Mkoa wa Simiyu umeidhinishiwa jumla ya
shilingi bilioni 13.1 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na miradi ya maendeleo katika bajeti ya mwaka
2018/2019.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala
wa Barabara (TANROADS)'Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent wakati
akiwasilisha taarifa katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika
Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Kent amesema kati ya fedha hizo shilingi
bilioni 11.461 zimeidhinishwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara kutoka
katika mfuko wa barabara na shilingi bilioni 1.595 utekelezaji wa miradi
12 ya maendeleo yenye urefu wa
kilometa 78.2.
Aidha, Kent amezungumzia maendeleo ya
ujenzi wa daraja la mto Sibiti na kubainisha kuwa ujenzi wake umefikia asilimia
85 na jitihada zinaendelea kufanyika, ili ifikapo mwezi Machi, 2019 liwe
limekamilika kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. John Pombe Magufuli mwezi Septemba, 2018 wakati akiweka jiwe la msingi la
ujenzi wa daraja hilo.
Naye Mratibu wa Wakala wa Barabara
Mijini na Vijijini (TARURA), Mhandisi. Salvatory Yambi amesema katika bajeti ya
mwaka 2018/2019 Mkoa wa Simiyu umeidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni
5.4 na kubainisha kuwa hadi sasa TARURA inaendelea kutekeleza miradi 29
yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3.6 ambayo ipo katika hatua
mbalimbali za utekelezaji.
Awali akifungua kikao cha Bodi ya
Barabara kwa niaba ya Mwenyekiti wa kikao hicho na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amepongeza
TANROADS na TARURA kwa kazi kubwa wanayoifanya mkoani humo, hususani katika
kusimamia ujenzi na matengenezo barabara hali iliyochangia kuufungua mkoa na
kuchochea kukua kwa uchumi.
Akichangia hoja katika kikao hicho,
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge ameshauri kuwepo na uhusiano wa karibu
kati ya TARURA na Halmashauri hususani katika maandalizi ya Bajeti, ili
vipaumbele vya TARURA vizingatie vipaumbele vya Halmashauri ambao ndio
wanaokutana na wananchi moja kwa moja na kujua mahitaji yao.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa Simiyu,
Jumanne Sagini ametoa wito kwa Wakurugenzi wa halamshauri kutenga fedha kwa
ajili ya matengenezo ya barabara ambazo haziko chini ya TARURA hususani katika
kipindi hiki cha maandalizi ya bajeti.
Katika kikao hiki pia wajumbe mbalimbali
walipata nafasi ya kuchangia hoja ambazo zililenga kuboresha miundombinu ya
barabara na madaraja, masuala yote ambayo Mhandisi Kent alieleza kuwa
yatafanyiwa kazi na yanayohitaji hatua zaidi kutoka katika wizara yenye dhamana
yatafikishwa.
"Nashauri wananchi washirikishwe
katika zoezi la uwekaji wa alama za vivuko wakati barabara ya Maswa-Bariadi
itakapokamilika ili viwekwe mahali penye uhitaji" Mkuu wa Wilaya ya Maswa,
Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe
"Ili daraja la Sibiti liweze kuleta
tija zaidi tunaomba TANROADS iandae mpango wa dharura wa kujenga daraja la Mto
Itembe ili kuwaondolea adha wananchi
waweze kuvuka kutoka eneo moja kwenda kwingine pindi mvua
zinaponyesha." Mhe. Leah Komanya, Mbunge wa Viti Maalum CCM.
Mwenyekiti Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Mhe. Robert Lweyo ameshauri ijengwe round about (mzunguko) Mjini Bariadi katika
makutano ya barabara ya Ngulyati-Bariadi, Lamadi- Bariadi na Maswa-Bariadi,
jambo ambalo Mhandisi Kent aliahidi kuliandikia barua na na kuliwasilisha
katika wizara yenye dhamana na ujenzi.
Meneja wa Wakala wa
Barabara(TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent akiwasilisha taarifa
yake ya Mkoa katika kikao cha Bodi ya barabara , kilichofanyika Desemba 14,
2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha bodi ya barabara kwa niaba ya
Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo
pichani), kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Mratibu wa Wakala wa
Barabara mijini na Vijijini(TARURA)Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Salvatory Yambi taarifa
yake ya Mkoa katika kikao cha Bodi ya barabara , kilichofanyika Desemba 14,
2018 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo katika kikao cha Bodi ya barabara
, kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa
Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kwa makini masuala
mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao hicho, Desemba 14, 2018 Mjini
Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la
Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya barabara
mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Mbunge wa Viti Maalum
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Leah Komanya akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya
barabara , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kwa makini
masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao hicho, Desemba 14, 2018
Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe. Tano Mwera(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt.Seif
Shekalaghe wakitelezana jambo, katika kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu
, kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa
Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kwa makini masuala
mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao hicho, Desemba 14, 2018 Mjini
Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo(kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe.
Andrew Chenge wakiangalia kwa makini taarifa zilizopo katika makablasha ,
wakati wa kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba
14, 2018 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa
Halamshauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja katika kikao
cha Bodi ya barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini
Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa
Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kwa makini masuala
mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao hicho, Desemba 14, 2018 Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya
barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Nsimeki akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya
barabara mkoa wa Simiyu , kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment