Wednesday, August 12, 2020

DKT GWAJIMA AAGIZA MIKOA YOTE NCHINI KUFANYA UKAGUZI WA VITUO VYA AFYA

" Mikoa yote fanyeni ukaguzi katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya kama mlivyofanya kwa vichache na mkagundua matatizo mengi kwenye usimamizi wa mfumo wa ugavi na ikaonekana bayana kwamba mkiongeza usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi mnaziba mianya ya watu fulani ambao wanadhani vituo hivyo ni shamba la bibi," 

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima.katika kikao kazi kilichowahusisha Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya, katika kikao kazi kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya. 

Aidha, Dkt. Gwajima amesema taarifa ya ukaguzi huo unapaswa kufanyika kila robo inapokamilika na taarifa iwasilishwe wiki mbili baadaye na kufafanua kuwa taarifa ya awali itapokelewa Oktoba 15 baada ya kukamilika kwa robo ya kwanza ya mwezi Juni-Septemba mwaka 2020/2021. 

Ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanywe na wataalam waliobobea kwenye masuala ya ukaguzi wakiwemo wakaguzi wa ndani na maafisa ugavi ambapo amesisitiza wataalam hao wawezeshwa kufika katika vituo hivyo na kupata nafasi ya kufanya ukaguzi katika mifumo mbalimbali ya uedneshaji wa vituo hivyo ili waweze kubaini baadhi ya matatizo ya kimifumo pia. 

Katika hatua nyingine Dkt, Gwajima amewataka wakurugenzi wa Halmashauri  kufungua maduka ya dawa jamii katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuongeza hali ya upatikanani wa dawa na mapato. 

Wakati huo huo Dkt. Gwajima ameupongeza mkoa wa Simiyu kwa kufanya vizuri katika eneo la ukaguzi na ufuatiliaji jambo ambalo limechangia kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na mapato ya vituo kuongeza hadi mara tano ya mapato ya awali. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa Wafamasia mkoani hapa kujitathmini katika utendaji kazi wao ili kuhakikisha kuwa wanadhibiti matumizi ya dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya. 

Aidha, Mtaka amesema ni vema viongozi wote katika ngazi ya wilaya na mkoa kuhakikisha anatimiza wajibu wake na katika utoaji wa huduma za afya ndani ya mkoa  ikiwa ni pamoja na kufuatilia taarifa za ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amesema katika kipindi cha Januari hadi julai 2020 mkoa huu umefanya ukaguzi katika vituo 42 vya huduma

Kati ya vituo 119 kubaini kasoro mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujazaji hafifu wa leja, thamani ya dawa kutoingizwa katika vitabu na kasi ya matukio kukosekana kwa dawa. 

Dkt. Dugange  amemeongeza kuwa baada ya ukaguzi huo kumekuwa na udhibiti wa upotevu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, kuongezeka kwa wateja vituoni  na mapato yameonezeka; ambapo mapato ya mwezi Januari kwa vituo 22 yalikuwa shilingingi 37, 349, 762 kabla ya ukaguzi na kufikia 78,778,964 mwezi Julai baada ya ukaguzi. 

Naye Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Mika Mollel amesema ili wakaguzi wa ndani waweze kufanya kazi yao vizuri ni vema wakapewa nafasi ya kuingia katika mifumo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mifumo ya dawa na ukusanyaji wa mapato huku akiomba waaajiri kuwawezesha wakaguzi hao kutekeleza majukumu yao. 

Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Enock Yakobo ametoa rai kwa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa zinakuwa na rekodi sahihi ya dawa na jambo la hali ya upatikanaji wa dawa lijadiliwe katika vikao vya halmashauri na watakaohusika katika upotevu wa dawa na mapato wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya, katika kikao kazi kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akifunga  kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Festo Dugange akionesha cheti alichokabidhiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kama pongezi kwa kuwa mkoa wa pili  katika usimamizi wa huduma za afya, katika  kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kikao kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu (mbele) na baadhi ya wajumbe wakifuatilia kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkurugenzi wa Tiba na Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Kaminyoge akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Mika Mollel akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera  akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi  akichangia hoja katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Baadhi ya viongozi wakiwa katika kikao kazi cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao kazi  cha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, Viongozi mbalimbali, wataalam  wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya,  kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!