Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umemtunuku cheti cha shukrani aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ikiwa ni kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu katika Mkoa wa Simiyu wakati wa uongozi wake, kabla ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM kuwa Mgombe wa Ubunge katika Jimbo la Butiama mkoani Mara.
Akimkabidhi
cheti hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema uongozi umetoa cheti hicho kama alama katika kushukuru
na kuthamini mchango wa Ndugu
Sagini katika maendeleo ya sekta ya
elimu na mkoa wa Simiyu kwa ujumla.
“Tunakutakia
kila la heri na tunaahidi kuwa tutaendelea kuishi ndoto na dhamira ulizoshiriki
kuzitengeneza ukiwa na Mkuu wetu wa mkoa Mhe. Anthony Mtaka ili kuhakikisha
elimu inasonga mbele na mkoa wa Simiyu unakuwa nambari moja katika kila eneo,”
alisema Bi. Mmbaga.
Akipokea
cheti hicho aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
amewashukuru viongozi wa mkoa kwa kutambua mchango wake huku akibainisha kuwa
wakati wa uongozi wake kama msimamizi mkuu wa utekelezaji wa yale waliyokuwa
wakikubaliana alipata ushirikiano kutoka kwa viongozi na watendaji kuanzia
ngazi ya mkoa hadi wilaya.
“
Ninawashukuru sana viongozi wa mkoa mkiongozwa na kiongozi Mkuu Mhe. Mkuu wa
Mkoa kwa kutambua mchango wangu, nimefarijika kuona mimi nilipotoka Simiyu
kwenda kwenye shughuli za kisiasa, yale tuliyopanga kama mkoa yametimia maana
mwaka juzi tulishika nafasi ya kumi, mwaka jana tukabaki hapo lakini mwaka huu
nasikia mmeshika nafasi ya tatu hongereni sana, natamani lengo la kushika
nafasi ya kwanza litimie,” alisema Sagini.
Aidha,
Sagini ameomba Mkoa wa Simiyu ukubali kuwa marafiki wa Wilaya ya Butiama na Mkoa
wa Mara kwa ujumla, ili kuendeleza ushirikiano
kati ya wilaya na mikoa jirani; huku akitoa wito kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu
kukubali na kutoa ushirikiano pale watu wa Butiama na Mara watakapohitaji kujifunza
na kupata uzoefu kutoka kwao.
Jumanne Sagini aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu mwishoni
mwa mwezi Aprili mwaka 2016 na aliachia
nafasi hiyo Julai 03 mwaka huu baada ya kuanza kushiriki mchakato wa kugombea
ubunge katika Jimbo la Butiama ambapo amepewa
ridhaa na Chama Cha Mapinduzi kupeperusha bendera ya Chama hicho katika
Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
MWISHO
Aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (kulia) akipokea cheti maalum kutoka Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga ambacho kimetolewa Agosti 24,
2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta
ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa na
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.
Aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini akionesha cheti maalum kilichotolewa Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo
la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa
uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.
Aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini na mkewe Bi. Mariam Sagini wakiwa na cheti
maalum kilichotolewa Agosti 24, 2020 kwa ndugu Sagini na uongozi wa mkoa wa
Simiyu kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani
Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.
Aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (kulia) akipokea cheti maalum kutoka Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga ambacho kimetolewa Agosti 24,
2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta
ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa an
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia
CCM.
Aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini (aliyeshika cheti) akifurahia jambo mara
baada ya kupokea cheti maalum kutoka
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ambacho kimetolewa Agosti 24, 2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo
la kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya elimu mkoani Simiyu wakati wa
uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa
na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea wa Ubunge Jimbo la Butiama
kupitia CCM.
Aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini
akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokea cheti maalum kutoka Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga ambacho kimetolewa Agosti 24,
2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta
ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea
wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.
Aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini
akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokea cheti maalum kutoka Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga ambacho kimetolewa Agosti 24,
2020 na uongozi wa mkoa kwa lengo la kutambua mchango wake katika kukuza sekta
ya elimu mkoani Simiyu wakati wa uongozi wake, ambapo kwa sasa ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Mgombea
wa Ubunge Jimbo la Butiama kupitia CCM.
0 comments:
Post a Comment