Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba ameutaka uongozi wa Kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega kuimarisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato (kudhibiti upotevu wa mapato) ili kuongeza mapato yatakayosaidia kununua dawa na kuboresha miundombinu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Dkt.
Kulemba ameyasema hayo Septemba 10, 2020 katika nyakati tofauti wakati wa ziara
ya usimamizi shirikishi iliyofanyika katika kituo hicho, ambapo moja ya malengo
ya ziara ilikuwa ni kukagua mifumo ya ukusanyaji wa mapato na hali ya utoaji wa
huduma za afya kwa ujumla wake.
“Imarisheni
mfumo wa ukusanayaji mapato nataka wakati ujao mapato yaongezeke mara mbili ya
sasa, mkumbuke kuwa kwa kadri tunavyodhibiti upotevu wa mapato ndiyo
tutakavyoboresha utoaji wa huduma; tutaweza kununua dawa na kufanya maendeleo
ya kituo chetu hali itakayochangia kuongeza ufanisi katika huduma zinazotolewa
kwa wananchi,” alisema Kulemba.
Ameongeza
kuwa Uongozi wa Kituo hicho unapaswa kuhakikisha kuwa mfumo wa GoT-HOMIS unaohusika
na usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya unafungwa na
kufanya kazi kituoni hapo, ili kudhibiti aina yoyote ya upotevu wa mapato kwa
kuwa taarifa ya kila huduma na mapato zitaingizwa katika mfumo huo.
Naye
Afisa Afya kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema pamoja na kuimarisha
mfumo wa mapato uongozi huo uboreshe mazingira kwa kusafisha mara kwa mara
maeneo ya kituo hicho pamoja na kupanda bustani za maua.
Akizungumza
kwa niaba ya watumishi wa idara ya afya wilaya ya Busega, Kaimu Mganga Mkuu wa
wilaya amesema watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na mganga mkuu wa mkoa
ili kutimiza azma ya serikali ya kutoa huduma zinazotakiwa kwa wananchi na kwa
wakati.
Baadhi
ya wananchi waliopata huduma za matibabu katika kituo cha afya Lukungu wameupongeza
uongozi wa kituo kwa namna ulivyoboresha utoaji wa huduma na kuomba hali ya
upatikanaji wa dawa iimarishwe zaidi na miundombinu ya kutoa huduma ikiwemo
huduma za upasuaji, wodi za kulaza wagonjwa ziongezwe ili wapate huduma zote kituoni hapo.
“
Kwa upande wa huduma mimi nimehudumiwa vizuri, nimepokelewa vizuri na wauguzi
wamenisikiliza baada ya kunisikiliza nimeenda kwenye vipimo na nilivyorudi kwa
daktari amenieleza tatizo langu akaniandikia dawa, nashukuru dawa zote nilizoandikiwa nimepewa,”
Mandege William Manyama, mkazi wa Kijiji cha Lukungu.
“Huduma zote nilizokuwa nazihitahitaji nimezipata na
nimehudumiwa ndani ya muda mfupi, ombi langu serikali ione namna ya kuongeza
huduma hasa za kulaza wagonjwa ili tuipate hapa hapa badala ya kupelekwa kwenye
vituo vingine na hospitali,” alisema Daud Moshi mkazi wa Kijiji cha Lukungu.
MWISHO
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(katikati) akitoa maelekezo kwa baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo
cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi
shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(kulia) akifanya ukaguzi katika wodi ya
wazazi katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara
ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba akitoa maelekezo kwa baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo
cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi
shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Mfamasia wa Halmashauri
ya Wilaya ya Busega akichangia jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa
Huduma za Afya ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa
Kituo cha Afya Lukungu wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo
hicho Septemba 10, 2020.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(katikati) akitoa maelekezo kwa baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo
cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi
shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Baadhi ya wananchi
wakisubiri huduma katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.
Baadhi ya watoa huduma
za afya katika kituo cha afya cha Lukungu wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo kwa
watoa huduma hao wakati akiwa katika
ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Afisa Afya katika Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akichangia
jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa wa
Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa Kituo cha Afya Lukungu wakati
wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Afisa Afya katika Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akichangia
jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa wa
Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa Kituo cha Afya Lukungu wakati
wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Moja ya majengo ya
kutolea huduma katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.
Wodi ya wazazi katika
kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.
Baadhi ya Maafisa wa
Idara ya Afya mkoa wa Simiyu na Wilayani ya Busega na watoa huduma za afya
katika kituo cha afya cha Lukungu wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo kwa watoa huduma hao wakati akiwa katika ziara ya
usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Busega wakifuatilia
kikao cha Idara ya Afya mkoa wa Simiyu na Wilayani ya Busega na watoa huduma za
afya katika kituo cha afya cha Lukungu kilichofanyika wakati wa ziara ya
usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(kulia) akitoa maelekezo kwa baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo
cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi
shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.
0 comments:
Post a Comment