Wanafunzi wa Darasa la Saba na Kidato cha nne Mkoani Simiyu wameahidi kufuata nyayo za kidato cha Sita kuendelea kufanya vizuri katika mitihani yao ya Kitaifa na kubaki katika nafasi tatu bora Kitaifa kama walivyofanya Kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa umekuwa wa tatu kati ya mikoa 29.
Hayo
yamesemwa na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Somanda (B )
na kidato cha nne kutoka Shule ya sekondari Simiyu (Bariadi) waliowawakilisha
wenzao katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi
waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita iliyofanyika24 Agosti 2020 Mjini
Bariadi
“Tunawapongeza dada na
kaka zetu kidato cha sita kwa kufanya
vizuri kwenye mtihani wao wa taifa tunaahidi kufanya vizuri kama wao;Shule yetu
ya msingi Somanda B ina mkakati wa kuingia katika shule kumi bora kitaifa na
kutoa wanafunzi wanne katika wanafunzi kumi bora Kitaifa,tunaahidi hatutawaangusha,”alisema
Ezra Paulo mwanafunzi wa darasa la saba Somanda.
“ Matokeo ya Kidato cha
Sita yametuhamasisha kujipanga zaidi kwa mwaka 2020, kupitia fursa mbalimbali
ambazo tunapewa na viongozi wetu zikiwemo kambi za kitaaluma tunapata fursa ya
kujisomea zaidi kuliko tukikaa majumbani, tunaahidi kufanya vizuri zaidi ya
dada na kaka zetu walivyofanya ikizingatiwa kuwa shule yetu inabeba jina la
mkoa,” Sarah Ndamo kutoka Simiyu Sekondari.
Kwa upande wake mwanafunzi
Benard S. Benard kutoka shule ya sekondari Binza wilayani Maswa ambaye amepata
daraja la kwanza pointi nne, amewaasa wanafunzi wenzake kuongeza bidii katika
masomo kushirikiana na kuutumia vizuri muda wanaokuwa shuleni ili waweze
kufikia malengo yao.
Naye Mkuu wa Shule ya
Sekondari Bariadi, Mwl. Ally Simba amesema siri kubwa ya wanafunzi wa shule
hiyo kufanya vizuri zaidi na kuifanya kuwa ya kwanza kimkoa na ya 24 Kitaifa ni
kufanya mitihani ya mara kwa mara huku akibainisha kuwa wamejipanga kuwa katika
shule kumi bora Kitaifa na kuibadilisha shule hiyo ili iwe miongoni mwa shule
maalum nchini.
Akizungumza kwa niaba
ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amesema
siri kubwa ya kufanya vizuri ni mikakati iliyowekwa na mkoa pamoja na utekelezaji
wake ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujiamini huku
akisisitiza kila mdau atimize wajibu wake ili mkoa uendelee kufanya vizuri.
Afisa Elimu wa Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema mkoa umetimiza azma yake ya kutoka nafasi ya
10 mwaka 2019 na kuingia nafasi ya tatu
Kitaifa mwaka 2020 na kuongeza ufaulu kutoka GPA ya 3.0443 kufikia 2.894; huku akishauri kuwa ili Simiyu iendelee
kufanya vizuri zaidi ni vema ufundishaji
makini uimarishwe zaidi..
Jumla ya wanafunzi 955
walisajiliwa kufanya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2020 mkoani
Simiyu, kati yao wanafunzi watano hawakufanya mtihani na katika wanafunzi 950
waliofanya mtihani, wanafunzi 208 wamepata daraja la kwanza, 507 wamepata daraja la pili, 228 daraja la tatu, wanafunzi 06 wamepata daraja la nne na mmoja amepata daraja sifuri.
Pamoja na kutoa shilingi laki moja kwa kila alama A iliyopatikana kwenye somo lake mwalimu aliyefanya vizuri,wanafunzi wawili waliopata daraja la kwanza pointi nne wamepewa shilingi laki mbili kila mmoja; Mkoa pia umetambua mchango wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini katika kukuza sekta ya elimu kwa kumtunuku cheti.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi ya shilingi laki tano Mkuu wa
Shule ya sekondari Bariadi, Mwl. Ally Simba iliyotolewa kama pongezi kwa shule
hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 10 mkoani Simiyu na ambayo imeshika
nafasi ya 24 Kitaifa kati ya shule zaidi ya 500, katika hafla ya kuwapongeza
walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita ambapo
mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi.
Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Benard S Benard .kutoka Shule
ya Sekondari Binza wilayani Maswa aliyepata daraja la kwanza pointi nne, wakati
wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa
Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya
tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Mussa Abdallah kutoka
Shule ya Sekondari Bariadi wilayani Bariadi aliyepata daraja la kwanza pointi
nne, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri
katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika
nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi
katika idara ya elimu, walimu, wanafunzi na wadau wa elimu wakifuatilia matukio
mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri
katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu
umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Shekhe wa mkoa wa
Simiyu, Mahamoud Kalokola akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na
wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka
2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti
24, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu
na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka
2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti
24, 2020 Mjini Bariadi.
Mchungaji wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Somanda Bw. Timotheo Alfred
akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya
vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa
Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini
Bariadi.
Katibu wa CCM Mkoa wa
Simiyu, Bi. Haula Kachwamba akieleza
jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika
Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika
nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi
kutoka katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoa wa Simiyu wakifuatilia matukio
mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri
katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu
umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, mhe. Aswege Kaminyoge akieleza jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu
na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka
2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti
24, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akieleza
jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika
Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika
nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya
sekondari ya Simyu Mjini Bariadi, wakieleza malengo yao katika kufikia nafasi
ya kwanza kitaifa katika Mtihani wao wa Taifa, katika hafla ya kuwapongeza
walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha
Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa,
iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Mmoja wa walimu katika
shule ya sekondari ya wasichana Maswa akipokea zawadi kutoka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi.
Mhe. Festo Kiswaga katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya
vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa
Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini
Bariadi.
Baadhi ya walimu,
wanafunzi na wadau wa elimu wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya
kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa
kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu
Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi
katika idara ya elimu, walimu, wanafunzi na wadau wa elimu wakifuatilia matukio
mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri
katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu
umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi zawadi mmoja wa walimu kutoka shule ya
sekondari Bariadi , katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya
vizuri katika mtihani wa kidato cha sita ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi
ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha
Walimu Tanzania mkoa wa Simiyu, Mwl. Kulwa Dwese akieleza jambo katika hafla ya
kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa
kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu
Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju na
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakiteta jambo kabla ya kukabidhi
zawadi kwa walimu na wanafunzi, katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi
waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo
mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020
Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe. Benson Kilangi akieleza
jambo katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika
Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika
nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Makatibu
Tawala wa Wilaya mkoa wa Simiyu wakiteta jambo katika hafla ya kuwapongeza
walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha
Sita mwaka 2020 ambapo mkoa wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa,
iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa
shule za msingi wilayani Bariadi
wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi
waliofanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo mkoa
wa Simiyu umeshika nafasi ya tatu Kitaifa, iliyofanyika Agosti 24, 2020 Mjini
Bariadi.
0 comments:
Post a Comment