Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mwita Waitara amezitaka Halmashauri zote nchini
zinazoshiriki Maonesho ya Nanenane kuona namna ambayo watalaam wake watakavyoipeleka
elimu waliyoipata katika maonesho hayo kwa wakulima na itakavyowasaidia
wakulima, wafugaji na wavuvi hususani walioko vijijini kuleta tija katika
uzalishaji.
Waiatara ameyasema hayo mara baada ya kutembelea baadhi ya mabanda ya maonesho na sehemu ya vipando vya mazao katika Viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambako maonesho haya yanafanyika kitaifa mwaka 2020.
Amesema halmashauri
zinapaswa kuwatumia wataalam wa kilimo, mifugo na uvuvi kuhakikisha kuwa
wanatumia elimu waliyoapata katika maonesho hayokuwafikia wakulima, wafugaji na
wavuvi.
"Katika maonesho haya siku zote huwa kunakuwa na vitu vizuri tunavyoviona changamoto ipo kwenye kuyapeleka haya yaliyopo kwenye viwanja kwenda kule kwa wananchi," alisema Waitara.
Aidha, Mhe. Waitara ameupongeza mkoa wa Simiyu kwa kuwa kinara wa viwanda vidogo vidogo pamoja na viwanda vya kimkakati kikiwemo kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio wilayani Maswa.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Kiilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema vijana wengi wanakabiliwa na
changamoto ya upatikanaji wa ardhi huku akitoa rai kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI
kusisitiza Halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ameahidi kuwa mkoa huo uko tayari kutoa maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana huku akisisitiza kuwa Simiyu itakuwa mkoa wa mfano okatika utekelezaji wa agizo hilo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment