Waziri
wa mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina amewaongoza wakazi wa Wilaya ya Meatu na
Mkoa wa Simiyu katika mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani
Meatu Elias Shukia aliyefariki katika ajali ya gari Mkoani Singida akitokea
Dodoma na kusababisha kifo chake na dereva na kusababisha watu wengine watano
kujeruhiwa.
Ajali hiyo imetokea Julai 14 eneo
la Mkiwa Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida ,baada ya gari walilokuwa wakisafiria
aina Toyota landcluser DFPA 0148 la Halmashauri ya Meatu kupasuka tairi na
kupinduka mara tatu na kusababisha vifo hivyo viwili,huku majeruhi wa ajali
hiyo Mkurugenzi Mtendaji, Mwenyekiti wa Halmashauri na Maafisa wa Halmashauri
hiyo walipata majeruhi.
Mpina ametoa pole kwa familia,
wananchi, Chama Cha Mapinduzi na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu na kuwataka
kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa kuondokewa na madiwani watatu na
dereva katika matukio mawili tofauti ya ajali na akawaomba wasifikiri kitu
kingine tofauti juu ya kutokea kwa ajali hizo badala yake wajue kuwa ni mapenzi
ya Mungu.
“ Kuna watu wanaweza wasiamini kuwa
ajali zinaweza zikatokea Meatu kwa muda fupi hivi kama ilivyotokea kwetu,
naomba ndugu zangu wananchi, viongozi tusiingie kwenye mtego huo tujue tu kuwa
haya ni mapenzi ya Mungu kama walivyosema viongozi wetu wa dini kuwa Mungu
ndiye anayejua hatma ya maisha yetu” alisema Mpina.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa pole kwa familia, chama na wananchi kwa msiba
huo na amewaagiza Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kuhakikisha
stahili zote za marehemu zinalipwa kwa wakati kwa familia ya marehemu.
Aidha, amewaomba viongozi wa dini
kufanya maombi kwa ajili ya wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla
kuomba Mwenyezi Mungu kuwaepusha viongozi na wananchi na mitihani ya ajali
iliyotokea mfululizo.
“Wakati tunawaaga madiwani wetu
wale wawili waliofariki kwenye ajali ya kwanza, Mwenyekiti wa Halmashauri
na madiwani wengine walikuwa kwenye matibabu , leo tunamuaga
Mhe. Shukia Mkurugezi na Mwenyekiti wako kwenye matibabu kwa sababu ya majeraha waliyoyapata katika ajali, sisi kama wanadamu tunaamini kwenye ulimwengu wa roho tuna nafasi ya kuomba, niwaombe viongozi wa dini tumwombe Mungu atuepushe na mitihani hii” alisema

Mbunge wa Jimbo la Meatu Salum
Khamis amesema kifo cha mhe. Shukia ni pigo kubwa kwa kata ya Mwanhuzi na
Meatu kwa ujumla kwa kuwa marehemu Shukia enzi za uhai wake alikuwa mtetezi
ndani ya Chama Cha Mapinduzi na wananchi katika shughuli za maendeleo.
Akitoa mahubiri wakati wa ibada ya
Mazishi, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala aliwakumbusha waombolezaji
wote kuishi wakimtegemea Mungu, kwa kuwa kila mtu hapa duniani anaishi kwa
neema ya Mwenyezi Mungu, hivyo wanapaswa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
Marehemu Shukia ameacha mke na
watoto wanne, BWANA ALITOA , BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMINA!
MWISHO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akiweka shada la maua katika
kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia
ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea
Dodoma kikazi, baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo akitoa heshima za mwisho
kwa mwili wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias
Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida
akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani
Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa heshima za mwisho kwa
mwili wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia
ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea
Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akitoa sala wakati wa ibada ya
mazishi aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia
ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea
Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya
Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali
ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi ,kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika
Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mbunge wa Meatu, Mhe. Salum Khamis akitoa salamu za rambirambi katika msiba
wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye
alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma
kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Anthony Diallo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina
na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi wakiteta jambo jambo
kwenye msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias
Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida
akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani
Meatu.
Vijana wa CCM na Vijana wa KKKT Meatu wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili
wa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki
dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi kuelekea
kwenye mazishi yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo (kulia) na Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Anthony Diallo wakiweka shada la maua katika kaburi la
aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye
alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma
kikazi baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Anthony Diallo akitoa salamu za
rambirambi katika msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu,
Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani
Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17,
2018 wilayani Meatu.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi, Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Maswa, Mhe. Paul Jidayi na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt.
Joseph Chilongani, wakiteta jambo jambo
kwenye msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias
Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida
akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani
Meatu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Anthony Diallo na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi
wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai
14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai
17, 2018 wilayani Meatu.
Mama mzazi wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias
Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida
akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani
Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiongoza maombi ya kuuombea Mkoa
wa Simiyu, wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi
wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai
14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai
17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakiwa katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye
alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma
kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu, ibada hiyo ilifanyika . Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Baraka Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiteta jambo na viongozi
wengine wa Dayosisi hiyo kwenye ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya
Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali
ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika
Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa
Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki
dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla
ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakiungana na viongozi wa dini
mkoa wa Simiyu, kuuombea Mkoa huo kabla ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi
wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari
Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika
Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiweka shada la maua katika
kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia
ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea
Dodoma kikazi, baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018
wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akiweka shada la maua katika kaburi la
aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye
alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma
kikazi, baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani
Meatu.
Mbunge wa Jimbo la Meatu Salum Khamis akiweka shada la maua katika kaburi
la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye
alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma
kikazi, baada ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani
Meatu.
Baadhi ya Viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wakiwa
katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu,
Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani
Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika
Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kanisa la Kiinjili Kilutheri
Tanzania Dayosisi ya Kusini Mashariki ya
Ziwa Victoria wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata
ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika
ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika
Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiweka shada la maua katika
kaburi la aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia
ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea
Dodoma kikazi, baada ya mazishi ya
diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiongoza ibada ya mazishi ya
aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye
alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma
kikazi, wakati wa mazishi ya diwani huyo
yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani
Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akizungumza na waombolezaji
katika msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias
Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida
akitokea Dodoma kikazi kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17,
2018 wilayani Meatu.
Baadhi ya ndugu wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu,
Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani
Singida akitokea Dodoma kikazi, wakisikiliza mahubiri ya viongozi wa dini kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika
Julai 17, 2018 wilayani Meatu..
Baadhi ya waombolezaji na ndugu wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi
wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari
Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma kikazi, wakisikiliza mahubiri ya
viongozi wa dini kabla ya mazishi ya
diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akiongoza ibada ya mazishi ya
aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia ambaye
alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea Dodoma
kikazi, kabla ya mazishi ya diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mjane wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias
Shukia ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida
akitokea Dodoma kikazi, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mume wake, kabla
ya mazishi yaliyofanyika Julai 17, 2018 wilayani Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,mhe.Anthony Mtaka akitoa salamu za rambirambi katika
msiba wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwanhuzi wilayani Meatu, Mhe.Elias Shukia
ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari Julai 14, mkoani Singida akitokea
Dodoma kikazi, kabla ya mazishi ya
diwani huyo yaliyofanyika Julai 17, 2018
wilayani Meatu.
0 comments:
Post a Comment