Tuesday, January 11, 2022

Ajali Mbaya Mkoani Simiyu-Kafulila Atioa Salamu za Rais Samia na Kuomba Utulivu.

Gari iliyokuwa imewabeba waandidhi wa Habari

Mkuu wa Mkoa Simiyu , Mhe. David Kafulila amewapa pole wakazi wa wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kufuatia ajali mbaya ya gari iliyochukua maisha ya watu 14.

" Huu ni msiba mkubwa kwenye historia ya wilaya na mkoa wetu. Kupoteza watu 14 kwa ajali ni msiba mkubwa kitaifa. Nimewasiliana na  Rais, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amepokea taarifa ya ajali hii kwa masikitiko makubwa na amenituma kufikisha kwenu salaamu za pole, na kwamba yupo nasi katika majonzi haya".Amesema Kafulila.

Aidha RC. Kafulila amesisitiza utulivu kwa wananchi wakati taratibu za Serikali zinaendelea.  " Ni ajali mbaya lakini niwaombe utulivu.  Miili 6 kati 14 imetambuliwa na  Marehemu wote sita walikuwa sehemu ya msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Gabriel na hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza tayari ameondoka  na miili hiyo kuelekea Mwanza kwa taratibu zingine. 

Kwetu hapa zoezi la kutambua miili 8 linaendelea.  Hivyo tuendelee kuwa watulivu "... ajali hii imetokea siku moja kabla ya siku iliyopangwa kwajili ya maombi maalum Mkoa wa Simiyu yatakayongozwa na viongozi wa dini zote Mkoani hapa kesho kuanzia saa 3 asubuhi.

Ajali hii imetokea leo 11/1/2022 saa 06.25 asubuhi, Kijiji cha Kalemela katika Barabara ya Musoma- Mwanza ,Wilaya ya Busega. Magari mawili STK 8140 TOYOTA LANDCRUISER iliyokuwa ikitokea Mwanza kwenda Wilaya ya Ukerewe kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza iligongana uso Kwa uso na gari no. T.281 DER TOYOTA HIACE ,iliyokuwa ikitoka Lamadi( Simiyu) kwenda Mwanza.

Mpaka  saa sita mchana,watu 14  wamefariki na kati yao wanawake ni 5 na wanaume 9. Aidha wanahabari 6 waliokuwa kwenye gari la Serikali na dereva wao ni sehemu ya waliofariki. 

Waandishi wa habari Waliofariki ni 

1.Husna Milanzi - ITV

2.Johari Shani - Uhuru Digital

3.Antony Chuwa - Habari leo Digital 

4.Abel Ngapenda - Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza

5.Steven Msengi - Afisa Habari Ukerewe.

Majeruhi wa ajali ni sita, ambapo 2 wapo kituo cha afya NASA  na 4 wamepelekwa hospitali ya Rufaa Bugando.

Majeruhi ni:-

1.Tunu Heman - Freelancer

2 Vany Charles  - Icon TV

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Simiyu Bracius Chatanda chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa magari yote MAWILI ambapo dereva wa LANDCRUISER alianza kuligonga ubavuni gari no T 816 DCY TATA BUS akiwa amehama na kwenda kulia na baadaye kwenda kuligonga gari aina ya Hiace iliyokuwa nyuma umbali wa kama M.38. Kamanda Chatanda amethibitisha vifo hivyo 14 ikiwa ni pamoja na Madereva wote. 

Aidha RC Kafulila amesisitiza kwamba taarifa ya mwisho kuhusu uchunguzi wa ajali itapatikana baada ya Kamati ya Usalama Mkoa kupokea taarifa ya   uchunguzi ya usalama barabarani.Mwisho.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!