Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.
Zainab Taleck na kumhakikishia Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka
2018 Ndg. Charles Kabeho kuwa atachukua hatua dhidi ya mapungufu yaliyobainika
wakati Mwenge wa Uhuru ukipitia baadhi ya miradi ya maendeleo mkoani Simiyu.
Mtaka amesema ushauri na
mapendekezo yaliyotolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 Ndg. Charles
Kabeho yatafanyiwa kazi,ikiwa kuna mahali pa kuchukua hatua, hatua stahiki zitachukuliwa na ikiwa kuna
mahali pa kufanya maboresho ili miradi hiyo itekelezwe katika viwango vinavyokidhi
haja ya kutoa huduma kwa wananchi, Serikali ya mkoa itahakikisha inasimamia.
“Ndugu Kiongozi wa
Mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 na wakimbiza Mwenge wenzako,
tunawashukuru kwa kuwa sehemu ya jicho la tatu kwenye miradi inayotekelezwa
ndani ya mkoa, niwahakikishie kwamba tutachukua stahiki pale ambapo palionesha
ukakasi kwenye taarifa zetu na pale ambapo mliona kunahitajika hatua ili miradi
iweze kufanya kazi kwa ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi tutachukua
hatua” alisema Mtaka.
Kwa upande wake Kiongozi
wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Kabeho amewashukuru viongozi na
wananchi wa Mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano waliompa yeye na wakimbiza Mwenge
wenzake walipokuwa Simiyu.
Aidha, Kabeho alitoa
rai kwa watumishi wa Umma kuachana na kufanya kazi kwa uzembe na mazoea badala
yake wafanye kazi kwa weledi na bidii, hususani katika usimamizi wa miradi ili
iweze kutekelezwa kwa wakati katika viwango vya ubora unaotakiwa na wananchi
wapate huduma kwa wakati.
Mwenge wa Uhuru
umekabidhiwa katika kijiji cha Wishiteleja katika Wilaya ya Kishapu mkoani
Shinyanga ambapo ukiwa mkoani Simiyu ulipitia miradi 36 yenye thamani ya
shilingi bilioni 8.4.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Taleck katika Kijiji cha Wishiteleja
wilayani Kishapu mkoani Simiyu Agosti 20, 2018.
0 comments:
Post a Comment