Wadau mbalimbali
wa elimu wamechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya
ya Busega mkoani Simiyu katika Harambee iliyofanyika Mjini Nyashimo, ambapo
zimepatikana jumla ya shilingi 254, 969,000/= fedha taslimu zikiwa ni shilingi 15,360,000/=
ahadi shilingi 241,809,000/= na mifuko ya saruji 127.
Akiongea na wadau
hao Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ambaye alialikwa kama
Mgeni rasmi wa Harambee hiyo, Luteni Kanali Josephat Mshashi, Mkuu wa Kikosi
cha 27 Makoko Musoma amesema upo umuhimu wa kuhakikisha watoto wanapata elimu
kwa kuwa elimu ni urithi hivyo kila mmoja awe na uchungu wa kuona watoto
wanasoma.
“Hakuna urithi
tunaoweza kuwapa watoto wetu zaidi ya elimu tusipowapa elimu rasilimali zote
ambazo tunazipigania leo hii, tunavyopambana kulikomboa Taifa letu kiuchumi
itakuwa kazi bure kwa sababu tutabaki na Taifa la watu ambao ni watumwa wa watu
wenye elimu” alisema Mshashi
Awali akitoa
taarifa ya hali ya vyumba vya madarasa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Busega, Bw. Anderson Njinginya amesema halmashauri hiyo ina upungufu wa vyumba
vya madarasa 107.
Mmoja wa Wadau wa elimu
katika Wilaya ya Busega, Bw. Deo Kumalija ambaye alichangia katika harambee
hiyo ametoa wito wadau wa maendeleo na wananchi kuchangia shughuli za maendeleo
katika maeneo waliyopo, ikiwemo ujenzi wa shule kwa kuwa maendeleo yao
yataletwa na wao wenyewe.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
ameupongeza uongozi wa wilaya ya Busega kuandaa harambee hiyo huku akiwataka kusimamia
fedha zilizopatikana, ili zifanye kazi iliyokusudiwa, na kuwasisitiza wazazi,
walezi na jamii yote kwa ujumla kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa
kwenda kidato cha kwanza wanaenda shule.
“Nawapongeza sana
viongozi wa wilaya ya Busega wakiongozwa na Mhe. DC kwa kuandaa harambee hii,
fedha hizi mhakikishe zinasimamiwa vizuri na zifanye kazi iliyokusudiwa, lakini
pia mhakikishe watoto wote waliochaguliwa wanaenda shule, haiwezekani juhudi
kubwa namna hii ifanyike kuchangia halafu watoto wasiende shule” alisema Mtaka.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega Mhe. Tano Mwera amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
kuwa Viongozi watasimamia fedha yote iliyopatikana na kuhakikisha inafanya kazi
itakayokuwa na thamani halisi ya fedha hiyo(value for money).
Akitoa shukrani
kwa viongozi na wadau mbalimbali wa elimu waliochangia katika harambee hiyo Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya Busega, Mhe. Vumi Magoti ametoa wito kwa madiwani kuwahamasisha
wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kata zao, ili fedha
zilizopatikana ziweze kuwasaidia katika ukamilishaji.
Pamoja na kutafuta
wadua wa elimu waliochangia zaidi ya shilingi milioni 70 katika harambee hiyo Mbunge
wa Jimbo la Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni amesema kwa kushirikiana na wadau
ameshatoa vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati 1700 na mifuko ya saruji 640 ambavyo vimeshasambazwa
na kusaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani humo.
MWISHO.
Wadau
wa elimu na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakichangia katika harambee
ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini
Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa
wilayani humo.
Mkuu
wa Wilayaya Busega Mhe. Tano Mwera (kushoto) na Mbunge wa Busega,Mhe. Dkt.
Raphael Chegeni wakiteta jambo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni
kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ambaye alialikwa kama Mgeni rasmi wa
Harambee hiyo, Luteni Kanali Josephat Mshashi, Mkuu wa Kikosi cha 27 Makoko Musoma
akizungumza na wadau wa elimu, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni
kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Wadau
wa elimu na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakichangia katika harambee
ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini
Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa
wilayani humo.
Mdau
wa Maendeleo katika Wilaya ya Busega, Bw. Deo Kumalija akichangia katika
harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega,
iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba
vya madarasa wilayani humo.
Wadau
wa elimu na viongozi mbalimbali mkoani Simiyu wakifurahia katika harambee ya kuchangia
ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo
lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya Busega, Mhe. Vumi Magoti(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, mhe. Dkt. Seif Shekalaghe wakiteta jambo katika harambee ya kuchangia
ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo
lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Wadau
wa elimu na viongozi mbalimbali mkoani Simiyu wakifurahia katika harambee ya kuchangia
ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo
lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akieta jambo na Katibu Tawala
Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini katika harambee ya kuchangia ujenzi wa
vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa
ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(wa pili kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya Busega, Mhe. Vumi Magoti katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba
vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni
kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Kutoka
kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa Wilaya ya Maswa, mhe. Dkt. Seif Shekalaghe
na Mbunge wa Jimbo la Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni wakiteta jambo, katika harambee ya kuchangia ujenzi
wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo
likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi,Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wadau wa elimu katika
harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega,
iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba
vya madarasa wilayani humo.
Baadhi
ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wadau waelimu wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani
Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto
ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wadau wa elimu katika
harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega,
iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba
vya madarasa wilayani humo.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akiwasilisha mchango wa
Sekretarieti ya Mkoa, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni
kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mfanyabiashara
na Mjumbe wa NEC , Bw. Gungu Silanga Shekalaghe akizungumza na wadau wa elimu katika
harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega,
iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba
vya madarasa wilayani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera
akizungumza na wadau wa elimu katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni
kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mdau
wa elimu katika Wilaya ya Busega, Bw. Deo Kumalija akizungumza na wadau wa
elimu wenzake katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa
wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na
changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Huduma za Jamii, Mhe. Mickness Mahela(wa pili kushoto) akiwa na
madiwani wenzake wakiwasilisha mchango wa madiwani katika harambee ya kuchangia
ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo
lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya( wa pili kushoto) na baadhi ya
wakuu wa idara wakiwasilisha mchango wao katika harambee ya kuchangia ujenzi wa
vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa
ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Baadhi
ya wadau wa elimu wakifuatilia harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni
kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Baadhi
ya wadau wa elimu wakifuatilia harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni
kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
Baadhi
ya wadau wa elimu wakifuatilia harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni
kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment