Wadau wa Elimu mkoani
Simiyu wamekiri kuwa kambi za kitaaluma zimekuwa na mchango mkubwa katika
kuuwezesha mkoani huo kushika nafasi ya kumi Kitaifa katika matokeo ya Mtihani
wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2018, kutoka nafasi ya 26 mwaka 2017.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2018 kilichofanyika Julai 24, Mjini Bariadi ambapo pia walimu wa Kidato cha Sita waliowezesha wanafunzi kufaulu kwa alama A na B katika masomo yao wamepongezwa na kupewa zawadi ya fedha taslimu na vyeti.
Kikao hiki kimewashirikisha viongozi na Watendaji wa Serikali ngazi ya Mkoa
na Wilaya, Wakuu wa Shule na walimu wa shule za Sekondari za kidato cha tano na
sita, wadhibiti ubora, Maafisa Elimu Wilaya na Kata, Wenyeviti wa Bodi za
Shule, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Chama cha Walimu na wadau wengine.
Baadhi ya wadau waliochangia katika tathimini
hiyo wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa kuanzisha wazo
la kuwa kambi za kitaaluma ambazo zimeleta mafanikio makubwa na kutoa maoni ya
namna ya kuboresha na kuzifanya kambi hizi kuwa mkakati endelevu katika kuinua
ubora wa elimu mkoani Simiyu.
“Nampongeza sana mkuu wetu wa Mkoa kuja na wazo
hili la kuwa na kambi za Kitaaluma na Mkuu wa Mkoa amesema ni agenda ya kudumu
katika mkoa , kama walimu, wazazi, wanafunzi, sisi viongozi na wadau wengine wa
elimu katika Mkoa wetu tukiendelea kushirikiana, kambi hizi zitabadilisha mfumo
wa elimu na kuufanya mkoa ung’are katika sekta ya elimu” Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe.
“Kambi za Kitaaluma zimechangia kuufikisha mkoa
kwenye nafasi ya 10 Kitaifa lakini nashauri iundwe kamati ya ndogo ya Maafisa
Taaluma kutathmini mazuri na changamoto za kambi za kitaaluma ili tuweze
kuboresha zaidi na kuufanya mkoa kufanya vizuri zaidi” Mwl.Baraka Owawa Katibu
Chama cha Walimu Wilaya ya Bariadi.
Nao viongozi wa madhehebu ya dini walioshiriki
katika kikao hicho cha tathmini wamesema
wanaunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya elimu na wakaahidi
kushirikiana na Serikali kwa kuwa hata vitabu vya dini navyo vinahimiza kupenda
na kuthamini Elimu.
Afisa Taaluma wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo
Simime akitoa tathmini ya matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka
2018 amesema idadi ya wanafunzi waliopata daraja la I imeongezeka kutoka
wanafunzi 43 mwaka 2017 na kufikia 119, daraja la II imeongezeka kutoka 304
mwaka 2017 hadi 451, daraja III toka 325 mwaka 2017 hadi 381.
Aidha, amesema idadi ya wanafunzi waliopata
daraja sifuri imepungua kutoka kutoka wanafunzi 29 mwaka 2017 hadi wanafunzi 14
mwaka 2018 ambapo amebainisha kuwa shule sita kati ya 11 mkoani humo
zimefanikiwa kuondoa daraja sifuri mwaka 2018.
Amesema pamoja na kambi za Kitaaluma mkoa
uliweka mikakati ambayo pia imechangia kuongeza ufaulu kuutoa kwenye nafasi ya
26 mwaka 2017 hadi 10 Kitaifa mwaka 2018,
ambayo ni kuhakikisha walimu wanafundisha vipindi vyote na kufidia vilivyopotea
na kufanya mtihani wa utimilifu (Mock) wa Mkoa na kanda uliowasaidia walimu
kubaini mada zenye changamoto na kufanya mapitiao ya mada hizo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka amewapongeza walimu,wazazi wanafunzi na wadau wote wa elimu waliofanikisha mkoa
kufanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2018, huku
akisisitiza kuendelea kuweka mikakati ya kuboresha uendeshaji wa kambi za
kitaaluma ili waweze kufikia lengo walilojiwekea la kufikia ‘single digit’
nafasi ya 1-9.
