Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally
amesema Mkoa wa Simiyu ni mkoa wa kwanza ukifuatiwa na Mkoa wa Singida, Dodoma
na Pwani katika utekelezaji wa Ilani ya
CCM kwa mshikamano kati ya Serikali na Chama Tawala
Dkt. Bashiru amesema hayo wakati
akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi
katika Kilele cha Maonesho
ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
“ Simiyu ni Mkoa wa Kwanza kwa
Tanzania Bara katika Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, matokeo
tunayoyaona, haya yanayotufurahisha chanzo chake ni mshikamano baina ya
Viongozi wa Chama na Serikali katika Mkoa” alisema Dkt. Bashiru.
Wakati huo Dkt. Bashiru ameitaja
mikoa mitatu ikiongozwa na Simiyu ambayo inafanya vizuri katika Utekelezaji wa
Ilani ya CCM kuwa ni pamoja na Singida, Dodoma na Pwani, huku akieleza kuwa
katika mikoa hii viongozi na watendaji wa Chama wanafanya kazi kwa kushirikiana
na Chama.
Aidha, ameitaja mikoa minne
ambayo haifanyi vizuri kuwa ni Mara, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam na
akawataka viongozi wa Chama na Serikali katika mikoa hiyo kujirebisha ili waweze kufanya kazi kwa kushirikiana.
Amesema
Chama kimeumizwa sana na makundi na kinapata tabu pale ambapo viongozi wa Chama
na Serikali hawana mtazamo mmoja hivyo amewataka viongozi wa mikoa ya Mara,
Mbeya, Arusha na Dar es Salaam kushikamana na kuwa kitu kimoja ili waweze kuwatumikia
wananchi ipasavyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema uhusiano kati ya
Chama na Serikali kwa mkoa huo kuanzia
ngazi ya Kijiji na Tawi hadi mkoa uko vizuri na akimhakikishia Katibu Mkuu wa
CCM kuwa mshikamano baina yao utaendelea kuimarishwa.
Katibu
Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na wananchi Bariadi katika Kilele cha Maonesho ya Nananane Kitaifa mwaka 2018 yaliyofanyika Uwanja wa Nyakabindi Bariadi
0 comments:
Post a Comment