Wednesday, December 12, 2018

SIMIYU KUANDAA MWONGOZO WA UWEKEZAJI KWA KILA KIJIJI

Mkoa wa Simiyu umejipanga kuandaa mwongozo wa uwekezaji  kwa kila Kijiji na Mtaa utakaobainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika kijiji na mtaa husika katika vijiji vyote 471 na Mitaa 92 ya wilaya zote tano za Mkoa huu, ikiwa ni maandalizi ya utekelezaji wa Falsafa ya Bidhaa Moja Kijiji Kimoja(OVOP) mwaka 2019/2020.


Hayo yamebainishwa  Desemba 11, 2018 Mjini Bariadi katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Mitaa 92, Watendaji wa Kata 130 na Maafisa tarafa 16 juu ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, kwa kushirikiana na Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF), ambalo pia limewahusisha viongozi na watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa.

Awali akifungua kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa huu unatekeleza Falsafa ya Bidhaa Moja Wilaya ambayo ilianza baada ya ESRF kufanya utafiti na kuibua fursa 26 ndani ya mkoa na sasa inajipanga kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na kuanza utekelezaji wa Bidhaa Moja Kijiji Kimoja.

"Miaka mitatu ya utekelezaji wa Bidhaa Moja Wilaya Moja imetosha, mwaka 2019/2020 ni Bidhaa Moja Kijiji Kimoja, ESRF watatusaidia kufanya utafiti utakaoonesha kila kijiji kina fursa gani; Mkoa wa Simiyu utakuwa mkoa wa kwanza kwenye nchi hii ambao kila kijiji na mtaa utakuwa na mwongozo unaoonesha fursa za uwekezaji za kijiji au mtaa huo" alisisitiza.

Mtaka ameongeza kuwa mara baada ya kukamilisha mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji, mkoa utaandaa utaratibu kwa kushirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) kuona namna ya kuweka teknolojia/mashine zitakazotumika kuongeza thamani mazao ya kilimo, mifugo na mengine yanayopatikana katika kijiji au mtaa husika kulingana na fursa zitakazoainishwa.

Kwa upande wake Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Prof. Samwel Wangwe amesema mkoa wa Simiyu unafanya vizuri katika kilimo hivyo fursa za kuongeza thamani ya mazao ya kilimo zitakuwa kipaumbe cha kwanza, ikifuatiwa na uwekezaji kwenye miradi itakayoleta maendeleo ya binadamu pamoja na mageuzi katika masuala ya kijamii.

Nao Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata wamewapongeza viongozi wa Mkoa kwa maono ya kila kijiji na mtaa kuwa na mwongozo wa uwekezaji  na kuahidi kusimamia kikamilifu fursa zitakazoibuliwa katika maeneo yao, ili ziweze kuleta mapinduzi ya Kiuchumi kwa wakazi wa Simiyu.

" Nimeupokea vizuri sana mpango wa kila kijiji na mtaa kuwa na mwongozo wake wa uwekezaji, binafsi naahidi kusimamia kikamilifu fursa zote zitakazoibuliwa kupitia mafunzo tuliyopewa leo na tafiti zitakazofanywa na wataalam, ili zilete mapinduzi ya Kiuchumi kwa wananchi na mkoa wa Simiyu kwa ujumla" Twaibu Abdul Rashid,  Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinamweli wilaya ya Itilima.

"Tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa kuja na wazo hili ambalo tunaamini tukilisimamia vizuri litainua sana mkoa wetu kiuchumi, maana wananchi watakuwa wanafahamu kuwa ni eneo gani katika kijiji au mtaa wao linaloweza kuwainua kiuchumi kupitia uwekezaji watakapotambua fursa za uwekezaji zilizopo" Amina Yusuph Mtendaji wa Mtaa wa .. Ng'waswale, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo amesisitiza kuwa ili kufikia malengo ya kuinua mkoa huo kiuchumi ni kuendeleza ushirikiano uliopo katika ya viongozi  wa Chama na Serikali na wananchi.
MWISHO 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Kata 130, Maafisa Tarafa 16 katika kongamano lililolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kuibua fursa za uwekezaji, kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, kwa kushirikiana na Wataalam kutoka ESRF, ambalo pia liliwahusisha viongozi na watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa.

Kutoka kushoto mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Prof. Samwel Wangwe na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, wakifurahia jambo mara baada ya kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Kata 130, Maafisa Tarafa 16 wa namna ya kuibua fursa za uwekezaji  kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Prof. Samwel Wangwe akiwasilisha mada kwa Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Kata 130, Maafisa Tarafa 16 juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa mkoani Simiyu, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wataalam kutoka ESRF, Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwemo Watendaji wa Vijiji, mitaa na kata (wenye fulana za rangi ya yachungwa na nyeupe) , baada ya kongamano la kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya namna ya kuibua fursa za uwekezaji, kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Baadhi ya Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani)  katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji hao juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Baadhi ya Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani)  katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji hao juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Baradi, Mhe. Festo Kiswaga wakiteta jambo katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimtambulisha Mtaalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Bw. John Kajiba, katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF)  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani)  katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji hao juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wataalam kutoka ESRF, Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwemo Watendaji wa Vijiji, mitaa na kata (wenye fulana za rangi ya yachungwa na nyeupe) , baada ya kongamano la kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya namna ya kuibua fursa za uwekezaji, kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) akizungumza na Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ofisini kwake, kabla ya  kongamano la kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya namna ya kuibua fursa za uwekezaji, kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Kata 130, Maafisa Tarafa 16 katika kongamano lililolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kuibua fursa za uwekezaji juu ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, kwa kushirikiana na Wataalam kutoka ESRF, ambalo pia liliwahusisha viongozi na watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Kata 130, Maafisa Tarafa 16 katika kongamano lililolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kuibua fursa za uwekezaji juu ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, kwa kushirikiana na Wataalam kutoka ESRF, ambalo pia liliwahusisha viongozi na watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Kata 130, Maafisa Tarafa 16 katika kongamano lililolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kuibua fursa za uwekezaji juu ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, kwa kushirikiana na Wataalam kutoka ESRF, ambalo pia liliwahusisha viongozi na watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa.
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF)  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani)  katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji hao juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wataalam kutoka ESRF, Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwemo Watendaji wa Vijiji, mitaa na kata (wenye fulana za rangi ya yachungwa na nyeupe) , baada ya kongamano la kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya namna ya kuibua fursa za uwekezaji, kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!