Wananchi
wa Vijiji vya Mkuyuni, Ikungulyabashashi, Mwahalaja na Lulayu Kata ya Ikungulyabashashi,
wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wameishukuru Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa
Daraja la Ikungulyabashashi na kukiri kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutarahisisha
na kuimarisha mawasiliano na usafirishaji.
Hayo
yamebainishwa na baadhi ya wananchi kutoka katika kata Vijiji hivyo mara baada
ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho
kufungua daraja hilo, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani
Bariadi Agosti 17, 2018.
Wamesema awali kabla ya
kukamilika kwa daraja hilo walikuwa
wakipata changamoto ya kusafirisha mazao na mifugo yao na wakati mwingine kusafiri wao wenyewe
hususani kipindi cha masika hivyo kufanya mawasiliano kuwa magumu kati ya pande
mbili zinazotenganishwa na daraja hili.
“Kukamilika kwa daraja hili
kutaongeza uzalishaji kwa kuwa mawasiliano ya pande zote mbili yatakuwa vizuri
tofauti na mwanzo ambapo tulikuwa tunapata shida ya kusafirisha mazao yetu,
mifugo na sisi wenyewe kusafiri kutoka
upande mmoja hadi mwingine hasa wakati wa masika” alisema Joshua Yakobo mkazi
wa Kilalo.
“Tunaishukuru sana Serikali kukamilisha Daraja
hili ambalo litarahisisha sana mawasiliano sasa hivi wakazi wa vijiji vya Kata
ya Ikunguyabashashi watakuwa wanavuka katika daraja hilo kwenda kufanya
biashara katika minada ya Dutwa, Nyakabindi na Bariadi Mjini” alisema Benjamin
Malala.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho alikagua ujenzi wa daraja hilo na
kuridhishwa hatimaye akaupongeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA)
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa kujenga daraja hilo kwa kuzingatia viwango.
Akisoma taarifa ya Ujenzi wa
Daraja hilo Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini naVijijini(TARURA), Halmashauri
ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Nyamagulula Masatu amesema daraja la
Ikungulyabashashi lenye urefu wa mita 16.8, upana wa mita 6.6 linajengwa kwa
ufadhili wa Department For International Developments (DFID) kwa usimamizi wa
TARURA.
Ameongeza kuwa ujenzi wa daraja
hili utagharimu jumla ya shilingi 345,293,434/= huku akibainisha kuwa faida kuu
ya mradi huu ni kurahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka mashambani kwa
wakulima kwenda kwenye masoko.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi umepita katika miradi minne yenye thamani ya
shilingi milioni 568 ikiwemo mradi wa maji wa Kasoli na Shule ya Msingi Otto
Busese ambayo imejengwa kwa ufadhili wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha
Alliance Ginnery Limited kiilichopo Kasoli Bariadi.
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha
Kuchambua Pamba cha Aliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola amesema kuwa Kampuni yake
inatambua kuwa nayo ni sehemu ya jamii, hivyo imeamua kushirikiana na jamii
katika kuchangia maendeleo ya huduma za jamii katika elimu, afya na maji.
“Tumeshirikiana na jamii katika
kuimarisha huduma za jamii, Kasoli
tumechimba kisima cha maji, tumejenga madarasa mawili na matundu matano ya vyoo
katika kila shule inayotuzunguka, tumejenga Bweni la watoto wa kike katika
shule ya Sekondari Mwamlapa na tunaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha
kuwa tunaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha elimu” amesema Ogola.
Mwenge wa Uhuru unaendelea na
mbio zake mkoani Simiyu ambapo Agosti 18 utakuwa katika Wilaya ya Busega,
Agosti 19 utakuwa katika Wilaya ya Maswa na Agosti 20 utakabidhiwa katika Mkoa
wa Shinyanga.
MWISHO
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akikata utepe
kuashiria ufunguzi wa Daraja la Ikungulyabashashi wilayani Bariadi mkoani
Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17,
2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akifungua
Daraja la Ikungulyabashashi wilayani Bariadi mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa
Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akizungumza
na Wanafunzi wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari
Nyasosi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa
Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akiangalia
kiatu kilichotengenezwa na Kikundi cha Vijana wa Dutwa wilayani Bariadi Mkoani
Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17,
2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwisha
ndoo ya maji Bi. Joyce Paulo mkazi wa Kijiji cha Kasoli wiayani Bariadi mkoani
Simiyu mara baada ya kufungua mradi wa kisima kirefu cha maji Kasoli, wakati Mwenge
wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho na viongozi
wengine w Wilaya ya Bariadi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Festo
Kiswaga(kulia) wakishangilia mara baada ya kiongozi huyo kufungua Shule ya Otto Busese (iliyojengwa
kwa ufadhili wa Alliance Ginnery Limited), wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika
mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Mkimbiza
Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg Ipyana Alinuswe Mlilo akitoa Ujumbe wa Mwenge wa
Uhuru mwaka 2018 katika Shule ya Sekondari Kasoli wiayani Bariadi, wakati Mwenge
wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi
akimkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles
Francis Kabeho, kabla ya kukabidhiwa Mwnge wa Uhuru na Mkurugnezi mwenzake wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi , Ndg. Melkizedeck Humbe Agosti 17, 2018.
Mwananchi
Clement Mlanda akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho huku akiwa amaeshika Mwenge wa
Uhuru, mara baada ya nyumba yake kufunguliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,
Agosti 17, 2018.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Bariadi, Bw. Albert Rutaihwa akisalimiana na Mkimbiza
Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg Issa Abass Mohamed mara baada ya kukabidhiwa
rasmi kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwena Halamshauri ya Wilaya ya
Bariadi, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti
17, 2018.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akitoa Ujumbe
wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 katikaViwanja vya Shule ya Msingi Ikungulyabashashi
wilayani Bariadi, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo,
Agosti 17, 2018.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi (kushoto)
akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Ndg. Melkizedeck Humbe wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake
wilayani humo Agosti 17, 2018
Meneja
wa Wakala wa Barabara Mijini naVijijini(TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi, Mhandisi. Nyamagalula Masatu akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru pamoja na Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akitoa Ujumbe
wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, mara baada ya daraja la Ikungulyabashashi kufunguliwa
na Mwenge wa Uhuru Agosti 17, 2018.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi (kulia)
akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Bariadi , Mhe. Festo Kiswaga mara
baada ya kuupokea kutoka kwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, Ndg. Melkizedeck Humbe, ili aweze kuendelea na itifaki, Agosti 17,
2018.
0 comments:
Post a Comment