Friday, January 14, 2022

Mkoa wa Simiyu Wafanya Kongamano la Maombi, Kuuombea Mkoa!

Kongamano la kuuombea Mkoa wa Simiyu limefanyika hivi karibuni kuuombea Mkoa, ili uweze kuepukana na Majanga mbalimbali kama vile Ukame, Magojwa, Misiba na ajali.Kongamano hilo la maombi limefanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Mji Bariadi. 

 Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amesema ili kupata mafanikio yoyote yale duniani ni lazima kumtanguliza Mungu, sababu ya uzito wa jina lake kwenye hatma yetu,kwani yapo mahubiri ambayo mwenyezi mungu anayahubiri katika maisha yetu kwa vitendo.Upo uwezekano wa sisi kupata neema kwa sababu ya wachache walio na Mungu au kupata matatizo kutokana na wenzetu wachache tulionao.katika kusisitiza hilo Mhe Kafulila alitoa mfano wa Abraham wa kwenye masimulizi ya biblia ambaye alimuomba mwenyezi Mungu na kumsihi zaidi ya mara tatu asiliangamize jiji la Sodoma na Gomora naye Mungu alisikiliza sihi na maombi ya Abrahamun zaidi ya mara tatu. 
 Mhe. Kafulila aliendelea kutoa mfano wa  Yona ambaye kwa kukimbia jukumu alilopewa na Mwenyezi Mungu la kwenda kuwahubiria watu wa Ninanwi alisababisha balaa nadani ya  chombo na bahari kuchafuka kiasi cha kwamba chombo kilitaka kuzama, Wakati hali hii inatokea kila mtu alliyekuwa ndani ya chombo alisali kwa Mungu wake na baada ya Yona kutupwa baharini na kumezwa na samaki chombo kilitulia na kisha Yona kutapikwa katika jiji la Tarshishi.Yote haya yaonyesha kwamba hata tuwe katika hali gani wa kumtegemea ni Mwenyezi mungu nmaye  husikia sala za watu wake.

 Mhe. Kafulila ameeleza kuwa tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, majanga yamekuwa yakitokea mara kwa mara mkoani humo hususani vifo vya viongozi mbalimbali na hata kifo cha msaidizi wake wa karibu,aidha magonjwa, ukame na aksidenti za barabarani kutia ndani ajali iliyotokea 11/1/2022 ambayo ilisababisha vifo vya watu 15 kufikia leo, ni majanga ambayo yameupata mkoa wetu kwa kipindi kifupi cha wakati

."Hivyo nimeona ni vyema sisi sote kwa umoja wetu bila kujali dini wala itikadi tukutane kwa pamoja na kumsihi Mwenyezi Mungu kupitia haya maombi maalum atuepushe na majanga haya yote pamoja na kushukuru kwa baraka ambazo tayari ametupatia". Amesema Kafulila.

 Kongamamo hilo limeshirikisha viongozi wa Dini zote mkoani Simiyu, wananchi na wanakwaya kutoka katika dini zote.Katika kongamano hilo kwaya mbalimbali zilitumbuiza zikiwa na ujumbe wa kumsihi Mwenyezi Mungu atuepushe na majanga yote na kumshukuru kwa baraka ambazo ameupatia Mkoa wa Simiyu.Pamoja na kuuombea mkoa wa Simiyu,viongozi wa dini walimuombea Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan na kumshukuru kwa vipaumbele ambavyo amevipa Mkoa wa Simiyu.

Viongozi wa Dini walisisitiza Amani, Umoja na Upendo pamoja na tabia ya  kumtegemea Mwenyezi Mungu kwani Mungu asipoijenga Nyumba waijengao wafanya kazi bure. Aidha Viongozi hao walisisitiza pamoja na kuwa na dini mbalimbali cha muhimu ni upendo ambapo tukiwa na upendo ni rahisi kuvumiliana na hivyo kutokeza amani. 

Kila Kiongozi wa Dini alipewa eneo la kuliombea ikiwa pamoja na amani na upendo, magonjwa, ukame, ajali na ustawi wa viongozi.

 "Aidha niwashukuru viongozi wote wa dini kwa jinsi mlivyojipanga na kuongoza maombi haya sina cha kuwalipa zaidi niseme ahsanteni sana.Pamoja na kuwashukuru Viongozi wa dini zote,pia niwashukuru Wanakwaya ambao nanyi ni sehemu ya dini kwani kwa nyimbo zenu mmetoa mahubiri tosha".Amesisitiza Kafulila.

Mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akitoa neno la shukrani kwa Viongozi wa dini zote Mkoani Simiyu mara baada ya kongamano la kuuombe Mkoa wa Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!