Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary
Mwanjelwa ametoa wito kwa wananchi hapa nchini kupanda miti kwa wingi ili
kuboresha mazingira, kutunza uoto wa asili, kuwa na uhakika wa mvua na
kuepukana na ukame.
Ushauri huo ameutoa katika Uwanja wa Nyakabindi
katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe ya Wakulima Nane nane wakati wa zoezi la
kupanda miti, lililofanyika leo Agosti 02, 2018
Mwanjelwa amesema ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabia ya nchi zoezi la upandaji hapa nchini linapaswa kuwa
endelevu kwa wananchi.
"Tumepanda miti hii kwenye Uwanja wa
Nanenane Nyakabindi Bariadi ni sehemu ya uhamasishaji kwa viongozi na wananchi
wote kupanda miti, nitoe rai kwa viongozi na wananchi wote mkoani Simiyu
kuendeleza zoezi hili ili maana tukipanda miti tunaboresha mazingira, tunapata mvua ya
uhakika, kuboresha uoto wa asili hata mifugo yetu inapata malisho"
alisema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel amesema upandaji wa miti una
uhusiano Mkubwa na mifugo katika Ustawi wa malisho, huku akitoa wito kwa
uongozi wa Mkoa wa Simiyu kuendeleza zoezi hili ili kumuunga mkono Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuifanya Tanzania kuwa ya kijani.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu , Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema mkoa unatarajia
kupanda miti zaidi ya milioni tatu .
Katika hatua nyingine Naibu waziri wa
Kilimo ametembelea Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kulipongeza
jesho hilo kwa namna linavyopambana na majanga ya moto na kusisitiza kuendelea
kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wananchi juu ya kukabiliana na majanga
ya moto.
MWISHO
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akipanda mti katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, katika zoezi lililofanyika leo
Agosti 02, 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akiumwagilia maji mti alioupanda katika Uwanja wa
nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, katika zoezi
la viongozi kupanda miti lililofanyika leo Agosti 02, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akipanda mti katika Uwanja wa
nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, katika zoezi
lililofanyika leo Agosti 02, 2018.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi, Profesa. Elisante Ole Gabriel akipanda mti katika Uwanja wa
Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu katika zoezi
lililofanyika leo Agosti 02, 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akisisitiza jambo juu ya umuhimu wa upandaji miti, katika zoezi
la upandaji miti lililofanyika Agosti 02, 2018, katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kilimo kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti, katika
Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Bw. Martin Malima akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipotembelea banda la maonesho la
Mamlaka hiyo, katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi
mkoani Simiyu, Agosti 02, 2018.
Mwenyekiti wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Titu Kamani (kulia) na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.
Omary Mgumba(wa tatu kulia)wakiwa na viongozi wengine, wakitembelea mabanda ya
maonesho ya Taasisi mbalimbali, katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 02, 2018.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya
kutembelea banda la maonesho la UTT, katika
Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Agosti
02, 2018
:- Naibu Waziri wa
Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akipokea maelezo kutoak kwaMaafisa wa Wizara ya Fedha,
alipotembelea banda la maonesho la wizara hiyo katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 02, 2018.
0 comments:
Post a Comment