Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), William Mwakilema amesema Uwanja
wa Ndege Simiyu unaotarajia kujengwa
Eneo la Igegu wilayani Bariadi utakapokamilika utaongeza huduma za Utalii katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti.
Mwakilema
ameyasema hayo wakati ziara ya Balozi wa
Indonesia hapa nchini , Prof.Dkt. Ratlan
Pardede na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mei
16 ili kujionea wanyama na vivutio
mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo.
Amesema
Hifadhi ya Serengeti ina uwanja ambao unaowezesha ndege ndogo kutua hivyo, ujenzi
wa uwanja wa Simiyu utakaowezesha ndege
kubwa kutua itakuwa ni nyongeza ya huduma, ambapo ndege kubwa zitakapotua Simiyu watalii ambao
hawawezi kutembea mwendo mrefu kwa kutumia magari, watachukuliwa na ndege ndogo
kutoka Simiyu na kupelekwa Seronera(Serengeti).
Ameongeza
kuwa, kuwepo kwa uwanja huo kutasaidia
kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za Utalii, ambapo wafanyabiashara wengi wa huduma za Utalii watavutiwa kuwekeza
mkoani Simiyu kwa ajili kutoa huduma kwa wageni watakaotua uwanjani hapo na
wanaoenda kufanya utalii Serengeti.
Aidha,
Mwakilema amesema Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inaendelea
kushirikiana na Mkoa wa Simiyu kuhakikisha kuwa rasilimali zote ndani ya
hifadhi ziko salama na zinaendelea kutunzwa ili Taifa liweze kunufaika kiuchumi kupitia
utalii.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mpango wa Mkoa huo ni kufikisha kwa
wepesi huduma za Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo mkoa
umepanga kujenga uwanja huo wa ndege katika Eneo la Igegu wilayani Bariadi
ambalo liko karibu kabisa na Hifadhi hiyo.
“Tumepanga
kujenga Uwanja wa Ndege pale Igegu ili kufikisha huduma za utalii kwa wepesi
katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na mwaka huu wa fedha 208/2019 tumetengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa
uwanja huo utakaokuwa na ukubwa wa
kilometa 2.5, pia sisi kama mkoa
tutahakikisha tunafungua malango yote ya watalii kuja kwenye vivutio vyetu”
alisema Mtaka
“Tunapokamilisha
miundombinu ya barabara ya Lamadi-Bariadi-Maswa-Mwigumbi ni pamoja na kuona
namna tutakavyounganisha ufunguaji wa
barabara zitakazowezesha watu kwenda kwenye hoteli zote za kitalii zilizojengwa
ndani ya hifadhi hasa zilizo katika eneo letu, ili huduma za utalii
zirahisishwe” alisisitiza.
Kwa
upande wake Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti amesema atazungumza na Wafanyabiashara wa Indonesia na kuwaalika
kuwekeza katika Sekta ya Utalii nchini Tanzania hususani Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti, huku akisisitiza kutoa wito kwa wananchi wa Indonesia kutembelea
Hifadhi ya Serengeti ili kuja kujionea vivutio mbalimbali vya utalii.
Balozi
wa Indonesia, Prof. Dkt. Ratlan Pardede amehitimisha ziara yake kikazi mkoani
Simiyu ambapo ameahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Indonesia na Tanzania na
hasa Mkoa wa Simiyu katika masuala ya kilimo na biashara ya zao la pamba,
uwekezaji wa viwanda vya nguo, bidhaa za ngozi na mbolea pamoja na utalii.
MWISHO
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), William Mwakilema akizungumza
na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara
yao katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mei 16
ili kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi
hiyo
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), William Mwakilema(kulia) akitoa
maelezo juu ya uwanja mdogo wa ndege wa hifadhi hiyo (Seronera) kwa Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof.
Dkt. Ratlan Pardede na Viongozi wa Mkoa
wa Simiyu wakati wa ziara yao katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mei 16 ili kujionea wanyama na vivutio mbalimbali
vya utalii katika hifadhi hiyo.Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), William Mwakilema (kushoto) akiwaongoza Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (katikati) na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuelekea eneo la kupokea taarifa wakati wa ziara yao katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mei 16 ili kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), William Mwakilema (katikati) akiwaongoza
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (wa pili kulia) kuelekea eneo
la kupokea taarifa wakati wa ziara yao katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mei
16 ili kujionea wanyama na vivutio
mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) na baadhi
ya viongozi wa Mkoa wa huo wakati wa ziara ya Balozi wa Indonesia hapa nchini,
Prof. Dkt. Ratlan Pardede na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti Mei 16 ili
kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akiteta jambo na Balozi wa
Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede wakati wa
ziara ya Balozi huyo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mei 16 ili kujionea wanyama na vivutio mbalimbali
vya utalii katika hifadhi hiyo.
Balozi
wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede akizungumza
na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), William Mwakilema
na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake katika Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti Mei 16 ili kujionea wanyama na
vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo.
Balozi
wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (kushoto) akiangalia wanyama Mamba na Viboko katika Mto Grumeti wakati wa ziara
yake katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mei 16 ili kujionea wanyama na vivutio mbalimbali
vya utalii katika hifadhi hiyo.
Baadhi
ya Tembo waliopo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambao ni moja ya vivutio vya utalii katika hifadhi hiyo.
0 comments:
Post a Comment