Katika kikao hicho pia Mtaka ameagiza kuwa muda
wa wanafunzi wa madarasa ya mtihani katika Shule za Sekondari za
Serikali(Kidato cha nne na cha sita)kuzimiwa taa utakuwa saa sita usiku siyo
saa nne usiku, hivyo akiwataka walimu kuweka utaratibu wa viongozi wa wanafunzi
kuendelea na ratiba kwa niaba yao baada ya ratiba ya walimu inayoishia saa nne
usiku.
Wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2018 walikaa
katika kambi za Kitaaluma kwa muda wa siku 10 mwezi Aprili, aidha wanafunzi wa Kidato
cha nne na Darsa la saba wa mwaka 2018 waliwekwa katika kambi za kitaaluma
mwezi Juni kwa siku 21 kwa ajili ya kujiandaa na mitihani yao ya Taifa.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akifungua kikao cha Tathmini ya Matokeo ya
Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi
kupata alama A na B, ambacho kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Baadhi ya wadau wa elimu mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza
Mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa kikao
cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa
walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B mkoani humo, ambacho
kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Afisa Taaluma Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akitoa
taarifa ya matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2018, katika
kikao cha tathmini ya Matokeo hayo
kilichofanyika Julai 24, Mjini Bariadi.
Katibu wa Chama cha
Walimu( CWT) Mkoa wa Simiyu, Mwl. Said Mselem akichangia hoja katika kikao cha
Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa
walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B mkoani humo, ambacho
kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Baadhi ya Wenyeviti wa
Kamati za Elimu, Afya na Maji za Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kikao
cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa
walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B mkoani humo, ambacho
kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato
cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama
A na B mkoani Simiyu, ambacho kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Mchungaji wa Kanisa la
AICT Bariadi, Amosi Ndaki akichangia hoja katika kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha
Sita mwaka 2016 na pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A
na B mkoani Simiyu, ambacho kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu,
Dkt. Joseph Chilongani akimkabidhi cheti cha pongezi (Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka) Mwl. Makame S. Makame kutoka Shule ya Sekondari
ya Bariadi kwa kuwezesha wanafunzi wa kidato cha Sita mwaka 2018 kufanya vizuri
katika somo la Kiswahili, baada ya kikao cha tathmini ya Matokeo hayo kilichofanyika Julai 24, Mjini
Bariadi.
Baadhi ya wadau wa elimu mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu
wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa kikao
cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa
walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B mkoani humo, ambacho
kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Shekhe wa mkoa,
Mahamoud Kalokola akichangia hoja katika kikao Tathmini ya Matokeo ya Mtihani
wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi
kupata alama A na B mkoani Simiyu, ambacho kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bw.
Donald Magesa wakati wa kikao
cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa
walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B mkoani humo, ambacho
kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akimkabidhi cheti cha pongezi (Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka) Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyaranja wilayani Meatu Mwl. Leticia Kalekwa kwa shule hiyo kushika nafasi ya tatu Kimkoa katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2018 , baada ya kikao cha tathmini ya Matokeo hayo kilichofanyika Julai 24, Mjini Bariadi.

Dkt. Joseph Chilongani(katikati walioketi) (Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa
wa Simiyu, wakuu wa Shule za Kidato cha tano na sita na Maafisa Elimu Kata, baada
ya kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na
pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B, ambacho
kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi akichangia
hoja katika kikao Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016
na pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B mkoani Simiyu,
ambacho kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu,
Dkt. Joseph Chilongani(wanne kulia walioketi) (Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
wa mkoa wa Simiyu, Wenyeviti wa Kamati za Huduma za Jamii za halmashauri, baada
ya kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na
pongezi kwa walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B, ambacho
kimefanyika Mjini Bariadi Julai 24, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu,
Dkt. Joseph Chilongani(wanne kulia walioketi) (Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
wa mkoa wa Simiyu, Walimu walipata vyeti vya pongezi, baada ya kikao cha
Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2016 na pongezi kwa
walimu waliofanikisha wanafunzi kupata alama A na B, ambacho kimefanyika Mjini
Bariadi Julai 24, 2018.
0 comments:
Post a Comment