Katika kuwawezesha wanawake na vijana katika sekta ya biashara serikali imesema imeandaa mfuko maalum utakaowasaidia wajasiriamali wanaopata mafunzo katika taasisi mbalimbali kama SIDO na VETA kwa kuwapa mikopo ya mtaji
Hayo yamebainishwa na waziri wa viwanda na biashara, Mhe. Innocent Bashungwa kwenye kongamano la biashara na kilimo biashara kwa wanawake na vijana mkoani Simiyu lililofanyika Agosti 05, 2020 katika Viwanja vya nanenane Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Bashungwa amesema serikali inafanya kila jitihada kuwawezesha wanawake na vijana kwani wanatambua kuwa nguvu kazi kubwa ya taifa inatokana na makundi hayo.
Katika hatua nyingine Bashungwa amewaagiza katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara na kushirikiana na wa wizara ya kilimo kuhakikisha kliniki ya biashara inayotembea kufanya kazi kwa ufanisi.
Kwa upande wake Dkt Never Zehaya kutokana chuo Kikuu cha Nelson
Mandela aliyegundua viuatilifu vya wadudu wahalibifu wanaoshambulia mazao
mbalimbali ya wakulima ameiomba serikali kupunguza uagizaji wa dawa hizo nje ya
nchi na badala yake kununua zinazotengenezwa nchino lengo likiwa ni kuwapa
nguvu na uwezo wa uzalishaji mkubwa.
MWISHO
TAZAMA PICHA MBALIMBALI AMBAZO WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA, MHE. INNOCENT BASHUNGWA AAKIWA AMEAMBATANA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKATI ALIPOWASILI KATIKA VIWANJA VYA NYAKABINDI NA WAKATI AKITEMBELEA MABANDA YA MAONESHO YA NANENANE YA TAASISI MBALIMBALI
0 comments:
Post a Comment