Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kimeahidi kuwa kiko tayari kuanzisha kituo cha kupima makohozi kwa kutumia panya waliofundishwa kubaini vijidudu vya Ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao wanaweza kupima sampuli nyingi kwa wakati mmoja ikilinganishwa na vipimo vya maabara.
Hayo yamebainishwa jana
na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mmbaga kikao kazi cha tathmini ya
utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kifua kikuu ngazi ya jamii uliokuwa
ukitekelezwa na mkoa wa Simiyu kwa
kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Management and Development for
Health (MDH), kwa miaka mitatu kuanzia Januari 2018 na unatarajiwa
kuhitimishwa Desemba 2020, ambacho kilifanyika jana Mjini Bariadi.
“Tumeona ni muhimu
tukaangalia tunavyoweza kutumia teknolojia nyingine kufanya upimaji wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu, kwa mfano
tumepata fursa ya kushirikiana na wenzetu wa SUA kipindi cha nanenane mwaka huu wamesema wako tayari kutusaidia kuanzisha
kituo cha upimaji wa makohozi kwa kutumia panya waliofundishwa,” alisema
Mmbaga.
Aidha, Mmbaga amesema mkoa
wa Simiyu umeonekana kufanya vizuri katika kuwafikia wagonjwa wa Kifua kikuu
ikilinganishwa na mikoa mingine saba ambayo yote inatekeleza mradi wa kudhibiti
kifua kikuu ngazi ya jamii chini ya shirika lisilo la Kiserikali la Management and Development for
Health (MDH) ambapo umevuka lengo na kuwafikia wananchi kwa asilimia 102.
Pamoja na mafanikio
hayo Mmbaga ameelekeza wataalam wafanye tathmini ya malengo yao na waweke
malengo mapya yatakayokusudia kuwafikia wananchi wengi wenye uhitaji, ili
kupata jamii yenye afya itakayotekeleza kwa vitendo azma na dira ya mkoa ya
kuwa mkoa wenye uchumi shindani kwa kutumia rasilimali na fursa zilizopo.
Kwa upande wake Mratibu
wa Huduma za kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma, Dkt. Emmanuel John amesema kwa
mwaka 2019 Mkoa wa Simiyu ulikuwa na lengo la kuwafikia wagonjwa wa Kifua Kikuu
1631 ambapo mpaka kufikia mwezi Desemba 2019 wagonjwa takribani 1673 walikuwa wamefikiwa sawa na asilimia 102
ya lengo.
Dkt. John ameongeza
kuwa katika wagonjwa waliokuwa wameanzishiwa matibabu kwa mwaka 2018/2019 asilimia 72 waliweza kupona kabisa, huku
akibainisha kuwa katika asilimia 28 baadhi yao walifariki, baadhi walipotea katika
mifumo ya matibabu (watoro); huku akiweka bayana kuwa kwa mwaka 2020, lengo la Mkoa ni kuwafikia wagonjwa 1779.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa
Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba amesema kuwa wataalam wa afya ngazi ya mkoa na
halmashauri watahakikisha wanafanya marejeo ya malengo yao yaweze kuakisi hali
halisi ya mahitaji ya jamii ili wananchi wengi waweze kufikiwa na huduma za
upimaji na matibabu ya Kifua Kikuu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Management and Development for
Health (MDH), Bw. Eliamin Busara amesema katika awamu ijayo shirika hilo
linatarajia kujikita zaidi katika mpango wa Kifua Kikuu na uboreshaji wa huduma
za mama na mtoto hususani katika kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Wakati
huo huo Busara ametoa wito kwa Serikali kupitia halmashauri kuwa na mipango ya
namna ya kuendeleza huduma zilizokuwa zikitolewa kwa wananchi kupitia mradi huo
ili huduma za afya zisitetereke hususani katika upimaji na matibabu ya Kifua
Kikuu.
MWISHO
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba
akichangia hoja katika kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa
kudhibiti kifua kikuu ngazi ya jamii uliokuwa ukitekelezwa na mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Management and Development for
Health (MDH) kwa miaka mitatu kuanzia Januari 2018 na unatarajiwa
kuhitimishwa Desemba 2020, ambacho kilifanyika jana Mjini Bariadi.
:- Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kifua kikuu ngazi ya jamii uliokuwa ukitekelezwa na mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Management and Development for Health (MDH) kwa miaka mitatu kuanzia Januari 2018 na unatarajiwa kuhitimishwa Desemba 2020, mara baaada ya kufungua kikao hicho ambacho kilifanyika jana Mjini Bariadi.
Baadhi ya washiriki wa
kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kifua kikuu ngazi
ya jamii uliokuwa ukitekelezwa na mkoa
wa Simiyu kwa kushirikiana na shirika
lisilo la Kiserikali la Management and
Development for Health (MDH) kwa miaka
mitatu kuanzia Januari 2018 na
unatarajiwa kuhitimishwa Desemba 2020, wakifuatilia
mada zilikuwa zikiwasilishwa katika kikao hicho ambacho kilifanyika jana Mjini
Bariadi.
Baadhi ya washiriki wa
kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kifua kikuu ngazi
ya jamii uliokuwa ukitekelezwa na mkoa
wa Simiyu kwa kushirikiana na shirika
lisilo la Kiserikali la Management and
Development for Health (MDH) kwa miaka
mitatu kuanzia Januari 2018 na
unatarajiwa kuhitimishwa Desemba 2020, wakifuatilia
mada zilikuwa zikiwasilishwa katika kikao hicho ambacho kilifanyika jana Mjini
Bariadi.
Baadhi ya washiriki wa
kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kifua kikuu ngazi
ya jamii uliokuwa ukitekelezwa na mkoa
wa Simiyu kwa kushirikiana na shirika
lisilo la Kiserikali la Management and
Development for Health (MDH) kwa miaka
mitatu kuanzia Januari 2018 na
unatarajiwa kuhitimishwa Desemba 2020,
wakifuatilia mada zilikuwa zikiwasilishwa katika kikao hicho ambacho
kilifanyika jana Mjini Bariadi.
Baadhi ya washiriki wa
kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti kifua kikuu ngazi
ya jamii uliokuwa ukitekelezwa na mkoa
wa Simiyu kwa kushirikiana na shirika
lisilo la Kiserikali la Management and
Development for Health (MDH) kwa miaka
mitatu kuanzia Januari 2018 na
unatarajiwa kuhitimishwa Desemba 2020,
wakifuatilia mada zilikuwa zikiwasilishwa katika kikao hicho ambacho
kilifanyika jana Mjini Bariadi.
Mmoja wa wawasilishaji
akiwasilisha taarifa katika kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa
kudhibiti kifua kikuu ngazi ya jamii uliokuwa ukitekelezwa na mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Management and Development for
Health (MDH) kwa miaka mitatu kuanzia Januari 2018 na unatarajiwa
kuhitimishwa Desemba 2020, ambacho kilifanyika jana Mjini Bariadi.
Moja ya panya wa Chuo
Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) wanaotumika kupima makohozi kubaini vijidudu vya
Kifua Kikuu ambao tayari wamepewa mafunzo
0 comments:
Post a Comment