Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof.
Dkt. Ratlan Pardede amesema moja ya malengo makuu ya ziara yake mkoani Simiyu
ni kwenda kuona mkoa huo unavyozalisha pamba na kuona namna ya kuongeza
ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania(Simiyu) katika biashara ya zao la
pamba.
Balozi Pardede amesema hayo wakati wa
kikao maalum kati yake na viongozi wa Serikali na baadhi ya wafanyabiashara wa
Mkoa huo Mjini Bariadi.
"Nimekuja kuona Simiyu kama mkoa
unaoongoza kwa kilimo cha pamba Tanzania, nijue namna mnavyolima,
mnavyoichakata, lengo hasa likiwa ni kuongeza kiwango cha pamba inayonunuliwa
na nchi ya Indonesia kutoka Tanzania, kwa kuwa nchi yetu inahitaji pamba kwa
ajili ya viwanda vya nguo "
Amesema Indonesia inahitaji zaidi ya
asilimia 90 ya pamba kama malighafi katika viwanda vilivyopo nchini humo
ambayo huagizwa nje ya nchi hiyo, hivyo kutokana na Mkoa wa Simiyu kuwa
kiongozi katika uzalishaji wa pamba nchini mkoa huo unaweza kuuza pamba yake nchini
Indonesia.
Ameongeza kuwa ili pamba ya Tanzania
iweze kununuliwa nchini Indonesia inapaswa kuzalishwa katika ubora unaotakiwa
na kuuzwa kwa bei isiyokuwa ya juu zaidi ikilinganishwa na pamba kutoka katika mataifa mengine
yanayozalisha pamba.
Mhe. Balozi ameyataja maeneo mengine
ambayo Indonesia itaongeza ushirikiano na Tanzania hususani mkoa wa Simiyu kuwa
ni mifugo, miundombinu na umeme hasa unaozalishwa kwa kutumia
maji(Hydroelectric Power).
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
amemuomba Balozi Pardede kuwakaribisha wawekezaji kutoka Indonesia kuja kuwekeza
mkoani humo katika ujenzi wa viwanda vya nguo(textile industries), huku
akiwahakikishia upatikanaji wa ardhi bila malipo yoyote.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Ndg. Jumanne Sagini amemuomba Balozi wa Indonesia hapa nchini na Serikali ya
Indonesia kuona uwezekano wa kuanzisha mafunzo kwa watumishi wa Simiyu,
kuwezesha wafanyabiashara wa Indonesia kushirikiana na wenzao wa Simiyu katika
masuala mbalimbali ya kibiashara.
Aidha, Sagini ameomba
ushirikiano kati ya Tanzania na Indonesia kuendelea kuimarishwa
katika ngazi ya Taifa na kwa Mkoa ambapo ameomba Balozi huyo kuona namna
ya kusaidia Mkoa wa Simiyu kuwa na Mkoa
au Mji pacha nchini Indonesia.
Mhe. Balozi Prof. Dkt. Ratlan Pardede
yuko katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu ambayo inatarajiwa kuhitimishwa Mei
17 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kulia), Katibu Tawala wa Mkoa, Jumanne Sagini(kushoto)
wakiteta jambo na Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede
mara baada ya kikao kati ya balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika
mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Balozi wa Indonesia
hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede akizungumza na viongozi wa Mkoa wa
Simiyu katika kikao maalum mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya
kikazi ya siku nne.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa
Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede mara baada ya kikao
kati ya balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi siku
ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Jumanne Sagini akiwasilisha
taarifa ya Mkoa kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede katika
kikao kati ya balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi siku
ya kwanza ya ziara yake mkoani humo
.
Mwakilishi
wa Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Emmanuel Luangisa
akizungumza katika kati ya Balozi wa
Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika
mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi wa
Serikali, Viongozi wa dini na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Balozi
wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (hayupo pichani) katika
kikao na Balozi huyo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake
mkoani humo.
Baadhi
ya viongozi wa Serikali, Viongozi wa dini na wataalam wa Mkoa wa Simiyu
wakimsikiliza Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (hayupo
pichani) katika kikao na Balozi huyo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya
kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Baadhi ya viongozi wa
Serikali, Viongozi wa dini na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Balozi
wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (hayupo pichani) katika
kikao na Balozi huyo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake
mkoani humo.
Balozi wa Indonesia
hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kikao kati ya Balozi huyo na
Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake
mkoani humo.
Balozi wa Indonesia
hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi na Wataalam wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kikao kati ya Balozi
huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya
ziara yake mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment