia vizuri soko hili la kanda ya ziwa siyo kama miaka ile ya nyuma kwa
sasa hivi soko hili naweza kusema ni soko salama kwa bidhaa hizi, hata zikikutwa
sokoni ni chache sana, pamoja na hilo tunawaeleimisha wananchi, suala la
udhibiti siyo la taasisi tu, hata wananchi ni wadau wakubwa katika udhibiti na
huwa tunapata taarifa kutoka kwa rai wema juu ya wafanyabiashara wasio
waaminifu wanaofanya biashara haramu za dawa, tumewabaini na tumewachukulia
hatua,” alisema Mziray.
Akifungua
kikao kazi hicho Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Ekwabi Mujungu amesema kufanya
kazi bila taarifa (kumbukumbu) ni tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka
huku akiwataka kupitia kikao kazi hicho kuja na suluhisho la kudumu.
“Mnaohusika
si lazima mpaka watu watoke Dar es
salaam kuja kuona dawa bandia fanyeni kazi kwa viapo vyenu,” alisema Mujungu
Kwa
upande wao baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho wameishukuru TMDA kutoa
mafunzo ambayo yatawaongezea maarifa na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao
hususani ya ukaguzi kwa ufanisi.
“Elimu niliyoipata leo itanisaidia sana katika
kufanya kaguzi mbalimbali pia imenisaidia kujua kuwa ni jukumu letu wataalam
kuwapa elimu wamiliki wa maduka ili wauze bidhaa zilizosajiliwa na wajenge
utamaduni wa kukagua bidhaa zao (dawa) na kubaini dawa zilizoisha muda wake ili
watumiaji wa mwisho au walaji wasiumizwe kwa kuuziwa dawa zisizofaa” alisema
Linah Kirumbi Daktari wa Mifugo Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment