Viongozi wa wananchi, wenyeviti wa vitongoji na vijiji 120 vya
wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wameridhia mchango wa shilingi elfu hamsini kila
kaya kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambao utatolewa kwa mwaka, ambapo baada
ya kaya kutoa mchango huo hazitachangia mchango mwingine wowote.
Hayo wameyasema katika
mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Nguzo nane Mjini Maswa baina ya
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na viongozi wa vitongoji ,vijiji
na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi Mkoa, viongozi wa dini na wananchi, lengo likiwa ni
kujadili azimio lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa
la Uchangiaji shughuli za maendeleo hususani ujenzi wa miundombinu ya elimu na
afya.
“Kwanza ni vizuri ikafahamika kwamba viongozi wa wananchi
wameridhia mchango, hii habari ya nani kasema hapana ni lazima tutoe uhuru wa
kutoa maoni, sidhani kama ingekuwa sahihi tuje hapa tuamue kuwa haya ni maelekezo;
lakini pili hatujasema adhabu kuwa asiyetoa mchango huu atafanywa nini
waandishi wa habari saidieni kuondoa uzushi huu kwenye mitandao” amesema Mtaka.
Mtaka amesema ni vema ikafahamika wazi kuwa baada ya kaya kutoa mchango huu wananchi hawatachangiswa mchango
wowote, huku akisisitiza kuwa mchngo huu hautazihusu zilizo chini ya Mpango wa
Kunusuru kaya Maskini TASAF III pamoja na kaya za wananchi walio katika
misamaha mbalimbali ya Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akihitimisha mkutano huo amesema uamuzi wa
kuwa na mchango huo umetokana na kuona wananchi wamekuwa wakichangishwa
michango mingi ya rejareja ambayo ilikuwa ikizidi kiasi cha shilingi elfu 50, hivyo Halmashauri ikaona ipo haja ya kuwa na
mchango mmoja ambao utakuwa na unafuu.
“Huu mchango ni sawa
na michango mingine ambayo Wananchi wamekuwa wakichangia siku zote kwa ajili ya
shughuli za maendeleo, lakini sasa hivi Halmashauri baada ya kuona wananchi wakichangia
rejareja wanachangia fedha nyingi, iliona ni vema kukawa na mchango mmoja kwa
mwaka wa shilingi elfu 50” alifafanua Mtaka.
Awali akitoa ufafanuzi
kuhusu mchango huo Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amesema wilaya
hiyo ilifikia uamuzi wa kuwa na mchango mmoja kutokana na michango iliyokuwa
ikitolewa rejareja kutokuwa na matokeo yaliyokusudiwa, ikiwa ni pamoja na
miradi iliyokusudiwa kujengwa na fedha za michango hiyo hususani miundombinu
yal elimu na Afya kutokamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Erasto
Mbigili Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbalagane amesema anaunga mkono wazo la kuwa na mchango mmoja
kwa mwaka ambao utawarahisishia Wenyeviti wa Vijiji na vitongoji na kuwaondolea
kero ya kwenda kila mara kuwasumbua wananchi kuomba michango.
Naye John Dalawida Mwenyekiti
Kitongoji cha Matale amesema anaunga mkono wazo hilo ambalo limeanzia kwa
madiwani ambao ni wawakilishi wao na anaamini litasaidia ukamilishaji wa maboma
ya vyumba vya madarasa na zahanati waliyoanza kujenga ili kuboresha miundombinu
ya sekta ya elimu na afya wilayani Maswa.
Jeremia Shigala Diwani
wa kata ya Zanzui amesema Baraza la madiwani lilizimia kuja na mchango huo
baada ya wataalam wa Halmashauri kuonesha mchanganuo kuwa wananchi wilayani humo
wamekuwa wakichangia wastani wa shilingi elfu 70 kwa mwaka, hivyo alilipokea na kuahidi kwenda
kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa
mchango huo wa mara moja.
Katika Mkutano huo
viongozi wa Chama na Serikali walitoa michango yao ya fedha taslimu, ahadi na
vifaa vya ujenzi ili kuuunga mkono wazo la ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya
katika wilaya ya Maswa, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aliahidi kutoa shilingi
1,000,000/=, Mkuu wa wilaya hiyo aliahidi kutoa shilingi 500,000/= Mkurugenzi
wa Halmashauri aliahidi kutoa shilingi 500,000/= na Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM (NEC) akaahidi kutoa jumla ya mabati 500 kama mchango wake.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na Viongozi
wa Vitongoji, Vijiji, Kata, Wilaya na Mkoani Simiyu katika Mkutano uliofanyika
katika Uwanja wa Nguzo Nane Mjini Maswa.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakifuatilia mkutano
baina ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi
wa vitongoji ,vijiji na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa
ni kujadili azimio lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya
Maswa la Uchangiaji shughuli za maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick
Sagamiko (kulia) akifafanua jambo katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka na viongozi wa vitongoji ,vijiji
na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa ni
kujadili azimio lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa
la Uchangiaji shughuli za maendeleo.
Diwani wa kata ya Zanzui Mhe. Jeremia Shigala akichangia hoja katika kikao
cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wa vitongoji ,vijiji
na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa ni kujadili azimio
lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa la Uchangiaji
shughuli za maendeleo.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakifurahia jambo katika Mkutano wa viongozi
wa vitongoji ,vijiji na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa
ni kujadili azimio lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya
Maswa la Uchangiaji shughuli za maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa , Mhe. Dkt. Shekalaghe akipokea mchango kwa Katibu
wa CCM Mkoa, Bw. Donald Magesa mara baada ya kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wa vitongoji ,vijiji
na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa ni kujadili azimio
lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa la Uchangiaji
shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mhe. Enock Yakobo akifafanua jambo katika kikao cha
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wa vitongoji ,vijiji
na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa ni
kujadili azimio lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa
la Uchangiaji shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Mhandisi. Paul Jidayi akifafanua jambo
katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wa vitongoji
,vijiji na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa
ni kujadili azimio lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya
Maswa la Uchangiaji shughuli za maendeleo.
Diwani wa Viti Maalum CCM , Mhe. Leticia Lolela akichangia hoja katika kikao
cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wa vitongoji ,vijiji
na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa ni kujadili azimio
lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa la Uchangiaji
shughuli za maendeleo.
Kutoka kulia mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mkuu wa
Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC)
Mhe. Gungu Silanga wakiteta jambo wakati wa kikao maalum cha kujadili azimio
lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa la Uchangiaji
shughuli za maendeleo katika Uwanja wa Nguzo Nane Mjini Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na na viongozi wa vitongoji
,vijiji na wadau mbalimbali wa maendeleo ,wakiwemo
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa na wananchi, lengo likiwa
ni kujadili azimio lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya
Maswa la Uchangiaji shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo na Katibu Mkuu wa CCM
mkoa, Bw. Donald Magesa wakiteta jambo wakati wa kikao maalum cha kujadili azimio
lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa la Uchangiaji
shughuli za maendeleo katika Uwanja wa Nguzo Nane Mjini Maswa.
Kutoka kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mkuu wa
Mkoa, Mhe.Anthony Mtaka na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) Mhe. Gungu Silanga wakiteta jambo wakati wa kikao maalum cha kujadili azimio
lililopitishwa na Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Maswa la Uchangiaji
shughuli za maendeleo katika Uwanja wa Nguzo Nane Mjini Maswa.
0 comments:
Post a Comment