Aliyekuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (aliyevaa suti ya bluu nyeusi)
ametembelea mabanda leo Agosti 03, 2020 katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Nyakabindi Bariadi,
yanayofanyika Kitaifa mwaka 2020 katika Kanda ya Ziwa Mashariki inayoundwa na
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga.
Sagini ametoa wito kwa wananchi kutembelea maonesho hayo ambayo amekiri kuwa yamefana kwa kiasi kikubwa ili waweze kujifunza masuala mbalimbali yahusuyo uzalishaji kwenye tija katika kilimo, mifugo na uvuvi.
Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini
akikabidhiwa boksi la chaki na mmoja wa
wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza chaki cha wilayani Maswa wakati alipotembelea
mabanda ya maonesho Agosti 03, 2020
katika Maonesho ya Nanenane Kitifa yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa
Masharikinviwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
HABARI KATIKA PICHA, ALIYEKUWA KATIBU TAWALA WA MKOA WA SIMIYU AKITEMBELEA MABANDA YA MKOA WA SIMIYU AGOSTI 03/08/2020
0 comments:
Post a Comment