Monday, January 2, 2017

ZANZIBAR YARIDHIA MATUMIZI YA CHAKI ZINAZOTENGENEZWA SIMIYU

Na Stella Kalinga
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeridhia  kununua na kutumia  chaki zinazotengenezwa na Vijana wa Maswa Family  kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya  Maswa Mkoani Simiyu ili zitumike katika shule zake Msingi na Sekondari.

Kauli ya hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Riziki Pembe Juma alipotembelea kiwanda cha kutengeneza chaki na kujionea namna vijana wa Maswa Family wanavyojishughulisha na utengenezaji wa chaki hizo wilayani humo.

Ziara hiyo ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mkoani Simiyu, imefanyika kufuatia ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Ali Mohamed Shein aliyoitoa wakati wa Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 ya kumtuma Waziri huyo Mkoani Simiyu kuona namna uzalishaji wa chaki unavyofanyika na kuweka utaratibu wa Zanzibar inavyoweza kununua chaki hizo.  

Mhe.Riziki amewataka kuendesha kiwanda hicho kwa ubunifu na kukifanya kuwa endelevu ili kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Tanzania ya Viwanda.

Aidha, Mhe. Riziki ameihakikishia Serikali mkoani Simiyu kuwa Wizara yake itashirikiana na Mkoa huo katika masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya elimu na akaahidi kuwa wizara yake pia itakuwa balozi wa Chaki za Maswa visiwani Zanzibar.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema suala la ushirikiano wa kibiashara uliofanyika juu ya Chaki za Maswa (MASWA CHALKS)  kati ya Mkoa wa Simiyu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ni jambo la kihistoria, la kipekee ambalo limeonesha kuwa Serikali ya Zanzibar inathamini na kuunga mkono juhudi za mkoa huo katika kuinua uchumi wake na Taifa kwa ujumla.

“ Tunamshukuru sana Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kwa heshima aliyotupa viongozi na wananchi wa mkoa wa Simiyu, kwa kutekeleza  ahadi yake ya kumtuma Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kuja kuona utengenezaji wa chaki Maswa na kuweka makubaliano ya matumizi ya chaki hizo Zanzibar naahidi hatutamuangusha, tutatekeleza jambo hili kwa ushirikiano mkubwa” amesema Mtaka.

Mtaka amesema pamoja na kutengeneza Chaki wilayani Maswa, kusindika maziwa Wilayani Meatu mkoa huo umejipanga kuzalisha bidhaa zote ambazo malighafi yake inapatikana hapa nchini na kuyaongezea thamani mazao yote katika wilaya zote za Mkoa huo chini ya Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja”.

Mtaka amewataka  Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kuachana na dhana kuwa bidhaa bora ni zile zinazotoka nje ya nchi chini ya Kauli Mbiu “Buy Tanzania Watanzania tupende vya Kwetu”

 Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Ndg.Peter Bunyongoli amesema Ziara ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya  Mapinduzi wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu ni ishara ya umoja ambao ni njia mojawapo ya kudumisha Muungano, ambapo aliwashauri viongozi wenye dhamana katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuenzi Muungano huo.


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhe.Riziki Pembe Juma amefanya ziara ya siku moja Mkoani Simiyu ambapo alitembelea kiwanda cha chaki Maswa na kufungua nyumba ya walimu moja ambayo wataishi watu sita (six in one) kwa wakati mmoja , vyumba vya madarasa viwili na choo cha walimu matundu mawili (02) ya vyoo katika Shule ya Sekondari ya Jija.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali,Mhe.Riziki Pembe Juma (kulia) akisikiliza maelezo ya namna chaki hizo zinavyotenegenezwa kutoka kwa kiongozi wa vijana wa Kikundi cha Maswa Family kinajojihusisha na utengenezaji  chaki kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa alipotembelea kiwanda hicho wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali,Mhe.Riziki Pembe Juma (wa tatu kushoto) akiangalia chaki zilizotengenezwa  na  vijana wa Kikundi cha Maswa Family alipotembelea kiwanda hicho wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali,Mhe.Riziki Pembe Juma (mwenye ushugni wa bluu) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kutembelea kwanda cha kutengeneza chaki wilaya ya Maswa Mkoani humo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali,Mhe.Riziki Pembe Juma (mwenye ushungii wa bluu) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kutembelea kwanda cha kutengeneza chaki wilaya ya Maswa Mkoani humo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali,Mhe.Riziki Pembe Juma (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kushoto) , viongozi wa wilaya ya Maswa na Vijana wa Maswa Family wanaotengeneza chaki za Maswa(MASWA CHALKS)  baada ya kutembelea kwanda cha kutengeneza chaki wilaya ya Maswa Simiyu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali,Mhe.Riziki Pembe Juma (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kushoto) , viongozi wa wilaya ya Maswa na Vijana wa Maswa Family wanaotengeneza chaki za Maswa(MASWA CHALKS)  baada ya kutembelea kwanda cha kutengeneza chaki wilaya ya Maswa Simiyu.
Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndg.Issa Ahmed Rashid (kulia) akihoji jambo mara baada ya kupata maelezo na kujionea jinsi Chaki za Maswa zinavyotengenezwa, wakati wa Ziara ya Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma kiwandani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (wa pili kulia) akizungumza na vijana  wanaotengeneza Chaki za Maswa (Maswa Family) na Viongozi wa Wilaya ya Maswa (hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma wilayani Maswa mkoani Simiyukujionaea utengenezaji wa Chaki za Maswa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg.Fredrick Sagamiko (kulia) akizungumza na vijana wanaotengeneza Chaki za Maswa (Maswa Family) na Viongozi wa Wilaya ya Maswa (hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma wilayani Maswa mkoani Simiyu kujionaea utengenezaji wa Chaki za Maswa.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma(wa pili kushoto) akizungumza na vijana wanaotengeneza Chaki za Maswa (Maswa Family) na Viongozi wa Wilaya ya Maswa (hawapo pichani) wakati wa Ziara yake wilayani Maswa mkoani Simiyu kujionaea utengenezaji wa Chaki za Maswa

