Sunday, September 13, 2020

WADAU WA KILIMO SIMIYU WAJADILI MWONGOZO WA KILIMO CHA MKONGE

 Bodi ya Mkonge Tanzania imekutana na uongozi wa mkoa wa Simiyu na baadhi ya watendaji na wataalam wa kilimo kwa lengo la kujadili mwongozo wa kilimo cha mkonge mkoani hapa lengo likiwa ni kuhakikisha mkulima anazalisha mkonge bora na wenye thamani katika soko.

Akikabidhi muongozo huo kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadaye akawakabidhi maafisa Kilimo, Mratibu mkuu wa utafiti na masoko, Bw Hassan Kibarua amesema ni vema wataalam wa kilimo wakatoa elimu kwa wakulima wa mkonge juu ya kuzingatia ubora kuanzia uzalishaji ili usipungue thamani.

"Mkonge unatakiwa kuchakatwa si zaidi ya masaa 48 tangu kukatwa lakini kuna wakati mkulima anachakata mkonge uliokatwa zaidi ya siku tano, unakuwa umepungua ubora na unapofika sokoni unakuwa haupo kwenye daraja la ubora wa 3L ambalo lina bei ya juu, " alisema Kibarua.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!