Kaimu Kamishina wa Fedha na Logistiki wa Jeshi la Polisi ambaye pia ni mlezi wa mikoa ya Kipolisi ya Simiyu, Geita, Kagera, Mara, Mwanza na Tarime, Dhahiri Kidavashari amefanya ziara Agosti 26, 2020 mkoani Simiyu.
Katika
ziara yake amekutana na viongozi na askari wa Jeshi la polisi Viongozi wa Mkoa
ambapo ziara yake ililenga kuangalia utayari wa askari wa jeshi la Polisi
kuelekea katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
"Sisi
kama Jeshi la Polisi tumejipanga katika kuhakikisha kwamba amani na utulivu
unatawala katika kipindi cha kuanzia kampeni mpaka matokeo yanapotangazwa na
nchi inakuwa salama; tunaangalia utayari wa askari wetu katika rasimali watu,
vitendea kazi pamoja na elimu na utayari wa jumla kwa jamii," alisema
Kidavasha.
Pichani
ni kiongozi huyo alipokutana na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga akiwa ameambatana na viongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Simiyu
akiwepo Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu, Henry Mwaibambe.
0 comments:
Post a Comment