Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wakulima kuchangamkia fursa ya kilimo cha mbogamboga ili waweze kujipatia kipato kupitia kilimo hicho cha bustani ambacho uandaaji wake wa mashamba ni wa nafuu lakini kimekuwa na faida kubwa.
Mhe. Waziri Mkuu ameyasema hayo Agosti 08, 2020 wakati akihitimisha
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yaliyofanyika kanda ya ziwa Mashariki
katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Aidha, Mhe. Waziri Mkuu amewahimiza wakulima kuchangamkia mikopo
inayotolewa na taasisi za kifedha ili waweze kupata mitaji itakayowasaida
kuendesha shughuli za kilimo ikiwemo kilimo cha bustani, ufugaji na uvuvi.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga amesema katika upande wa
chanjo na uhimilishaji serikali imeweka bei elekezi ya uhimilishaji ambapo kwa
sasa Ng’ombe mmoja atagharimu kiasi cha 10,000 badala ya sh.25,000 ambapo
katika maonesho ya nane nane ambapo msimu huu Wizara hiyo imeweza kuhimilisha
Ng’ombe zaidi ya 100 bure .
Naye Waziri wa Kilimo Japheti Hasunga amesema kwa sasa Wizara ya kilimo
imejikita kuhamaisha wakulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuhamia
katika kilimo cha Biashara na tayari Wizara hiyo imeanzisha huduma za ugani
ambazo zitatolewa huku Jengo la Wizara ya kilimo lililopo ndani ya Viwanja vya
Nyakabindi likipangwa kutumika kutoa mafunzo mwaka mzima,ambapo amaewaomba
viongozi wa Mikoa husika kuhakikisha wanaleta wakulima ili wapate mafunzo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu
umekuwa ukifanya vizuri katika kilimo cha zao la pamba hivyo akaomba serikali
kuona namna ya kusaidia katika uongezaji wa thamani wa zao hilo, ambapo
amekizungumzia kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba kinachotakiwa kujengwa
wilayani Bariadi, kwamba kitakapojengwa kitaisaidia nchi kuokoa takribani shilingi bilioni 100 zinazotumika kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment