Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango Dodoma limeushukuru ,
uongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kukubali kutoa eneo la ekari 50 bure kwa ajili ya
ujenzi wa Tawi jipya la chuo hicho , katika Kata ya Nyakabindi Halmashauri ya Mji
wa Bariadi.
Shukrani
hizo zimetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango
Bibi.Mugabe Mtani , katika mazungumzo maalum na viongozi wa Mkoa wa Simiyu muda
mfupi kabla ya kikao cha Baraza hilo kilichofanyika mkoani Simiyu.
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa
Chuo cha Mipango Bibi. Mugabe Mtani ameshukuru kwa niaba ya Chuo
hicho kwa kupewa eneo hilo ambalo
litawawezesha kujenga miundombinu ya kutosha ya chuo hicho katika Mkoa wa
Simiyu.
“Tunashukuru sana uongozi wa Mkoa wa Simiyu
kwa kutupa hili eneo kubwa katika wakati huu ambao sisi tunaona ni wakati
muafaka kwa sababu tulikuwa kwenye mkakati wa kutafuta eneo la kujenga, pale
Mwanza tuna eneo ambalo kama tungelitumia lingetugharimu fedha nyingi kuliko
hili la Simiyu kwa sababu liko kwenye mawe” alisema Mtani.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango,
Hozen Mayaya amesema iwapo chuo hicho kitakamilika kujengwa kitasaidia
kutoa mafunzo ya maendeleo vijijini na hivyo kusaidia upatikanaji wa watalaam
hapa nchini wakiwemo wa mipango pamoja na kusaidia katika ufanyaji wa tafiti
mbalimbali.
Ameongeza
kuwa upatikanaji wa eneo hilo utasaidia lengo la Chuo la kuwa vituo vingi kadri
mahitaji yanavyoongezeka jambo ambalo litasaidia pia kusogeza huduma karibu na
wananchi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambako eneo hilo lipo, Bw. Melkizedeck Humbe amesema
Chuo cha Mipango kitapojengwa Mkoani Simiyu kitakuwa msaada mkubwa kwa Mkoa huo
ambao unajipambanua kwa Uchumi wa viwanda.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema kuwepo kwa chuo hicho kutaongeza hamasa ya elimu kwa vijana
wanaomaliza elimu ya sekondari na kidato cha sita kujiunga na vyuo vya
elimu ya juu ,huku akitoa wito kwa Taasisi zingine za umma na binafsi
kuwekeza katika sekta ya elimu.
“ Sisi
kama Mkoa tunatoa fursa kwa Wakuu wote wa Vyuo Vikuu hapa nchini wanaotaka
kujenga matawi ya Vyuo vyao ili waondokane na kulipa fedha nyingi kwa ajili ya
pango la majengo, mkoa wa Simiyu unawaakaribisha na tunawahakikishia
upatikanaji wa Ardhi Bure” alisema Mtaka.
MWISHO:
Kaimu Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango Bibi. Mugabe Mtani akizungumza
na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya
kikao cha Baraza hilo na kuona eneo
lililotolewa na Mkoa huo kwa ajili ya kujenga Tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Mipango Hozen Mayaya akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu
mara baada ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya kikao cha Baraza la Uongozi
wa Chuo hicho na kuona eneo lililotolewa
na Mkoa huo kwa ajili ya kujenga Tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg Jumanne Sagini akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Uongozi
wa Chuo cha Mipango waliofika Mkoani humo kwa ajili ya kikao
cha Baraza hilo na kuona eneo lililotolewa na Mkoa huo kwa ajili ya kujenga
Tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu.
Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akiwakaribisha wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha
Mipango waliofika Mjini Bariadi kwa ajili ya kikao cha Baraza hilo na kuona eneo
lililotolewa na Mkoa wa Simiyu kwa ajili
ya kujenga Tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu.
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo
cha Mipango Bibi. Mugabe Mtani akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya kikao cha Baraza
hilo na kuona eneo lililotolewa na Mkoa huo kwa ajili ya kujenga Tawi la Chuo
hicho mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg Jumanne Sagini akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe wa Baraza la
Uongozi wa Chuo cha Mipango waliofika
Mkoani humo kwa
ajili ya kikao cha Baraza hilo na kuona eneo lililotolewa na Mkoa huo kwa ajili
ya kujenga Tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu,
Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kulia), Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
wa Chuo cha Mipango Bibi. Mugabe Mtani (kushoto) wakifuatilia bbadhi ya hoja
zilizokuwa zikiwasilishwa na wajumbe wa Baraza hilo waliofika Mjini Bariadi kwa
ajili ya kikao cha Baraza hilo na kuona
eneo lililotolewa na Mkoa huo kwa ajili ya kujenga Tawi la Chuo hicho mkoani
Simiyu.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango Hozen
Mayaya(kulia) na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho
wakifuatilia mazungumzo kati ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na Kaimu Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho Bibi. Mugabe Mtani (hawapo pichani)
walipofika Mjini Bariadi kwa ajili ya kikao cha Baraza hilo na kuona eneo
lililotolewa na Mkoa huo kwa ajili ya kujenga Tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment