Maafisa elimu na wakuu wa
shule zote za sekondari Mkoani Simiyu wametakiwa kuhakikisha wanasimamia
ukamilishaji wa ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa kabla ya kufikia Aprili 20,mwaka huu ili kuruhusu wanafunzi
waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwaka 2019 waweze kuanza masomo.
Wito huo umetolewa Machi 13, 2019 na
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Ernest Hinju wakati wa kikao cha kuweka
mikakati madhubuti ya elimu Mkoani humo.
Hinju amesema kuwa maafisa elimu wote
pamoja na wakuu wa shule za sekondari wanatakiwa kusimamia vema ujenzi wa
maboma hayo ili yaweze kukamilika kwa wakati wakati na ubora unaotakiwa.
Ameongeza kuwa ni lazima ukamilishaji
huo ,ukawa ndani ya muda uliokusudiwa kwani tayari Serikali imeshaziwezesha
shule kiasi cha shilingi 12,500,000/= (kwa chumba kimoja) kwa ajili ya ukamilishaji
wa majengo hayo kwa haraka.
Naye Edda Malick kiongozi wa Mpango wa
kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) amesema kwa upande wao wameweza
kukamilisha ujenzi wa maboma kwa asilimia 60.
Malick ameongeza kuwa wameweza kufikia
asilimia hizo kutokana na jitihada na usimamizi madhubuti wa maafisa elimu na
wakuu wa shule
MWISHO
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Ernest Hinju
akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji wa idara ya Elimu ngazi ya Mkoa na
Wilaya katika kikao kazi kilichofanyika Machi 13, 2019 Mjini Bariadi.
Kiongozi wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP T) Mkoa wa
Simiyu, Edda Malick akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji wa idara ya
Elimu ngazi ya Mkoa na Wilaya katika kikao kazi kilichofanyika Machi 13, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi ya viongozi na watendaji
wa idara ya Elimu ngazi ya Mkoa na Wilaya wakiwa katika kikao kazi
kilichofanyika Machi 13, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment