Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) kufanya tathmini ya miradi iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kupitia mfumo wa ‘Force Account’ (Mfumo usiotumia wakandarasi/ wakandarasi katika ujenzi) na baadaye ije na usahauri kwa serikali juu ya namna ya kuboresha matumizi ya mfumo huo hususani katika suala la ubora.
Mtaka
ametoa rai hiyo jana Mei 06, 2021 wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na
mamlaka hiyo yakiwashirikisha wataalam wa Ununuzi na ugavi, maafisa masuuli na
baadhi ya watendaji ili kuwajengea uwezo ili waweze kufanya kazi ya ununuzi wa
umma kwa ufanisi ambayo yamefanyika Mjini Bariadi.
“Tusije
tukawa na miradi hapa lakini miaka kumi inayokuja tukajikuta kwenye tatizo
kubwa, kwa hiyo PPRA ije na ushauri kwa miaka mitano ya ‘Force Account’ pengine
mfumo huo ni mzuri zaidi kwenye ujenzi wa miradi ya aina gani,” alisema Mtaka.
Kwa
upande wake Afisa mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi. Leonard Kapongo amesema katika
mafunzo hayo wataalam hao watapata naasi ya kujifunza zaidi kuhusu mfumo huo,
utekelezaji wake na ikiwa kuna changamoto walizozibaini wakati wa utekelezaji
wa miradi kwenye maeneo yao ili zijadiliwe kwa pamoja na kubainisha kuwa PPRA
iko tayari kupokea ushauri.
Aidha,
Mhandisi Kapongo amesema wameamua kutoa mafunzo ya masuala ya ununuzi wa ummakwa
wataalam hao kwa lengo la kuwafundisho Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka sura
namba 410 ambayo ni sheria mama ya mwaka 2010 pamoja na marekebisho yake ya
mwaka 2016 ili waweze kufanya kazi za ununuzi kwa ufanisi.
Mhandisi Mpongo amesema pamoja na mkoa wa Simiyu mafunzo
hayo yameshatolewa katika mikoa mingine 14 ambayo ni Ruvuma, Njombe, Iringa, Kagera,
Shinyanga, Kigoma, Geita, Rukwa, Katavi, Tabora, Mbeya, Songwe, Dodoma na Mara.
Naye Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na ushauri wa PPRA,
Mhandisi Mary Swai amesema mafunzo hayo yatawasaidia wataalam kuzingatia sheria
ya ununuzi wa umma na kuzingatia taratibu katika ununuzi ikiwa ni pamoja na
kusimamia mfumo wa ‘force account’ waweze kuhakikisha ubora unaotakiwa
unapatikana na thamani ya fedha inaonekana.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment