Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw.
Jumanne Sagini amewataka watumishi wa Umma mkoani humo kuwa mabalozi wema wa
maadili ya utumishi wa umma katika maeneo ya kazi ikiwa ni pamoja na kutopokea
zawadi kwa wananchi wanaowahudumia kwa kuwa wanalipwa mshahara na Serikali kwa
kazi hizo.
Sagini ameyasema hayo Machi 14, 2019
Mjini Bariadi wakati akifungua mafunzo ya Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa
wa Simiyu, yanayoendeshwa na Mratibu wa Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais kwa
kushirikiana na Maafisa kutoka TAKUKURU na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Amesema watumishi wa umma wanalipwa
mishahara ili waweze kuwahudumia wananchi hivyo hawapaswi kudai chochote kutoka
kwa wananchi.
"'Acheni kupokea vizawadi vidogo
vidogo kwa huduma tunazotoa kwa wananchi ambazo tunalipwa mshahara kutokana na
huduma hizo; muwe mabalozi wa kueneza maadili mema kwa watumishi wenzenu
na nje ya maeneo yenu ya kazi ili ofisi zetu za Umma mkoani Simiyu ziwe mfano
wa kuigwa" alisema Sagini.
Aidha, Sagini amezitaka kamati zote za
kudhibiti uadilifu mkoani Simiyu mara baada ya mafunzo ziandae mpango
kazi wa namna ya kushughulikia kero mbalimbali za watumishi zinazohusiana na
ukiukwaji wa maadili katika utumishi wa Umma, ili kuwa na watumishi
wanaozingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya Utumishi wa Umma.
Akitoa taarifa ya mwenendo wa makosa ya
rushwa kwa watumishi wa umma, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Adili
Elinipenda ametoa wito kwa Wakurugenzi kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kuona
namna watakavyosaidia pale wanapoletewa barua za kuwafikisha watumishi
mahakamani kwa makosa ya rushwa ili
kutokuharibu ushahidi.
“Kesi tulizonazo mahakamani nyingi ni za
watumishi wa umma na baadhi ya mashahidi tunaowahitaji wanatoka ofisi hizo hizo
sasa wakurugenzi wamekuwa hawawasimamishi kazi,
kwa hiyo imekuwa ngumu kwa mtumishi kumtolea ushahidi mtumishi mwenzake
aliye naye ofisi moja na wakati mwingine ni bosi wake, sasa hapa nafikiri mtaona
ni busara gani itumike tunapowatumia barua za kuwafikisha watu mahakamani”
alisema Mkuu huyo wa TAKUKURU.
Naye Mratibu wa Utawala Bora kutoka
Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Apolinari Tamayamali amesema ni vema Mamlaka za
Serikali za Mitaa zikazingatia utaratibu wa sheria unaopaswa kufuatwa wakati
mtumishi anapohukumiwa kifungo au faini ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya
Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Pendo Haule kuhusu
kusimamishwa kazi kwa mtumishi ambaye ameshtakiwa mahakamani amesema kwa mujibu
wa Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, sheria imempa nafasi mwajiri ya kumsimamisha kazi au
kutomsimamisha kazi mtumishi ambaye ana
kesi mahakamani, lakini ikiwa kuwepo kwa mtumishi huyo kazini kunaweza kuharibu
ushahidi ni vema sheria ikafuatwa akasimamishwa kazi.
Awali akizungumzia lengo la kuandaa mafunzo kwa kamati za
kudhibiti wa Uadilifu, Mratibu wa
Utawala Bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Apolinari Tamayamali, amesema ni
kuwezesha kamati hizo kupata uelewa wa pamoja juu ya mkakati wa mapambano dhidi
ya rushwa awamu ya tatu, namna ya kuandaa mpango kazi na utoaji wa taarifa
katika masuala ya mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini.
Ameongeza kuwa jithada hizi za kutoa
elimu kwa kamati za udhibiti wa uadilifu zimaeanza mwaka 2017, ambapo hadi
kufikia mwaka 2018 mikoa takribani 16 imefikiwa na kwa sasa timu ya wataalam
iko katika mikoa yote 10 iliyo salia ili kukamilisha mikoa yote 26 ya Tanzania
Bara.
MWISHO
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati za
Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo
ya kamati hizo, Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mratibu wa Utawala
Bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu, Bw. Apolinari Tamayamali akizungumza na
wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani)
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kamati hizo, Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Bw. Adili Elinipenda akitoa taarifa ya
mwenendo wa makosa ya rushwa kwa watumishi wa umma, wakati wa mafunzo ya Kamati
za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika Machi 14, 2019 Mjini
Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Maafisa
kutoka Ofisi ya Rais Ikulu na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa
wa Simiyu, baada ya kufungua mafuzo ya kamati hizo Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu
wakifuatilia mafunzo ya kamati hizo yaliyotolewa Machi 14, 2019 Mjini Bariadi
na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Ikulu.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati
za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mafunzo ya kamati hizo
yaliyotolewa Machi 14, 2019 Mjini Bariadi na wataalam kutoka Ofisi ya Rais
Ikulu.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudhibiti Uadilifu za Mkoa wa Simiyu
wakifuatilia mafunzo ya kamati hizo yaliyotolewa Machi 14, 2019 Mjini Bariadi
na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Ikulu.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti
Uadilifu za Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya kamati
hizo, Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wajumbe wa Kamati za Kudhibiti
Uadilifu za Mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya kamati
hizo, Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment