Wananchi
takribani 1000 wa Kata ya Malambo wilayani Bariadi wakiongozwa na Mkuu wa
Wilaya hiyo, Mhe.Festo Kiswaga wamejitokeza kuchimba msingi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mkoa wa Simiyu
ambayo inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi huu .
Wakizungumza
katika nyakati tofauti baadhi ya wananachi walioshiriki katika zoezi hilo
wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa maono yake katika
kuleta maendeleo ya elimu mkoani humo na kuahidi kuwa watahakikisha wanamuunga
mkono ili malengo ya kuwa na shule ya vipaji maalum yanatimia.
“Tunamshukuru
Mkuu wetu wa Mkoa kwa kuja na maono haya ya kuwa na shule ya Ufundi ya Mkoa na
sisi kama wananchi wa eneo hili
tunamuunga mkono kiongozi wetu, nitoe wito kwa wananchi wenzangu kila
mmoja aweze kuchangia alicho na uwezo nacho
ili tuweze kujenga shule yetu hii ikamilike na watoto wetu waanze
kusoma” alisema Christina Matulanya Mkazi Malambo Bariadi.
Diwani
wa Kata ya Malambo Mhe.Kitebo Kitebo amesema wananchi wa Kata ya Malambo kwa
pamoja wameonesha ushirikiano toka walipotangaziwa kwa mara ya kwanza juu ya
kuanza kwa ujenzi wa shule hiyo, hivyo akawaomba kuendelea kushirikiana mpaka shule
hiyo ikamilike.
Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amewashukuru wananchi wake na akawaomba
waendelee kuonesha ushirikiano katika kufanikisha ujenzi wa shule hiyo ili wawe
mfano bora kwa wilaya nyingine zitakapoanza kujenga shule za vipaji maalumu
pia.
Katibu wa
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bariadi Nicholaus Kasendamila amesema Jitihada
hizo za Ujenzi wa Shule hiyo ya Mkoa zilizoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu lazima ziungwe Mkono ambapo amewataka Wananchi kuweka pembeni
siasa kwenye suala hilo la Maendeleo
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ambaye aliwatembelea Wananchi hao
amesema Kuwepo kwa Shule hiyo ya Ufundi kutaleta chachu kubwa katika
kuwapata watalaam wa fani mbalimbali katika utekelezaji wa azma ya Serikali ya
awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda na akawataka wazazi kuwasisitiza watoto
wao kusoma kwa bidii.
“Mkoa wa
Simiyu unajipambanua kama Mkoa wa viwanda ni lazima tuwe na shule ambazo watoto
wetu kwenye mitaala yao wanapomaliza kidato cha nne wanakuwa na stadi za ufundi
za kujiendeleza kimaisha, tunataka tujenge shule yenye karakana nzuri za ufundi
watoto watakaopita hapa waweze kuendesha maisha yao, tunataka shule hii ijibu
mahitaji ya mkoa” alisema.
Aidha, Mtaka
amesema hadi sasa wadau mbalimbali wamejitokeza kuchangia shule hiyo na mpaka
sasa jumla ya shilingi milioni 157 zimetolewa na wadau hao ili kuunga mkono
ujenzi wa shule hiyo na Serikali imetenga jumla shilingi milioni 58 kwa ajili
ya ujenzi wa Jengo la Utawala.
Ameongeza
kuwa baada ya kukamilisha shule hiyo ya Ufundi, Mkoa huo unatarajia kujenga
shule ya Wasichana , Shule ya Wavulana na shule maalumu ya mchepuo wa Kilimo
ambayo itatumika kama sehemu ya mazoezi kwa vitendo kwa Chuo cha Kilimo
Sokoine(SUA).
MWISHO
Baadhi ya wananchi wa kata ya Malambo Mjini Bariadi Mkoani Simiyu ,
waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya
Ufundi Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi huu, wakifurahia jambo na Mkuu
wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka alipowatembelea wakati wakiendelea na zoezi
hilo la kuchimba msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata
ya Malambo Wilayani Bariadi, waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa mabweni
ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu, inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi
huu.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Malambo Mjini Bariadi , waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa
mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa
mwezi huu.
Diwani wa Kata ya Malambo, Mhe.Kitebo Kitebo akizungumza na wananchi wa
Kata ya Malambo Wilayani Bariadi, waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa
mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa
mwezi huu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa
Kata ya Malambo Wilayani humo, waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa
mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa
mwezi huu.
Bibi. Christina Matulanya Mkazi wa Malambo Mjini Bariadi akizungumza na
wananchi wenzake wa Kata ya Malambo
Wilayani Bariadi, waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa mabweni ya Shule
ya Sekondari ya Ufundi Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi huu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bariadi, Bw. Nicholaus Kasendamila akizungumza na
wananchi wa Kata ya Malambo Wilayani Bariadi, waliojitokeza kuchimba msingi wa
ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu inayotarajiwa kuanza
kujengwa mwezi huu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bw. Donald Magesa akizungumza na wananchi wa
Kata ya Malambo Wilayani Bariadi, waliojitokeza kuchimba msingi wa ujenzi wa
mabweni ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa
mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment