Benki ya CRDB imekabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 60 kama mchango wa udhamini wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu, Kanda ya Ziwa Mshariki inayoundwa na mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kuanzia 01 Agosti, 2020 mpaka 08 Agosti, 2020
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo Julai 30, 2020 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya
Ziwa, Bw. Lusingi Sitta amesema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika
kusaidia wakulima ambapo amesema benki hiyo imejipanga katika kuhakikisha kuwa
wakulima wote wa pamba wanapata malipo yao kupitia akaunti za benki ya CRDB.
“Tumehakikisha
kuwa AMCOS zote tumefungua nao akaunti kama CRDB tutahakikisha kwamba kila
mkulima anayeuza pamba yake atalipwa kupitia akaunti yake ya CRDB na tumejipanga
kwamba kila alipo mkulima wa pamba nasi tupo hapo ,” alisema Lusingi.
Aidha,
Lusingi amesema CRDB imefungua tawi lingine katika Wilaya ya Meatu ambapo
amebainisha kuwa benki hiyo imepeleka gari ambalo lina mahitaji yote muhimu
katika utoaji wa huduma na wateja(wananchi ) hivyo wanaweza kupata huduma zote
katika gari hilo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Wakuu wa
Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ameishukuru benki ya CRDB kwa kukubali kuwa
mdhamini Mkuu wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 na kwa namna ambavyo
imekuwa ikiwajali wateja hususani wakulima ambapo imetoa zaidi ya asilimia 60
ya mikopo kwa wanunuzi wa pamba msimu wa mwaka 2019/2020 ili pamba ya wakulima
inunuliwe.
“Kuna
maana kubwa sana kwa CRDB kudhamini maonesho ya nanenane kwa sababu, lengo la
maonesho haya ni kuwasaidia wakulima wa kawaida kwenda kwenye ukulima wa
kisasa, hivyo inapotokea CRDB inajitokeza kusaidia maonesho kufana, inaenda sambamba
na lengo la nchi la kuinua wakulima wadogo wadogo kwenda kwenye ukulima wenye
tija,” alisema Kiswaga.
Wakati
huo huo Kiswaga amewahakikishia viongozi wa benki ya CRDB kuwa serikali
itaendelea kufanya kazi na benki hiyo katika matawi yote huku akitoa wito kwa
viongozi hao kutosita kuwaeleza viongozi wa serikali kila wanapohitaji msaada
katika maeneo mbalimbali.
Katika
hatua nyingine Kiswaga ametoa wito kwa wananchi kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na
Shinyanga inayounda Kanda ya Ziwa Mashariki ya Maonesho ya Nanenane pamoja na
maeneo mengine ndani na nje ya nchi; kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
maonesho ya Nanenane Kitaifa huku akiwahakikishia kuwa maonesho hayo yatakuwa
ya tofauti kuwataka watarajia kuona teknolojia mbalimbali zinazoleta mapinduzi
katika kilimo.
Kauli Mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 ni “KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA
VIONGOZI BORA 2020.”
MWISHO
:- Meneja wa Benki ya
CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta akizungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa
wa Simiyu kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, leo Julai 30, 2020 ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho
ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi Mhe. Festo Kiswaga akizungumza mara baada ya kupokea mfano wa hundi ya
shilingi milioni 60, leo Julai 30, 2020
kitoka kwa Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Bw. Lusingi Sitta ikiwa ni udhamini wa
Benki hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu; Kiswaga
amepokea kwa niaba ya Wakuu wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda
ya Ziwa Mashariki ya Maonesho hayo.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya makabidhiano ya mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, leo Julai 30, 2020 ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu
Meneja wa Benki ya CRDB
Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya makabidhiano ya mfano wa hundi ya shilingi milioni 60, leo Julai 30, 2020 ikiwa ni udhamini wa Benki hiyo katika Maonesho
ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yatakayofanyika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment