Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa
wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini alipokutana na Kamati ya Maadalizi ya Maonesho Nanenane
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambao walitembelea uwanja huo na kupewa eneo
ambalo litatumika na wizara hiyo kuonesha shughuli zake.
Sagini amesema viongozi wa Mkoa kwa kushirikiana
na viongozi wa Taasisi nyingine za Serikali wameshafanya mazungumzo na kuweka
mipango ya namna kila Taasisi itakavyoshiriki katika kuhakikisha miondombinu ya
maji, umeme na barabara inawekwa vizuri ili kufanikisha Maonesho hayo
“Tumeshazungumza na TANESCO na wako
tayari kuteremsha Transifoma kwenye eneo lile ili tupate umeme, tumezungumza na
Mamlaka za Maji ili tupate fedha za kuchimba kisima kirefu cha maji ya
kutosheleza wadau wetu na kuhusu barabara tumezungumza na TANROADS na TARURA,
tunatarajia wiki mbili zijazo mambo yatakuwa tofauti pale” alisema Sagini.
Aidha, Sagini amesema pamoja na
kushughulikia miundombinu, Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambayo inaunda
Kanda ya Nanenane ya Ziwa Mashariki, imeshafanya vikao vya wataalam na kuweka
mipango mbalimbali ya kufanikisha maonesho hayo na akabainisha kuwa Mei 17, kitafanyika kikao kikuu cha maamuzi kwa lengo
la kufikia maamuzi ya nini kinafanyika kwa wakati gani na nani atakayefanya.
Wakizungumza mara baada ya kutembelea eneo la Uwanja wa Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki, wawakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na kupongeza uongozi wa mkoa kwa juhudi
zinazofanyika, kuridhishwa na hali ya maandalizi ya uwanja wameshauri kasi ya
maandalizi iongezeke ili kuendana na muda uliobaki kuelekea maonesho.
“Viwanja tumeviona viko mahali pazuri na eneo tumepewa, kwa muda uliobaki
tunashauri waongeze speed(kasi) wameshaanza kugawa maeneo kwa wadau na
wameshaanza kuyasafisha, lakini waharakishe kuweka miundombinu ya maji,barabara
na umeme” alisema Merry Yongolo Mratibu wa Maonesho ya Nanenane Wizara ya
Mifugo na Uvuvi.
“Natoa pongezi kwa Mkoa wa Simiyu kwa kukubali kuwa mwenyeji wa Nanenane mwaka
huu hii ni fursa waitumie, sisi kama wizara pia tunaona hii ni fursa hasa
katika kukutana na wafugaji na wavuvi na kutatua changamoto zinazowakabili; ili
tuweze kufanikisha maonesho haya maandalizi ya mapema ni muhimu sana alisema
Dkt. Khamis Mkuli kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Naye Mkurugenzi wa shughuli za
utafiti Kanda ya Ziwa Moses Ngendelo amesema katika maonesho hayo wanatarajia
kuonesha teknolojia mpya ambazo zitawasaidia wafugaji, wakulima na wavuvi
kuongeza tija katika uzalishaji, hivyo akatoa wito kwa wakulima, wafugaji na
wavuvi kushiriki maonesho hayo ili waweze kuona teknolojia hizo.
Hivi karibuni Wizara ya kilimo imetangaza Kanda Mpya ya Maonesho ya Nanenane
ijulikanayo kama Kanda ya Ziwa Mashariki, ambayo inajumuisha mikoa ya Simiyu,
Mara na Shinyanga na Uwanja utakaotumika kwa ajili ya Maonesho hayo uko Eneo la
Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada wajumbe wa kamati ya Maandalizi
ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara ya mifugo na Uvuvi kutembelea Uwanja wa
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini Bariadi
Mkoani humo.
Bi. Merry Yongolo Mratibu wa Maonesho ya Nanenane Wizara ya Mifugo na Uvuvi
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya wajumbe wa
kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara hiyo kutembelea Uwanja
wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Dkt. Khamis Mkuli kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ziara ya wajumbe wa kamati ya
Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara hiyo katika Uwanja wa Maonesho ya
Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo
Nyakabindi, Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya watalaam wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wakiendelea na kusafisha eneo lao kwa kutumia greda
katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi,
Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, ikiwa ni
maandalizi ya Maonesho hayo yatakayofanyika Kitaifa mkoani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini (kulia) akiwaonesha baadhi ya
viongozi na wataalam kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga eneo la Uwanja
wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziawa
Mashariki uliopo Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani humo, wakati wa ziara yao
walioifanya hivi karibuni mara baada ya kufanya kikao cha pamoja.
0 comments:
Post a Comment