Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema wakati umefika kwa kamati na bodi
za Shule mkoani humo kujitathmini ikiwa zinafaa kuendelea na majukumu yao au
kujiuzulu pale Shule zao zinapofanya vibaya katika mitihani hususani ya Taifa.
Mtaka
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule za Halmashauri ya Mji Bariadi na
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari
Bariadi, katika kikao maalum
kilicholenga kujadiliana na kupanga
maandalizi ya Kambi za kitaaluma kwa Kidato cha Nne na Darasa la Saba Wilayani humo.
Amesema mara nyingi
wanafunzi wanapofanya vibaya kwenye mitihani wazazi wengi wamekuwa wakiwalaumu na
kuwanyoshea vidole walimu badala ya kutathmini mchango wao katika ufaulu wa
watoto wao.
“ Watoto wakifeli
mnaanza kuwanyoshea walimu vidole, huu mwaka watoto wakifeli kamati za shule
zijiuzulu, mnapowanyoshea walimu vidole hivi kamati za shule zenyewe huwa zinachukua
wajibu gani, jiuzuluni ili waje wazazi wengine wenye mawazo mapya yatakayozivusha
shule kwenda kwenye ufaulu mzuri” alisisitiza Mtaka.
Mtaka amewataka wazazi
washikamane na Serikali pamoja na walimu katika kuhakikisha wanafanya mapinduzi
ya Elimu kwa kuwa ufaulu wa wanafunzi unategemea ushirikiano wa wazazi, walimu na wanafunzi wenyewe, hivyo akasisitiza kuwa Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule wakafanye
vikao na wazazi kuweka mipango mizuri ya kufanikisha kambi za kitaaluma kwa
wanafunzi wa kidato cha nne na darasa la saba pamoja na maendeleo ya elimu kwa
ujumla.
Aidha, kama Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na
Usalama ya Mkoa Mtaka amewahakikishia wazazi kuwa wanafunzi wote watakaokuwa
katika kambi watatunzwa na kulindwa huku akiwatahadharisha watu wenye nia mbaya
kutowafuatilia wanafunzi wa kike kwa lengo la kuwarubuni kwa namna yoyote kwa
kuwa Serikali itawachukulia hatua wote watakaobainika.
Mtaka amesisitiza
wazazi wote kuchangia mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi watakaokuwa kambini ili
kuwezesha kambi hizo kufanyika hususani chakula, huku akiwaeleza wazazi kuwa
kupitia kambi hizo watarajie kuona mabadiliko ya kitaaluma kwa watoto wao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amezitaka Kamati na Bodi za Shule wilayani humo
kufanya vikao na Wazazi kwa ajili ya kuwaeleza wajibu wao katika kufanikisha
Kambi hizo za Kitaalamu na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo Mei
30, 2018 ofisini kwake.
Kiswaga amesema Kamati
zote ambazo zitashindwa kutekeleza agizo hilo zitavunjwa na Wenyeviti na
wajumbe wa Kamati hizo watawajibishwa
.
Wilaya ya Bariadi
itazindua rasmi kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne na Darasa la Saba Juni 06
mwaka huu.
MWISHO:
Baadhi ya Wenyeviti wa
Bodi na Kamati za Shule wa Wilaya ya Bariadi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao maalum cha maandalizi
ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la saba
zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika
Shule ya Sekondari Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule za Wilaya ya Bariadi (hawapo
pichani) , katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa
wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi
Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya Sekondari Bariadi
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule za Wilaya ya Bariadi (hawapo
pichani) , katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa
wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi
Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya Sekondari Bariadi
Baadhi ya Wenyeviti wa
Bodi na Kamati za Shule wa Wilaya ya Bariadi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao maalum cha maandalizi
ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la saba
zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya
Sekondari Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifurahia jambo katika kikao maalum cha maandalizi
ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba
zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya
Sekondari Bariadi, (kulia) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw.
Melkezedeck Humbe.
Baadhi ya Wenyeviti wa
Bodi na Kamati za Shule wa Wilaya ya Bariadi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao maalum cha maandalizi
ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la saba
zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya
Sekondari Bariadi.
0 comments:
Post a Comment