Saturday, March 16, 2019

DARAJA LA SIBITI KUKAMILIKA MACHI 24 MWAKA HUU


Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent amesema Ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti linalounganisha Mikoa ya Simiyu na Singida unatarajiwa kukamilika kwa awamu ya kwanza na magari kuanza kupita ifikapo Machi 24, mwaka huu.

Kent ameyasema hayo jana Machi 14, 2019 katika kikao cha bodi ya Barabara kilichofanyika Mjini Bariadi, kinachowashirikisha viongozi na wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa Wakala wa Barabara(TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA)Mkoani humo.

Kent amesema agizo la Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuhakikisha wanakamilisha daraja hilo kufikia mwezi Machi, 2019 ambalo alilitoa wakati aipoweka jiwe la Msingi la ujenzi wa daraja hilo Septemba, 2018.

“Ujenzi wa Daraja la Sibiti awamu ya kwanza kama ilivyoagizwana Mhe. Rais utakamilika tarehe 24 mwezi huu,mkandarasi anaendelea na umaliziaji watutala barabara kwenye mwingilio wa daraja kubwa; taratibu za kuongeza kazi ili kukamilisha kuweka tabaka la lami kilomita 25 zinaendelea” alisema Mhandisi. Kent.

Katika hatua nyingine Kent ameeleza mapenddkezo ya bajeti kuwa TANROADS Mkoa wa Simiyu imependekeza na kuomba jumla ya shilingi 11, 461,470 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilometa 1008.76, madaraja makubwa 62 na madaraja madogo 50.

Naye Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Salvatory Yambi amasema bajeti ya matengenezo ya barabara chini ya wakala huo Mkoani Simiyu ni shilingi 5,469,051,603.32 (Bajeti inayozingatia ukomo).

Nao baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara wametoa maoni yao juu ya kazi ya matengenezo ya barabara inayofanywa na TANROADS pamoja na TARURA kama ifuatavyo:-

“Tunaomba Serikali ione namna ya kuiongezea bajeti TARURA ili iweze kutekeleza majukumu yake vizuri maana na mtandao mkubwa wa barabara mjini na vijijini, itoke kwenye asilimia 30 na kufikia asilimia 40 na TANROADS wabaki na asilimia 60 kutoka kwenye asilimia 70 ya sasa” Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mhe. Robert Lweyo

“ Sisi tumeanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bariadi pale , tunaomba TARURA waweke kwenye bajeti yao fedha za ujenzi wa daraja la Mto Bariadi unaounganisha kata saba za Halmashauri yetu” alisema Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa.

“ Naishukuru sana TANROADS kwa kuweka taa katika Mji wa Lamadi, mmepafanya Lamadi papendeze na watu waweze kufanya biashara vizuri, ombi langu muone uwezekano wa kuweka taa katika Mji wa Nyashimo ambao ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Busega”Mhe. Tano Mwera, Mkuu wa Wilaya ya Busega.

Naye Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemtaka Mratibu wa TARURA Mkoa kuhakikisha agizo la Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Pombe Magufuli la kujenga barabara ya kilometa tatu katika Mji Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mwanhuzi.
 MWISHO

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent akitoa taarifa ya matengenezo ya barabara na madaraja kwa wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi..


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.


Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa  wa Simiyu, Mhandisi.Salvatory Yambi, akiwasilisha taarifa ya matengenezo ya barabara zilizo chini ya wakala huo, katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Ephraim Lema akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera wakiteta jambo, katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe na wadau wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho ambacho kilifanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe na wadau wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho ambacho kilifanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe na wadau wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao hicho ambacho kilifanyika Machi 14, 2019 Mjini Bariadi.





0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!