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma,(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt. Seif Shekalaghe (kulia) wote wakiwa na maboksi ya Chaki za Maswa (MASWA CHALKS) wakati wa Ziara yake wilayani Maswa mkoani Simiyu kujionaea utengenezaji wa Chaki hizo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma(wa pili kushoto) akionesha alama ya Shirika la Viwango Nchini (TBS) iliyopo katika boksi la chaki za Maswa kuthibitisha ubora wake mbele ya vijana wanaotengeneza  chaki hizo  (Maswa Family) na Viongozi wa Wilaya ya Maswa (hawapo pichani) wakati wa Ziara yake wilayani Maswa mkoani Simiyu kujionaea utengenezaji wa Chaki hizo.
Kiongozi wa Kikundi kinachojishughulisha na kutenegenza Chaki za Maswa cha Maswa Family (kushoto) Kelvin Steven  na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka (kulia) wakimkabidhi katoni  ya chaki Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma(wa pili kulia) mara baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza chaki hizo wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.
Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Jumaakisalimiana na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Maswa mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya ziara ya kutembelea kwanda cha kutengeneza chaki wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa mara baaada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya ziara ya kutembelea kwanda cha kutengeneza chaki, (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
Mkuu wa Shule ya Sekondari Jija akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba ya walimu,vyumba viwili vya madarasa na choo cha walimu  matundu mawili ya vyoo kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma (hayupo pichani) kabla ya waziri huyo kufungua nyumba hiyo wakati wa ziara yake wilaya ya Maswa  mkoani Simiyu.
Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma (kulia) akisoma jiwe la ufunguzi wa nyumba ya walimu aliyoifungua katika Shule ya Sekondari ya Jija wilayani Maswa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma (mwenye ushungi wa bluu) akipokea maelezo na Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa(kulia kwake) kuhusu nyumba ya walimu wanayoweza kuishi walimu sita (six in one) aliyoifungua katika Shule ya Sekondari ya Jija wilayani Maswa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma(wa pili kulia) akiagana na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Maswa baada ya kumaliza ziara yake wilayani humo ambapo alitembelea kiwanda cha chaki na kujionea utengenezaji wa chaki Mkoani Simiyu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma(kushoto) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Maswa baada ya kumaliza ziara yake wilayani humo ambapo alitembelea kiwanda cha chaki na kujionea utengenezaji wa chaki Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma(kushoto) ofisini kwake mara baada ya kuwasls Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara ya siku moja mkoani Simiyu.
Kutoka kushoto,Mku wa Kitengo cha Manunuzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar , Ndg.Issa Ahmed Rashid,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Fredrick Sagamiko, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Katibu wa Waziri na Katibu wa Vijana wanaotengeneza Chaki Wilayani Maswa cha Maswa Family wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mhe.Waziri kuwasili mkoani Simiyu kwa ziara ya siku moja.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ( kushoto) akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma(kulia)  ofisini kwake Mjini Bariadi baada ya Waziri huyo kuwasili Bariadi kwa ajili ya ziara ya siku moja.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa,Mhe.Peter Bunyongoli akizungumza na vijana wanaotengeneza Chaki za Maswa (Maswa Family) na Viongozi wa Wilaya ya Maswa (hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar ,Mhe.Riziki Pembe Juma wilayani Maswa mkoani Simiyu kujionaea utengenezaji wa Chaki za Maswa.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!